BI ZAHARA PART 7||KUMEKUCHA😯

  Рет қаралды 1,084

GendaGenda

GendaGenda

Күн бұрын

Пікірлер: 7
@RuwaydaAlly
@RuwaydaAlly 8 ай бұрын
Hahaha kumbe kuna nyumb mchawi akiingia haon kitu na wachawi kumbe wanasaltian hii kali
@Gendagend
@Gendagend 8 ай бұрын
😅😅😅😅kila mmoja anataka awe Mkuu,
@ZulfaJu-rb9qb
@ZulfaJu-rb9qb 8 ай бұрын
Wa kwanza
@Gendagend
@Gendagend 8 ай бұрын
👏
@Gendagend
@Gendagend 8 ай бұрын
BIBI ZAHARA (Mchawi wa kijiji) SEHEMU YA KUMI NA SABA(17) MTUNZI&MWANDISHI; JODA WA KISSANA MAWASILIANO: 0748862999 ** Malkia aliingia chumbani kwa chacha bila kuogopa,akaanza kusogea karibu na kitanda alichopo chacha. "Usiogope," Malkia Folesi alimwondoa hofu chacha maana anaonekana kuogopa Sana baada ya kumuona malkia ameingia chumbani kwake tena wakiwa peke yake. Ndani ya hiki chumba kulikuwa na kiti kidogo pembeni ya kitanda,kiti kilikuwa kimetengenezwa kwa kutumia fito pamoja na kamba za miti,malkia akakaa juu ya kiti kile akawa anatazamana na chacha. Mwanga hafifu wa taa ya asili ndio ulikuwa unawasaidia malkia folesi na chacha kuonana. Malkia akamtazama chacha machoni kwake kwa sekunde zipatazo kumi,akatabasamu na Kusema. "Leo utabiri unaenda kutimia" Maneno ya malkia folesi yakazidi kumshangaza Sana chacha, inakuwaje malkia aseme siku ya Leo ndiyo utabiri unaenda kutimia?ikabidi amuulize malkia. "Utabiri gani?,"Malkia folesi akakaa vyema kwa ajili ya kumueleza chacha. ** Upande wa pili katika kijiji cha Mashene,wachawi waliingia ndani ya nyumba waliyopo angel, Patricia na Mwita, cha ajabu kila mchawi aliyeingia ndani alikuwa anarudi na jibu lile lile,ilikuwa kila wakiingia ndani wanarudi mikono mitupu,yaani hakuna mchawi amefanikiwa kuwaona angel,Patricia na Mwita. Angel,Patricia na Mwita wamelala ndani,lakini wachawi wakiingia hawaoni chochote, kwa kifupi wachawi hawajafanikiwa kuwaona angel,Patricia na Mwita. Zahara akawa ananusa nusa juu Kama mbuzi,kuna harufu ya binadamu wa kawaida alikuwa anainasa kutokea ndani ya nyumba ya Mwita. " inawezekana vipi kusiwe na mtu na wakati nasikia harufu ya Chakula chetu ndani?,"Zahara alikuwa anajiuliza maswali mengi,hakuwa amekosea hata kidogo, ni kweli kuna watu ndani ila hauwezi kuwaona,Mwita amefanya zindiko katika nyumba yake,hauwezi kumuona mpaka yeye aamue. Baba otieno na mama Lucy wakakonyezana kisha mama Lucy akamwambia Zahara. "Mkuu,muda unazidi kwenda, twendeni tukatafute kafara nyingine, hapa tutarudi siku nyingine" Zahara alikuwa na shauku ya kutaka kuingia ndani akajionee mwenyewe, alikuwa anahisi huenda wachawi wenzie watakuwa hawafanyi ukaguzi vizuri kwa sababu hii siyo kawaida,anahisi harufu ya watu lakini hawaonekani. Mama Lucy akazidi kumuomba zajsra waachane na hii nyumba ya Mwita mpaka siku nyingine. "Mkuu,achana na hii nyumba, twendeni tukatoe kafara sehemu nyingine," Mama Lucy alikuwa anambembeleza Zahara. Zahara akapiga moyo konde "Basi sawa,kila mmoja achukue usafiri wake" Kila mchawi akachukua ungo wake,wakapanda juu ya ungo na kuanza kupaa,wachawi walipaa na kuiacha nyumba ya Mwita,walitumia mkia wa fisi Kama usukani wa kuongozea vyombo vyao vya usafiri. Mwita akiwa amejilaza chali kitandani,akafumbua macho huku akitabasamu,kumbe wakati wachawi wanaingia ndani kwake alikuwa macho, Mwita akasema kwa sauti ya chini. "Zamu yenu inakuja,endeleeni kunichokonoa tu," Mwita alipomaliza kutamka maneno yale akafumba tena macho kwa ajili ya kuutafuta usingizi. ** Katika kijiji cha watu wafupi,malkia folesi alikuwa bado yupo chumbani na chacha,maongezi yao hayakuwa mazuri kwani,chacha alionekana kutokukubaliana na alichoambiwa na malkia. Chacha akasema "Siwezi kumsaliti mke wangu kwa sababu za kijinga,tangu lini Mimi nikawa nasubiriwa na mizimu ya kwenu?Mimi nahusika vipi na nyie kukumbwa na ukame,?"chacha aliongea kwa jaziba Sana. Malkia folesi akamwambia " mizimu ya kijiji chetu ndio iliyokuchagua wewe na mke wako,nyie ni watu ambalo mtaweza kutusaidia sisi dhidi ya changamoto tunazopitia,himaya yetu imekumbwa na ukame kwa sasa,asali imekuwa chache,"Malkia aliongea maneno yale kwa sauti iliyojaa maombi ndani yake. Chacha akavuta na kushusha pumzi, kuna jambo ambalo kaambiwa alifanye ili awasaidie wanakijiji wote waliopo katika himaya hii,ila chacha hataki kufanya kitu anachoambiwa kufanya,amesema hataki kumsaliti mke wake.
@Gendagend
@Gendagend 8 ай бұрын
17c Baba otieno akadakia "Swadaktaa...umeanza kunipata maana yangu vyema" "Ndiyo,si unajua ndege wafananao huruka kundi moja?," Mama Lucy akawa anashika Shika kidevu cha baba otieno, kidevu ambacho ndevu zake zimekomaa Sana. Baba otieno akamwambia mama Lucy "Lengo la kumwambia Zahara tutoe kafara sita ni ili tuweze kumfanya akosee masharti,lazima atakosea tu kwa sababu huyu bado ni Mtoto mdogo Sana katika uchawi,hawezi kutuzidi sisi,sisi ni wakongwe" Mama Lucy akambusu baba otieno juu ya paji lake la uso,akasema. "Lakini najaribu kuwaza,vipi akikataa kuachia ngazi?" "Hahaha..akikataa atapatiwa adhabu na mizimu,atageuzwa kuwa msukule na yeye, hahaha," Baba otieno aliongea kwa Furaha. Baba otieno na mama Lucy, mpango wao ni kumdondosha zahara kwa kumbadilishia vifaa vya kutolea kafara,hivyo basi,baada ya Zahara kuruhusu wachawi waingie ndani ya nyumba wa kwa ajili ya kuandaa kafara,baba otieno na mama Lucy wakachukua kisu na chungu kingine tofauti na vile vinavyotakiwa kutumika katika aina hii ya kafara. Baba otieno na mama Lucy wanajiandaa kuingia ndani,wakishaingia wataenda kuandaa Mazingira ya kafara ikiwa ni pamoja na kuangalia uzito wa kiroho kwa mtu wanayetaka kumtoa kafara,endapo akiwa na nguvu basi watamuita Mkuu wao. Baba otieno alibeba kisu halafu mama Lucy akabeba chungu cha kutolea kafara, wawili hawa wanajiandaa kuingia ndani kwenda kumuandalia 'Bomu' Zahara. Zahara hakuwa anafahamu kama kuna mchezo mchafu ambao anafanyiwa na wachawi wenzie,uchu wa madaraka ndio umewafanya baba otieno na mama Lucy kutaka kumpindua Zahara na Bibi yake,lengo Lao wanataka wauchukue uchawi wa bi Zahara kisha wawe wachawi wakubwa kanda ya ziwa na sehemu zote ambazo uchawi wa bi Zahara umekuwa gumzo. TBC....
@Gendagend
@Gendagend 8 ай бұрын
17b Zahara akapiga moyo konde "Basi sawa,kila mmoja achukue usafiri wake" Kila mchawi akachukua ungo wake,wakapanda juu ya ungo na kuanza kupaa,wachawi walipaa na kuiacha nyumba ya Mwita,walitumia mkia wa fisi Kama usukani wa kuongozea vyombo vyao vya usafiri. Mwita akiwa amejilaza chali kitandani,akafumbua macho huku akitabasamu,kumbe wakati wachawi wanaingia ndani kwake alikuwa macho, Mwita akasema kwa sauti ya chini. "Zamu yenu inakuja,endeleeni kunichokonoa tu," Mwita alipomaliza kutamka maneno yale akafumba tena macho kwa ajili ya kuutafuta usingizi. ** Katika kijiji cha watu wafupi,malkia folesi alikuwa bado yupo chumbani na chacha,maongezi yao hayakuwa mazuri kwani,chacha alionekana kutokukubaliana na alichoambiwa na malkia. Chacha akasema "Siwezi kumsaliti mke wangu kwa sababu za kijinga,tangu lini Mimi nikawa nasubiriwa na mizimu ya kwenu?Mimi nahusika vipi na nyie kukumbwa na ukame,?"chacha aliongea kwa jaziba Sana. Malkia folesi akamwambia " mizimu ya kijiji chetu ndio iliyokuchagua wewe na mke wako,nyie ni watu ambalo mtaweza kutusaidia sisi dhidi ya changamoto tunazopitia,himaya yetu imekumbwa na ukame kwa sasa,asali imekuwa chache,"Malkia aliongea maneno yale kwa sauti iliyojaa maombi ndani yake. Chacha akavuta na kushusha pumzi, kuna jambo ambalo kaambiwa alifanye ili awasaidie wanakijiji wote waliopo katika himaya hii,ila chacha hataki kufanya kitu anachoambiwa kufanya,amesema hataki kumsaliti mke wake. "Mimi Siwezi kwakweli,naombeni mnirudishe katika maisha ya kawaida ,nataka kumpeleka mke wangu hospitali" Chacha alimuomba Sana Malkia folesi awarudishe katika maisha ya kawaida. Malkia folesi hakujibu chochote, akageuza shingo kushoto, macho yake yakatazama ukutani,ukuta ulikuwa ni mweusi kutokana na Giza lililopo,folesi akatamka maneno kadhaa huku akiwa anautazama ukuta,palepale kuna video ambayo ikawa inaonekana. Chacha akaonekana kuyatoa macho wakati alipokuwa anatazama video ambayo imewekwa na malkia folesi ukutani,haikuwa inafahamika ni vidio ya namna gani ambayo inaonekana mbele ya chacha,kwa muonekano wa sura aliouonyesha chacha bila Shaka ni jambo ambalo limemgusa moja kwa moja. Malkia akasema "Tazama kwa umakini,ukiwa tayari kufanya kazi na sisi karibu sana". Tukio la namna hii lilikuwa linaendelea pia katika chumba ambacho miss chacha alipatiwa kwa ajili ya mapumziko usiku wa Leo,mfalme Nzunda alikuwa chumbani kwa miss chacha,na yeye inaonekana kuna vidio ambayo amemuwekea mke wa chacha,matukio yamfanano yanaendelea kwa pamoja,mfalme Nzunda yupo na mke wa chacha,halafu chacha yupo na mke wa mfalme. Mfalme Nzunda akamwambia mke wa chacha " ukiwa tayari kunisaidia ,na Mimi nitakusaidia,"Mfalme Nzunda akasimama na kuanza kutoka nje ya chumba cha miss chacha,inavyoonekana kuna jambo ambalo linaendelea. ** Kilinge cha manjunju kikaendelea Kuzunguka nyumba moja baada ya nyingine,kuna nyumba zingine zilikuwa zimewekewa uzio wa kichawi,hivyo haikuwa kazi rahisi kupenya na kuingia ndani,kuna baadhi ya nyumba wanafamilia walikuwa ni watu wa kusali na kuswali,hata hapo ilikuwa ngumu kwa wachawi kuingia kiholela,kuingia kwao ni mpaka wajipange vyema. Hatimaye, msafara wa wachawi ukawa umefika nje ya nyumba ya Mzee mmoja wa busara,wachawi wakaandaa vifaa vyao vya kutolea kafara, walikuwa na kisu,chungu kidogo cheusi pamoja na kitambaa maalumu chenye rangi nyekundu,wachawi wakawa wanamsubiri Zahara atoe amri ya kuingia ndani, wakati Zahara anajiandaa kuwa-amru wachawi wake waingie ndani,Baba otieno na mama Lucy walikuwa wanatabasamu kwa mbali,bila Shaka,mpango wao wa kumdondosha Zahara unaanzia hapa. ** Chacha alionekana akiwa chumbani peke yake, malkia folesi ameshaondoka na kumuachia chacha maswali mengi kichwani kwake,hali hii haikuwa Upande wake tu,hata kwa mke wake alishindwa kabisa kupata usingizi kutokana na mambo ambayo wameelezwa,kuna kitu ambacho Mfalme Nzunda na mke wake walienda kuwaeleza chacha na mke wake,haifahamiki ni jambo gani ambalo linaendelea mpaka sasa. Chacha aliongea peke yake. "Hii inawezekana vipi?kwamba kufika Kwangu hapa ilitabiriwa?na kwanini niwe Mimi?huu ukame wanaouzungumzia ni ukame gani?mbona niliona kijiji kikiwa kimeshamiri uoto wa asili,tena uoto ulio na matunda ya kutosha? Sasa huu ukame ni ukame gani?," Chacha alikuwa anawaza na asipate majibu,malkia kamwambia kuwa,yeye na mke wake Chacha walitabiriwa Kama watafika hapa,na lengo la wao kuwa katika kijiji cha watu wafupi ni kutimiza Yale yote yaliyokuwa yanasubiriwa kwa hamu. Sasa basi,kuna jambo ambalo Chacha na mke wake wameambiwa,vilevile kuna video ya kichawi walionyeshwa ukutani,mpaka sasa haifahamiki ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaonekana mbele ya mboni za macho yao. Upande wa mke wa chacha,alikuwa anaongea peke yake chumbani. "Tulikuwa tunaelekea kijiji cha jirani kupata matibabu,hii inawezekana vipi tufike hapa,tena inasemekana Mimi na mume wangu tulikuwa tunasubiriwa kwa hamu?mbona sielewi?," Mke wa chacha aliendelea kuwaza. ** "Mkuu,tumekaa hapa nje kwa takribani dakika tano,lakini unaonekana kukaa kimya kwa muda mrefu,toa amri vijana waingie ndani kwa ajili ya kutoa kafara," hayo yalikuwa ni maneno ya baba otieno baada ya kumuona Zahara amesimama kimya pasipo kutoa amri kwa wachawi wenzake. Zahara akaendelea kubaki kimya huku akiitazama nyumba wanayotaka kwenda kutoa kafara,akavuta pumzi na Kusema "Wawili waingie ndani kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kutoa kafara," Zahara aliongea maneno yale kwa sauti ya chini,baada ya kutamka maneno hayo,baba otieno na mama Lucy wakatazamana kwa Furaha,walifurahi maana mpango wao unaenda kutimia. ** TURUDI NYUMA {Siku ya Jana} Baba otieno na mama Lucy kuna jambo la siri ambalo walilipanga,mpango wao waliuweka nyumbani kwa mama Lucy wakiwa wanapata Chakula cha jioni,mara ya mwisho baba otieno alikuwa anamponda mke wake na kumuita mbweha, walipomaliza kupata Chakula ,mama Lucy alimuuliza baba otieno. "Zahara amekubali kutoa kafara za watu sita,lakini nashindwa kuelewa tutam-malizaje!" Mama Lucy aliuliza swali lake huku akikaa juu ya mapaja ya baba otieno. Baba otieno akawa amekishika kiuno cha mama Lucy, akasema "Mpango wangu ni huu,kwa kawaida kafara yoyote ile lazima ifanyiwe maandalizi,na wanaohusika na kufanya maandalizi kwa mwezi huu ni Mimi na wewe," Baba otieno akavuta kwanza pumzi kisha akaendelea Kusema. "..Mimi na wewe ndio ambao tuna mamlaka ya kuandaa kafara kabla ya Mkuu na watu wengine kuingia ndani,hapo ndio mpango wetu utaanzia" Mama Lucy akamuuliza baba otieno "Mpaka sasa sijakuelewa, tutawezaje kumuangamiza Zahara?" Baba otieno akaachia kicheko cha dharau. "Hahaha...inamaana mpaka sasa bado haujanipata?" "Ndiyo,ningekuwa nimekupata wala nisingeuliza" Baba otieno akaachia tabasamu "Basi sawa,ngoja nikukumbushe jambo moja,kwa kawaida ,kafara ya mwezi wa sita huwa tunaitoa kwa malengo maalumu ikiwemo kupata nguvu,na huwa tunatumia kisu pamoja na chungu maalumu, endapo ukichanganya kisu na chungu ya damu basi aliyehusika na kutoa kafara atashushwa cheo na mizimu" Mama Lucy akafurahishwa na wazo la baba otieno. "Wazo zuri Sana,nimeanza kukuelewa taratibu, sisi tunazamu ya kuingia wa kwanza katika nyumba ya kutolea kafara,lengo lako tukabadilishe vifaa vya kutolea kafara,tukiweka kisu na chungu tofauti na hiki basi Zahara atashushwa cheo,na mtu anayeenda kurithi ni wewe,ukirithi wewe ni Kama nimerithi mimi"," Mama Lucy aliongea maneno Yale kwa Furaha tele.
BI ZAHARA | PART 9 |KIJIJI NDANI YA MTI?
23:31
GendaGenda
Рет қаралды 1 М.
Don’t Choose The Wrong Box 😱
00:41
Topper Guild
Рет қаралды 62 МЛН
Леон киллер и Оля Полякова 😹
00:42
Канал Смеха
Рет қаралды 4,7 МЛН
“Don’t stop the chances.”
00:44
ISSEI / いっせい
Рет қаралды 62 МЛН
MANYANG'AU WAMEHUSIKA NA KIFO CHA RAIS WETU MPENDWA EBRAHIM RAIS WA IRAN
12:35
UKUU WA MWAFRIKA (IBM)
Рет қаралды 26 М.
Frågor och svar
7:50
SFI Annika
Рет қаралды 11 М.
PENDO | TRUE STORY | LOVE & LIFE STORY
2:03:58
LUCAS LUMBASI SIMULIZI
Рет қаралды 21 М.
DAVINA - 11/14 (Season III) SIMULIZI ZA UPELELEZI BY FELIX MWENDA.
1:04:01
MFAHAMU MC MBONEKA MZEE WA 'IRUDIWE'
30:01
Azam TV
Рет қаралды 21 М.
WANAWAKE MJITUME VYA BURE VITAWAPONZA 😂😂😂
6:58
Said Twaha
Рет қаралды 4,7 М.
Sitaki Sitaki
9:04
Malika - Topic
Рет қаралды 54 М.
BI ZAHARA |PART 10|WANAFANYA MAMBO YA KIKUBWA KABURINI
46:05
GendaGenda
Рет қаралды 1,4 М.