Рет қаралды 667
Bunge la Tanzania limeombwa kufanya kikao cha dharura kujadili na kuishauri Serikali kuhusu hatua inazoweza kuchukua baada ya Serikali ya Marekani kusitisha kwa muda misaada yake kwa nchi mbalimbali ikiwemo ya dawa za kufubaza makali ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi.
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa maelekezo ya kusitishwa kwa misaada ya nchi hiyo kimataifa na tayari kuna hofu hatua hiyo inaweza kuhatarisha mamilioni ya watumiaji wa dawa hizo nchini na ndiyo sababu Bunge limeombwa kuingilia kati kama inavyoeleza taarifa hii.
#AzamTVUpdates #Azamnewsupdates
✍Warda John
Mhariri | @official_jennifersumi