Mama Faima, hao watoto hawajafa. Fanya bidii uwatafute, utawapata. Pole sana.
@HotDramasOfficially5 жыл бұрын
Gonga like kama unamkubali geah
@leylahley35425 жыл бұрын
Pole dada...mshukuru allah kwa kila jambo..lakini usikate tamaa rudi katika kitabu kitakatifu Quran..Nabii ibrahim hakukata tamaa hata baada ya kuambiwa yusuf na kakake wote wamepotea ameliwa na mmbwa mwitu yusuf..aliendelea kumwamini mungu kuwa ipo siku watoto wake wote watarudi..nakweli nabii ibrahim (A.w) aliwaona wanae ingawa ni kwa mda mrefu..kuw na imani huku ukimwomba allah huenda hawakufa wanao wapo hai.
@SalimSalim-cx1og4 жыл бұрын
ama kweli umesubiri innah ALLAHA maa sabireen.ALLAH atakuwezesha kupata watoto wako
@asiazuberi97225 жыл бұрын
😭😭😭😭pole sana dada wallah ss wanawake tunapitia magumu jamani wanawake wenzangu tuzidisheni dua tupate wanaume wenye hofu ya mungu khaa kila kukicha hafadhali ya jana mpka naogopa kuolewa
@rahmakawtharylupande69725 жыл бұрын
Na inakuaje mwanaume mwenye sifa mbaya anahitaji kuoa mwanamke mwenye tabia nzuri??
@rahmakawtharylupande69725 жыл бұрын
Yaani nawachukia sana wanaume washenzi kama huyu.hawa ni wa kuua tu.
@khdijaahmed84585 жыл бұрын
Kheri inshaallah my
@mesabendo75815 жыл бұрын
@@rahmakawtharylupande6972 kweli wakufa tu
@ericalexandre21662 жыл бұрын
Wanaume wenye hofu ya Mungu ipi tena maana nyinyi hata kama mwanaume ni jambazi ao hamumjui mradi tu ni wa dini yenu nyie munaolewa nae.
@azdatuppazdatupp2865 жыл бұрын
jaman hii story inasikitisha sana pole sana mama fahma mungu yupo ipo siku tu utamuona mwanao
@aisharamadhan52575 жыл бұрын
Toba lillah wanaume jamenii kueni wenye utuu mama analia hadi nami machozi yananitoka nimeumia sana
@dottocharles16365 жыл бұрын
Jamani huyu mama msimtukane kabisa .watoto wanatufanya tuvumilie mengi , yani ukifikilia swalalakuondoka ukimtizama mtoto unajipa moyo ngoja nivumilie yataisha .
@maryamkhamfar40295 жыл бұрын
Wee vumilia magunia ya mkaa mawili yanakusubiri, yaliyonikuta kwa kuangalia maslahi ya watoto siwezi hata kunyanyua mdomo nikamwambia mwanamke mwenzangu avumilie sbb ya watoto.....bora mtu uondoke ukaanze kuuza maandazi na sambusa kuliko kuja kufikwa na mabalaa
@zahrakmuamir71445 жыл бұрын
Unaangalia na sehemu yenyewe ya kuvumilia mtu haeleweki unamvumilia nn sa
@kalssambaboo97055 жыл бұрын
Sana mamy utajikuta unaumia ukitazama wanao unaona uvumilie tuuh
@joycejohn77545 жыл бұрын
Knaumiza sana jmana! Tunavumilia meng coz of watotot kumbe tunaumia
@azizaz16285 жыл бұрын
Wako wapi Sasa Hao watoto aliyovumiliya kwa ajiri yao?.
@muneerfawzi80265 жыл бұрын
Sijui ni mimi tu peke yangu machoz yamenitoka au kuna wengine
@zakiaulembo31554 жыл бұрын
Namm yananitoka ndg yng
@samiraabdimahamed44493 жыл бұрын
Lakini jamani uache watoto mpaka miaka 23? Week moja enyewe siwezi
@shazminefeysal69515 жыл бұрын
geah asante kwa heka heka hii tumejifunza love u geah
@happymwasyeba72605 жыл бұрын
Pole sana mwanamke mwenzangu
@shanimohamed92675 жыл бұрын
Mke wa mshenga anajua kinachoendelea akibanwa ataeleza ukweli,pole mama fahima.
@fatumaabdallah5665 жыл бұрын
Isee sie waolewaji tuwe makini mno na hawa waoaji loooh, hii habar imeniliza namuhulumia iyo mama faima maskini ya Mungu yani Mungu amlaani iyo mke mdogo na uyo mumewe aliekufa uongouongo na usikute hakuna alie kufa ndio maana havieleweki wanataka tu kumdhurumu huyu mama watoto wake😭😭😭. Mungu walaani hao mtu na mkewe kwa kufanya unyama huu na wanatumia mwamvuli wa dini kuficha maovu yao nawachukia mimi viumbe wa namna hii hasa hawa wanajifanya sunni wengi ni wanafki sunni wa kweli ni wachache mno Allah inusuru dini yetu ya kiislam na waja wanamna hii loooh. Unaoa mke zaid ya mmoja unajua kabisa uezi kuwamudu zaid ya kulala nao haki ikowapi hapo jamani kweli Allah ndivyo alivyoagiza mbona mnambindua mambo juu chini nyie baadhi ya wanaume wanafki mnaojifichia kwenye uswali sunni Mungu awalaani maisha yenu yote mpaka mfanye toba laaha sivyo muangamizwe kwa laana yake wanafki wakubwa nyie.
@sophiakassim67845 жыл бұрын
Kweli kabisa dada wengi wanatia doa uislam hasa wa kisunni
@wemakalamu35385 жыл бұрын
Gear habibu lifanyie kazi hilo neno mwenyeezi mungu atakulipa mema hapo na penginepo imeniuma sana
@eshaomari6363 Жыл бұрын
Kwanza polee geah kwa kazi nzitoo nadada pole kwa mazito mungu akupe subra lkn utapata kilicho chako ipo siku
@ladymashaallahilikeuaadvis9975 жыл бұрын
Daa geah msaidiye mm nakuamini kwa hekaheka kama hizi ,dadako kutoka kenya
@faizabaishe51725 жыл бұрын
Alhamdulilah, pole sana mungu akupe subra na imani katika Jambo hili la huzuni InshAllah heri.
@merryn48915 жыл бұрын
Pole sana Dada mwenyezi mungu akupe ujasiri
@autorichdiagnosis36325 жыл бұрын
Dah Maisha mengine yana uzembe. E MUNGU tusaidie
@sharifamustafa47935 жыл бұрын
Yarabi mjaaliye huyu mwanammke awapate watoto wake kwa rehma zako mwanamme ni mshenzi sana na huyo mkewe kuiba watoto wa mwenziwe
@wardaabasi65585 жыл бұрын
Allah ampe sabr huyu mama. Wanawake hatujaambiwa kama ndoa ni sabr tu. Tumeambiwa kama kwenye ndoa tuwe na mapenzi na huruma ( mawaddah warahma ) hivi ndio Ayah inavyosema. Kweli kumpiga mke na kumnyanyasa hayo mapenzi na huruma iko wapi? Sikatai Allah hakukosea aliposema oweni wawili watatu hadi wanne na kama mtaghofia kutofanya uadilifu basi bakini na mmoja!!! Imeandikwa hivyo kwa maana. Leo wanaume wengi hawatizami uadilifu. Uadilifu sio kitanda tu!! Bali na mambo mengine. Leo uwezo huna unang"ang'ania kuongeza mke. Ikisha baadhi ya wanaume huleta ile hadith ya kumsingizia Mtume. Kwamba kasema kila maisha yakiwa magumu ongeza mke mwengine. Baadae maisha yatakuwa mazuri. Wameitolea wapi? Mtume wetu anatupenda sana na naamini hatutakii mambaya Ummah wake. Na huyo mke wa mshenga mnafiki. Yeye kasema hapo alijua habari ya kwamba watoto wamechukuliqa. Kwa nini alipokuja huyo mama wa kambo na fahima kwake, hakufanya mbinu za kuwafanya wasubiri hapo kwake akawaita polisi bila wao kujua.. Samahanini kwa long message
@wemasamy66165 жыл бұрын
Da geah huyu Dada mshenga akamatwe mapema kabla hajatoroka ,, inaonekana kunamchezo hapo ,,
@gracechalagwa97455 жыл бұрын
Huyu mwanamke akili yake sio nzuri, miaka yote hiyo watoto wapo hapa tanzania asijue walipo watoto
@zuweinaalhabsya87735 жыл бұрын
Hana kweli yaaan a nashangaza kweli.
@ummusamira35185 жыл бұрын
Kajitahidi ila nimnyonge sana na kila kitu mmh Allah atanisaidia bila ya yeye kujishughulisha LA lolote
@happyrichards3195 жыл бұрын
Tatizo hapewi ushirikiano hata na vyombo vyetu vya usalama.. Unaniambia ingekuwa watoto wa matajiri wasingepatikana????
@TheSalma19995 жыл бұрын
Grace Chalagwa umeona eh
@mangisenya40124 жыл бұрын
Hapo kwenye mimba ya tatu ndipo ulipofeli dada. Upole una mwisho wake dada,angalia mustakabali wa maisha yako
@khadijasalum23025 жыл бұрын
Pole sana mama Allah atakulipia kesho kwa mungu huyo mume na mke mwenzako watayaona waloyafanya na subra ulikuwa unao maa shaa allah
@faaali2445 жыл бұрын
Pole sana kwa yalokukuta hio ni jumla ya mitihani Allah akufanyie wepesi ameen
@zahrakmuamir71445 жыл бұрын
Yaani na kipigo tena.ila una moyo we dada mm tusingefika huko kote
@safiaothman5175 Жыл бұрын
Laana za Mwenyezi Mungu Subhaanahu Wata'ala ziwashukie huyo mume na mkewe ,Aamiin.
@bintiiddy70435 жыл бұрын
Jaman sasa Hao watoto aliwauwa ama INNALLAHI WAINNAILLAHI RAJIUN 😭😭😭😭😭😭SHIKAMOO NDOA ZAKUOLEWA NA WANAUME WASIO JITAMBUWA JITAMBUWA
@maryisdory60285 жыл бұрын
Huwez kumjua mpenzi, lakn pia Ndoa za kiislamu zina ukandamizaji wa kijinsia Kwa wanawake yani wanakua hawana haki mbele za waume zao tofauti na ukristo.
@fatmam19975 жыл бұрын
@@maryisdory6028 ujk ugh n j bh hybrid yii i h h unlinkuhjhbnjkkjjhjjj j
@ahluljazira22595 жыл бұрын
@@maryisdory6028 usiongee usilolijua Baki na dini yako lakin jarib kuonesha heshima Kwa dini za wenzio
@AminaAhmed9995 жыл бұрын
@@maryisdory6028 hapana mary hawa hawaujui uislam wao. uislam unaruhusu mtu aoe zaidi ya mke mmoja pale ambapo anauwezo. na ni haki ya mke kupewa makazi malazi na mavazi. na wala si haki kuwachanganya wake wenza nyumba moja . kwa ufupi hayo yote waliyofanya ni kinyume na maadili ya kiislam. watu wangefata maamrisho ya dini ya kiislaam .basi mke angekuwa ni zaidi ya queen. watu wasome dini yao wajue haki wataishi maisha mazuri
@remiomar71545 жыл бұрын
Hili nifunzo kubwa Sana kwetu sisi watoto wakike kuolewa n mtu usiyejuwa kwao wala kushikamana n ndugu wamume ni mtihani mkubwa... Mm ndio maana mamangu akiwa mtu kaja tuu ataka mke humkatalia ikiwa kama n wanchi y mbali naistoshe wazazi w mume hawajuwi natumia nikiwa matatizo kama haya ukifikwa n jambo hujuwi nani atakupa ukweli...... Kama watoto wapo utawapata tuu damu n nzito kuliko maji mungu atawabaini ilakikubwa hao washenga ndio watasema ukweli watakapo shikwa ukweli wanaujuwa
@salamasalama39555 жыл бұрын
Pole sana dada😢 YARAB TUJAALIE WANAUME WENYE UPENDO NA IMAN NASIE 🙇
@likimaro65 жыл бұрын
Huyu mama Sele mbona anajichanganya maelezo? Ukimsikiliza mstari kwa mstari utaona kuna kitu anaficha. Labda kwa kujihami au kwa kujua kitu.
@salamasalama39555 жыл бұрын
@@likimaro6 Hamna bali niuchungu alionao nandio mana hatawanachokiongea hakina mpangilio
@abrahmaniomar98585 жыл бұрын
@@likimaro6 yaani wewe zaidi ya shetani, Huyu mama anateseka miaka 13.
@likimaro65 жыл бұрын
@@abrahmaniomar9858 wewe taahira umesikiliza mahojiano au unakurupuka? Mama Sele ni huyu aliyehojiwa mwishoni. Ujue mnakurupuka hata hamuelewi stori mmekaa kimbeambea. Mama Sele ni huyu anayehojiwa mwisho
@likimaro65 жыл бұрын
@@salamasalama3955 mama Sele ni huyu mshenga, hebu tulizeni akili mkisikiliza jambo jamani
@estheradriel98295 жыл бұрын
Huyo mshenga, huyo mama akamatwe aeleze anayajuwa yote, na siajabu ni ndugu yake anamfichia siri, utakuwaje mshenga kwa mtu usie mjua
@tumainimango81405 жыл бұрын
esther adrielambele2010 huyu mshenga anajua kila kitu
@mimaakenirram14055 жыл бұрын
daaah pole sana dd angu mungu atafanya wepesi utapata wanao lnshallha mm nilichogundua huyu mama sele atakuwa anajua alipo huyo fatma na huyo fatma atakuwa kamjaza maneno faima ata asiwe na wazo la kumulizia mama ake maana aliondoka akiwa na miaka kumi na tatu lazima atakuwa anamkumbuka mama ake hira damu ya mtu aipotei atawapata tu huyo mke mweza anawataka yeye ndo mana usikute ata watt awajakufa
@yuusufnuur57525 жыл бұрын
Nskusii dadaa mwajuma mungu h a kupe subra na fatilia hadi poolisi atafutwe huyo jaribu ssna huyo mshenga mkamate uende nae kotini haongee ukweli usiwe mkimya wakamate wote kwsnini dada ulikaa miakayotee wawaza nini hasaa wewe kama nzazi wawatoto pole sanaa ila pigania hao watoto kwa kila njia kama ni d à m yako utawapata insha Allah
@zakiaulembo31554 жыл бұрын
Daaah dada yng mwajuma nakusiliza roho inaniuma machozi yananitoka mana ilo tatizo la fayma tunalijua miaka mingi sana ila tuseme Allahmdulillah mungu atatenda mema inshallah
@gretagonga29665 жыл бұрын
kwanini uliendelea kuzaa nae wakati unajua siyo mtu mzuri???
@devothamedia51775 жыл бұрын
Kabisa anazidi kuzaa
@agriparose39425 жыл бұрын
greta gonga amenikera hapo tu
@nurudovino2885 жыл бұрын
Mungu wangu mbaka Inanitisha kuorewa loooh
@lifeandotherstuff58995 жыл бұрын
Plaxcidia Renatuh hata Kama ni mume wake kunakitu kinaitwa uzazi wa mpango
@happyrichards3195 жыл бұрын
Kwani mumeo huwezi kutumia kinga, kwa hiyo km ana magonjwa ya zinaa akuambukize tu kwa sababu ni mumeo. Kutumia kinga kunaepusha hata mimba zisizotarajiwa......
@fauzal52575 жыл бұрын
Anaejua wanaume pasua kijwa gonga laki apa
@mspwjjjso62612 жыл бұрын
Daah ,umenikumbusha maisha mama yangu maisha alitulea .
@selemanimkonga81505 жыл бұрын
Nimejifunza vingi kwenye hii habari ila tuendelee kuwatafuta watoto
@husnauthman76095 жыл бұрын
Daaar
@shababygirlshambuwa83885 жыл бұрын
duuu pole sana mwanamke mwenzangu mm yalinikuta hayo ila nashkuru nilipata msaada mkubwa kwa polis nasasa watoto nipo nao alhamdulilah na maisha yangu mazuri tu. alhamdulilah
@nafisamohamad31825 жыл бұрын
Naomba unijulishe Ulitumia njia gani ndio ikakusaidia kupata wanao plz nielekeze huo utaratibu niufuate dada waeza nisaidia coz watto wangu pia nimepokonywa nahitaji kuwachukua lkni sijui nifanyeje?
@shababygirlshambuwa83885 жыл бұрын
Nafisa Mohamad nilipokuwa nimeolewa hapakuwa mbali na anapo kaa wazazi wangu km mail tatu watoto wangu walichukuliwa wakiwa wadogo mmoja miaka miwili mmoja miezi minne hawakuja kuniomba walinihadaa wakasema wanaenda kuwasalimia jamaa zao wa kipemba na alikuja wifi yangu sikubisha aliwachukua wote wawili Dada masaa yalienda watoto hawajarudi sio mchezo siku zikaenda hatimae ikafika siku ya pili tumbo la uzazi linaniuma watoto wangu hasa yule mdogo wa miezi nilizidi kumuomba Allah tukenda kuwadai watoto hawapo tukiulizia tunaambiwa wamesafirishwa pemba Dada umasikini nilokuwa nao hakuna alonisikiliza nilikuwa nalia utasema nimefiwa polisi nimeenda ila haijawa kitu kwasababu baba wa watoto anapesa analishia polisi niliamini iPo siku Haki itapatikana hatimae ikatimia mwezi bila kujua watoto walipo Dada nilishauriwa niende nikafanyekazi ili nipoteze stress nikaenda oman nimekaa miaka miwili bila kuwaona watoto wangu wala kujua taarifa zao nilirudi omn sasa nikawa nnanguvu pesa si nnayo hahahaha ukiwa na pesa kila kitu rahisi tukaanza mchakato wa kuwatafuta watoto tukenda polisi tukatoa maelezo bwana akaitwa hayupo wala mawasiliano hayapo ila wazazi wake wapo alienda kuchukuliwa mamaake akawekwa ndani akaambiwa haachiwi mpaka mtoto wake aje wiki mbili zikakatika yatatu ndio bwana akaja polisi mamaake akatolewa ila alichoka sana hahahaha polisi hakuna bwana
@shababygirlshambuwa83885 жыл бұрын
Nafisa Mohamad tukenda mahakamani akaulizwa watoto walipo hakusema akarudishwa ndani kesi yake ikawa ameandikwa tuhuma za kutorosha watoto. siku ya pili tukenda tena mahakamani ushahidi ukakamilika bwana akasema watoto walipo aliwapeleka kwao pemba mkoani .akaambiwa anapewa siku mbili watoto wawe washarudi .alitafuta hakimu wake ila haikuwa jambo alizidiwa maarifa na hakimu alinisimamia mimi .sikujua kilichoendelea Dada siku ya tarehe ya mahakamani ikafika tukarudi shosti watoto waliletwa wamekuwa wakubwa ila walivokonda utasema wanautapia mlo aaaa kesi ikaenda juu zaidi nilikabiziwa watoto kwakweli nililia sana walikuwa wabaya hatari wamefujika kama vizee vya miaka sabini bwana akaambiwa mahakamani hakuna sheria ya kuchukua watoto wa kike na kuwalea wewe mwanaume pasi na mke .kwa mtoto wa kiume mpaka atimize miaka15 ila mwanamke mpaka 20 awe na akili timamu. ...shosti nilitupa hela kumpa wakili ila watoto wangu nnao .bwana alikaa sero sijui kwa mda gani. mimi nipo na watoto wangu tena wamerudi afya yao. hivi sasa wanasoma na maisha yangu mazuri tu alhamdulilah hawajaja hata familia ya baba wa watoto kuwauliza hali ila mm sijali kwasababu maisha kwa sasa wala hayanipigi chenga tena. dada sinania kwanza ta kuolewa nnamwaka wa Sita sasa. ukiwa na pesa naamini kila kitu unakiweza ktk dunia.
@nafisamohamad31825 жыл бұрын
@@shababygirlshambuwa8388 kweli mm tatizo ni uoga tu nafikiria uko mahakamani sijui nitaanzaje kujieleza lkni nmepanga nkirudi kwetu kenya nianze kufuatilia hio ishu sababu sasa nko dubai nafanya kazi watto wako na baba yao lkni naambiwa nisiwaache watateswa uko ikiwa sipo karibu nao.
@shababygirlshambuwa83885 жыл бұрын
Nafisa Mohamad aaaaaaa ok raha ya watoto walelewe na mama nasio baba kwasababu wanaume hawawezi kulea atawatupa mchana kutwa jioni ndio anarudi hajui ya mchana yanayowakuta watoto na sasa dunia imeharibika
@@annameryladislaus3048 umeona eee mara amwambie mke mwenzie kwanini hujanifulia nguo, mara mume wangu sijui kitu gani,ujue wanaume hawapendi mtu wa kujidekeza na mdomo mdomo juu.
@raniahabdurrahman45565 жыл бұрын
Umeonaeee?
@raniahabdurrahman45565 жыл бұрын
Yy anajua anasaidiwa badala awe mpole anataka ampelekeshe mwenzie eti kisa mume kasema asaidiwe.anawezaje kuuliza mbona hii hujafua? Mwenzie kakasirika sababu aliona anaamrishwa.huyu mkorofi huyuuy
@princessmeggyclement75915 жыл бұрын
Mara mboga ina mimajimaji😂
@nafisamohamad31825 жыл бұрын
Nimejifunza kupitia apa ndio nimejua kweli mwanamke ukiwa unaishi bila kaz nakumtegemea mume tu bc matatizo kama hayo na dharau pia lazma uzipate kwa uyo mume au familia yake😢afadhali niendelee kupambana na waarabu tu uku uku ili nijipatie ridhiki yangu hata nkirudi pia inshallah niwe nimeshajenga kajumba kangu nikapangishe kanilipe kila mwezi ndipo nkipata mwanaume atoeza ninyanyasa kwa kujua mm pia ni mtu nnaeweza kujituma nakuendeleza maisha yangu vizuri tu bila kuhitaji msaada wake.
@rahmabenta83495 жыл бұрын
Kwelii kabisaah ,wanawake tujitafitie cha kwetu jamani ,mambo yakumtegemeaah mwanaume mabaya sana hayaah
@happyrichards3195 жыл бұрын
Pole sana dada... Polisi wasilale wafatilie hili suala km wanao wapo hai ukutanishwe nao, km wamekufa uonyeshwe mahali wamezikwa upate amani..... Lkn pia iwe fundisho kwetu wanawake mwanaume anakupiga, anakunyanyasa, hawezi kukuhudumia unaye tu unasubiria mabadiliko, unasahau km mabadiliko ni ww mwenyewe... Umezaa mtt mmoja unaona bwana haeleweki, uzazi unakula kwa shida, mtt anateseka, hamuwezi kumhudumia inavyotakiwa... Mama unatakiwa uanze uzazi wa mpango na usitishe hayo mahusiano yasiyo na tija... Wanaume wa hivi ndo unakaa naye badae anakuua na kukuzika mwenyewe... Lets wake up jamani
@evachriss59065 жыл бұрын
Uyoo anae ojiwa ni mshengaaa,,,sukuma ndani anajua uyoo ata maongez yak tu anaonyesha anajua kwann uyo faima alivyo fika kwakwe kwann asimwambie mamaake mzazi ,,,wanawake jmn tuwe makin na wanaume mtoto wa kwanz mwanaume vitimbwi wapili bdo upoo watatu kaaaaaah ,,,mbk anakuja iba watatuu
@salhkasmm5583 жыл бұрын
Ulikuwa namoyo wakulalanae tena MTU kamahuyo hongera
mungu akufanyie wepesi😭daah inaumaa siolewi mm😭😭😭pole sana dada geah habib hongera kwa kazi nzur unayofanya
@suddykimindu6025 жыл бұрын
MARY NDEMASI
@oscaroscaroscar79745 жыл бұрын
Huyo mama ana huruma!! mama yake usimpende mtoto wake! umfiche na umuizeshe kimy kimya mahali zote ule wewe ..Iyo inaitwa rohoo mbayaaaaaa dada Mungu Atakusikia kilio chako!..Na kama mwanao akisikia hiii na hakiona lazima Akutafute!
@nasrasalim7112 Жыл бұрын
Ww dada mzembe mateso yote bado unampa na kujiachia
@lamecktheonest2255 жыл бұрын
Jamani samahani stori inasikitisha lakini nimecheka😁😁, eti akanipiga bao taa,,, pole sana dada Mungu muweza yataisha.😢😢
@anastasiasalome4095 жыл бұрын
Wewe😂😂😂😂 eti bao
@kingoman78955 жыл бұрын
Umenisikitisha sana mdogo wangu na pole sana na matatizo ALLAH atakufanyia wepesi Ameen
@jeffmauzo54835 жыл бұрын
Mmmh mtihani pole sana
@wemakalamu35385 жыл бұрын
Duu pole dadaangu mwenyeezi mungu akufanyie wepesi uke wenza balaa jamani hili sote wadada na wamama ni elimu tosha.
@robbyissack85755 жыл бұрын
Pole sana dada,najua machungu unayopitia
@secylovenessadaa42455 жыл бұрын
Pole sana Dada ,yaan kuuliza t wanaume wenye tabia hizo yaan kutesa mtu kama humtak mtt wa watu yanin kuoa ?wake wengi oa mwanamke ubaweza kumtunza ,shamon u
@she_gorjuss4 жыл бұрын
Daah pole dada jamani wanawake tutafuteni pesa 😭being independent is such a good feelings 😭😭😭😭maisha ya kutegemea mwanamme daah so sad
@jackiemasame41852 жыл бұрын
Kweli kabisa aisee
@ahmedalmalki29055 жыл бұрын
😭😭😭pole dada wanatakiwa wakamatwe uyo mume na mshenga wake wote wakamatwe
@madomadolove76435 жыл бұрын
Kabisaaa yani
@madiyamsonde5625 жыл бұрын
pore sana dada ilra tuwchege ujiga jama madeso yote ayo jamani bado unazw tu mimi mweye yalikuta lira nika nakili yagu nivumliya tu mbiba ilvofika mezo 8 nodoka jumbani wakasusa kunipa uduma lira npata msada porisi mpare mwangu nae uduma atowa name nkozao omani masha yanderea kishauona wanume adomeki usmuwache mwanao meba maisha mberkuwambe
@fsaad51164 жыл бұрын
Daaa alikua ashajipanga woow mtihani kweli
@khalidngwembele90754 жыл бұрын
Kama na ww umesikia neno IVO zaidi ya mara buku like hapa 😊😊
@stevemwakisimba59865 жыл бұрын
Uzembe wa hali ya juu sana huu sijawahikuona kwakweli!
@mc_mrope5 жыл бұрын
Mwenyezi MUNGU amsaidie kwa kweli
@mwanatz59805 жыл бұрын
Pole sana dada dah!yanauma sana mungu akusimamie amiin.
@SA-xj8hc5 жыл бұрын
Watu mufanye uzembe kisha mnasingizia dini .! Uislam tofauti na dini nyengine unaruhusu talaka . Quran inasema “oaneni kwa wema na muachane kwa wema”. Huyo jamaa toka hapo mwanzo si mume , huyu mpangaji wenu na mkewe alikulaghai wewe na familia yako na mkakubali kuwasikiliza watu ambao hata wao maisha yao ni ya nyumba za kupanga .Kama wana maarifa wangeweza angalau kumiliki banda lao.
@husnauthman76095 жыл бұрын
Hahaha umesema kweliii
@darajalakidatukilomgi23623 жыл бұрын
Somesheni watoto wa kike, muwawezesha kujitegemea na kujiwezesha, hii kesi yote ni kwa sababu ya kutegemea binadamu mwenzako, huyu Binti umri mdogo nguvu anazo lakini maisha anayoishi ya kizamani enzi za mwaka 47, Amkeni mabinti msome shule mfanye kazi za kujitegemea wenyewe
@portinagodson66945 жыл бұрын
DA GEA HII STORY IMEISHIA WAPI? KAMA HAJAFANIKIWA HUYO MAMA HEBU TUPE NJIA TUSAIDIE HUYO DADA APATE WATOTO WAKE NA HILO LIMWANAUME KAMA LIMEKUFA LIKAFIE MBELE TUTAONANA BAADAE MPUUZI MMOJA HUYO😎
@husnauthman76095 жыл бұрын
Mh
@shazminefeysal69515 жыл бұрын
mmmh wanaume wanatesa jamani ona dada wa watu analia kama mtoto, watoto wakwakwe mnyewe uchungu alipata akajifungua kwa maumivu makali lkn anapolwa watoto kama tonge mdomoni embu jamani tujitahidi kuwa na ubinadamu wanaume. Naomba jamani vyombo husika vimsaidie huyu dada apate watoto wake inshaallah
@beautyme52513 жыл бұрын
Ndoa dini, mimba Uzazi wa mpango nivitu Tofauti ukeweza, kusaidiwa mara 3 ujauzito na Babako nivitu tofauti, kuamini mtu yoyote na watoto ndio Kabisaa big NO
@aminashabani59375 жыл бұрын
Dad wanaume hawa hawana huruma jamani mungu anamuona huyo baba mdogo wa miezi 3 kampeleka wapi jamani inaniuma mnoo
@hawakitoki46775 жыл бұрын
Ee Mungu ndoa hz naogopa kuolewa wanawake tunateseka jmn
@azharmamyummyazhar47155 жыл бұрын
Hawa Kitoki usiogope habpty
@bigpompabig70745 жыл бұрын
Asalaam alkum, kwenye iki kisa, ulitakiwa ujifaam kwanza mnaelekea wapi na umetoka wapi ila mtu yy yote asichukulie advantage kwa misingi ya kiislam.pole sana Allah awalinde wanao na akufanyie wepesi kwa maisha yako magumu sote ni wanyonge.
@hellenkalimba50035 жыл бұрын
Unajua nimeskiliza hii stori mpk mwisho ndo nimegundua kuwa huyu dada na yeye kichwan sio mzima...kwakweli Mungu amsaidie tu
@naimamwaibanje1565 жыл бұрын
Kabisa,kumbe umeona kama mm😁.sasa ww mtu kakufulia nguo kibao kuacha nguo moja tu lawama!!!
@naimamwaibanje1565 жыл бұрын
Kabisaa,hata mm nimeona kama wewe
@janethpallangyo26335 жыл бұрын
Uwezo wake wa kufikiri ndio uliishia hapo- na malezi aliyokulia
@twariatiomary4865 жыл бұрын
Hahaaaaa
@zahrakmuamir71445 жыл бұрын
Mm pia naamini hivyo si mzm na pia kuna mambo mengine amejitengenezea haya mazingira yy mwenyewe
@rosekweka95445 жыл бұрын
Jamani dada pole Sana ni mitihani tu itapita ushauri wangu endelea kuwatafuta usichoke watafute ndugu zake wakakuonyeshe makaburi na vile vyeti vya vifo akuna mtu anaekufa alafu isijulikane pole sana
@sosovele61733 жыл бұрын
Huyu dada hakuwa na jauli nzuri mmhh
@fettyfetty60915 жыл бұрын
Allah amfanyie wepesi inshaallah.
@salimusaid73095 жыл бұрын
Inshaallah
@gracechalagwa97455 жыл бұрын
Huyu mwanamke akili yake sio nzuri
@shammoha52975 жыл бұрын
Ameen!
@aminatashaib16075 жыл бұрын
Mshenga yeye anajua walipo na kl kitu anajuwa pumbavu ahikiliwe huyo huyo kwanini kila akiibuka asikomae akamripoti hata kwamjumbe
@iddijuma36505 жыл бұрын
Dah...pole sana dadangu.....Da Gea i love you.
@hamidaalhabsi85684 жыл бұрын
AMAKWELI kuolewa wanawake mbona tunaipata mungu atusitiri yaarabi
@tausingomeni25685 жыл бұрын
Da gheh tunasubil mrejesho,msaidie jmn huyo dada anatia hata huruma naisi kufata sheria za mume ndio zimemponza
@salmaelhinai8335 жыл бұрын
So sad Allah atakufanyia wepesi
@sofiasofia39085 жыл бұрын
Duuuh pole my dear😭😭😭
@MA-kh2lr5 жыл бұрын
Mshenga na mke wakamatwe... Wanajua kila kitu... Ila walimfanyia uhasidi mama Fahima
@mwashashasaid37005 жыл бұрын
Hilo funzo tujifunze jaman...geah asante nakufatilia sana 254
Mamaeee wanaume WA Tanzania siwataki kabisaa bora nilivyoolewa ulaya yalinikuta haya zamani
@zainamohamedy65155 жыл бұрын
Huyo mama sele ni wakukamatwa akatoe maelezo vizur.mana anajikanyaga mwenyewe kwenye maelezo akamatwe tyuuu
@mariej69622 жыл бұрын
Roho ngumu sana kuanzia huyo mshenga, ndugu wa mume, mwanaume mwenyewe na kila mtu anayejua walipo, na hao polisi kuna wakati wanafanya vitu vya ajabu sana, inakuwaje mhanga akamtafute mtuhumiwa? Hivi mtu yeyote anaweza kulala kabisa usingizi akijua kabisa kuwa mama ameibiwa wanawe, roho gani hizo? Miaka 13 ya mateso makali mno. Pole
@evamlay89975 жыл бұрын
Yani wewe dada nauomba nikutukane kwanza mpumbavu sana unarudisha moyo nyuma kwa huyo mbwa mimi kwa watoto wangu dunia ingejua weeee kakuona poyoyo ningempa krambasi
@tumainimango81405 жыл бұрын
Eva Mlay hahaaa eva
@azizaz16285 жыл бұрын
Cha kushangaza watoto walipochukuliwa hakuwatafuta alipo sikia wamefariki ndiyo kumekucha Sasa anatafuta watoto🤔🤔
@raniahabdurrahman45565 жыл бұрын
😀
@yusrakamili64015 жыл бұрын
Yarab nakuomba hakika we hushindwi na kitu mwanamke mwenzangu na huu mwezi Wa haji amka usiku mwelekee Allah akika utapata watoto wako ile no damu yako na Dada gea chukua sweka ndani hao wanaobabaisha maneno ushungu anao upata hiyo Dada me pia nausikia lkn inshaallah Allah atakufanyia wepes nakufatilia
@ساننبرر5 жыл бұрын
Pole daa
@johanamagesa77094 жыл бұрын
Huo mdada anakosa hata kidogo. Allah kamtumia ili wanawake tujitambuye kuishi na watoto wa mwenzako vinzuri na kutumia mwanamke mwingine ili mine akuprnde.sasa akuzaa Nani kajipotezea muda wake .bwana Yuko mbele ya haki wanawake mmebaki duniani malipo ni hapa hapa akhera mahesabu
@saudaomary86875 жыл бұрын
Pole Sana dada mungu atakusaidia utamwona mwanao fahma na wengine
@lailmeeea49085 жыл бұрын
Mi naona niendelee kuishi msela tu basi mana sio kwa misukosuko hiyo khaaaaah wanaume Mungu anawaona
@rahmstifaallahndiemwenyeku67655 жыл бұрын
Pole sn
@mwalauzimchonga72665 жыл бұрын
Mmmh pole
@giannajoji79445 жыл бұрын
Hivi huyu mdada ana akili kweli??manyanyaso yote hayo bado anatoa dudu la yuyu!haki mi siwezi kabisa!!