WIMBO WA KATIKATI Zab. 80:1-2, 14-15, 17-18 (K) 3 (K) Ee Mungu, uturudishe, uangazishe uso wako nasi tutaokoka. Wewe uchungaye Israeli usikie, Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru. Uziamshe nguvu zako. Uje, utuokoe. (K) Ee Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi, Utazame toka juu uone, uujilie mzabibu huu. Na mche ule ulioupanda Kwa mkono wako wa kuume; Na tawi lile ulilolifanya Kuwa imara kwa nafsi yako. (K) Mkono wako na uwe juu yake Mtu wa mkono wako wa kuume; Juu ya mwanadamu uliyemfanya Kuwa imara kwa nafsi yako; Basi hatutakuacha kwa kurudi nyuma; Utuhuishe nasi tutaliitia jina lako. (K)