No video

FAHAMU UMUHIMU WA MIKATABA YA AJIRA KAZINI

  Рет қаралды 944

WAKILI TV

WAKILI TV

Күн бұрын

Msingi wa uhusiano wa kiajira baina ya mfanyakazi na mwajiri wake ni mkataba wa ajira. Mkataba wa ajira unaweza kuwa wa mdomo au wa maandishi. Ili kuhakikisha mambo ya msingi yanawekwa wazi Sheria inamtaka mwajiri kumpa mfanyakazi maelezo ya ajira yake kwa maandishi baada ya siku sita kuanzia siku ambayo mfanyakazi aliajiriwa, isipokuwa pale ambapo mfanyakazi amepewa mkataba wa maandishi ukiainisha waziwazi mambo hayo. Maelezo hayo ni haya yafuatayo
a. Jina, umri, anuani na jinsi ya mfanyakazi.
b. Mahali pa kuajiriwa,
c. Kazi na maelezo ya kazi yenyewe,
d. Tarehe ya kuanza kazi,
e. Aina na muda wa mkataba
f. Mahali pa kazi
g. Saa za Kazi
h. Ujira, mahesabu ya ujira huo na maelezo kuhusu malipo mengine,
i. Maelezo kuhusu likizo,
j. Jambo lingine lolote ambalo kisheria lazima litolewe maelezo.
Endelea kufuatilia mada hizi hapa katika channel yetu na tufuate katika mitandao ya kijamii
Angalizo: Mabadiliko yoyote ya maelezo ya ajira ni lazima yafanyike baada ya mwajiri kushauriana na mfanyakazi na kumpa taarifa ya mabadiliko hayo kwa maandishi---Mfano ishu ya korona na mambo mengine ambayo ambayo hayawezi kufikiriwa wakati mkataba unaingiwa na pande mbili
Aina za Mikataba ya Ajira
Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini imeigawa mikataba ya ajira katika aina kuu tatu ambazo ni;
a. Mikataba isiyokuwa na muda maalum
b. Mkataba wa muda maalum
c. Mkataba wa kazi maalum
Mikataba Isiyokuwa na Muda Maalum
Mkataba usiokuwa na muda maalum ni mkataba ambao ukomo wa ajira haujatajwa waziwazi. Chini ya mkataba huu mfanyakazi anaweza kuendelea na kazi mpaka kufikia umri wa kustaafu endapo haitatokea sababu yoyote ya kusitisha ajira kabla ya umri huo wa kustaafu.
Mkataba wa Muda Maalum
Mkataba wa Muda Maalum ni mkataba ambao kipindi cha ajira kimewekwa wazi na tarehe ya ukomo wa ajira ipo wazi na inajulikana. Hata hivyo Sheria imeeleza wazi kuwa aina hii ya mkataba itahusu
waledi na wafanyakazi wa kada ya uongozi.
Mkataba wa Kazi Maalum
Mkataba wa Kazi Maalum ni aina nyingine ya mkataba wa muda maalum ambao hutegemea kumalizika kwa kazi na malipo hufanyika kwa siku au baada ya kumalizika kwa kazi husika.
Endelea kufuatilia mfululizo wa mada hii hapa hapa katika channel yetu na tufuate katika mitandao ya kijamii kwa kubofya link hapa chini;
Twitter; / wakilitv
Instagram; / wakili.tv
Linkedin; / waki. .
Facebook: / wakilitv
#IjueSheria #Wakilitv #MikatabaYaAjira

Пікірлер: 2
@omarramadhani767
@omarramadhani767 4 жыл бұрын
Hi
@victaboy7273
@victaboy7273 Жыл бұрын
Kwa company kubwa labda . Lkn mtaani ni balaaa
Inasemaje,  Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini?
6:51
Global TV Online
Рет қаралды 3,4 М.
Mambo 5 Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuingia Mkataba.
8:27
Joel Nanauka
Рет қаралды 10 М.
ROLLING DOWN
00:20
Natan por Aí
Рет қаралды 10 МЛН
MBIVU NA MBICHI ZA MFANYAKAZI ALIYEFUKUZWA KAZI NCHINI TANZANIA
20:49
AINA ZA MIKATABA YA AJIRA TANZANIA
15:09
Kazi Na Sheria
Рет қаралды 731
Usitishwaji/Ukomo wa Mkataba wa Ajira-Part I
21:14
Kazi Na Sheria
Рет қаралды 2,2 М.
MKATABA WA AJIRA NA SIFA ZAKE
11:27
Kazi Na Sheria
Рет қаралды 2,1 М.
LUKUVI NGORONGORO  AUSEMA UJUMBE ALIOAGIZWA NA RAIS SAMIA
5:54
Mwananchi Digital
Рет қаралды 9 М.
Sababu na Taratibu za Kumfukuza Mfanyakazi
14:26
Kazi Na Sheria
Рет қаралды 4,3 М.
ROLLING DOWN
00:20
Natan por Aí
Рет қаралды 10 МЛН