HISTORIA YAANDIKWA JIJI LA DAR/WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII WAPATIWA VITENDEA KAZI VYA MIL. 19

  Рет қаралды 968

Muungwana  Tv

Muungwana Tv

Күн бұрын

Mstahiki Meya wa halmashauri ya jiji la Dar es salaam Mhe. Omary Kumbilamoto leo Aprili 20, 2024 amekabidhi vitendea kazi kwa wahudumu wa afya 200 wa ngazi ya jamii vyenye thamani ya shilingi milioni 19,000,000/=.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Meya Kumbilamoto amesema vitendea kazi hivyo vinaenda kuimairisha utendaji kazi wa wahudumu hao ambao wanaisaidia serikali na jamii kwa kutoa huduma za afya kwa ngazi ya jamii ikizingatiwa walikua wanafanya kazi kwenye mazira ambayo sio rafiki hususani kwenye mitaa na kata.
"Tunamshukuru Rais Samia kwanza kwa kuanza kuwalipa posho japo mlianza kwa kujitolea, pili sisi kama jiji tumeona tuwaunge mkono kutokana na kazi kubwa mnayofanya na jambo hili linaenda kuweka historia, hakuna halmashauri yoyote nchini iliyofanya hivi hivyo sisi tutakuwa alama ya kwanza kuwathamini ninyi wahudumu wa ngazi ya jamii" amesema Meya Kumbilamoto
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji hilo Dkt. Zaitun Hamza amesema wahudumu wote wa ngazi ya jamii kwenye halmashauri hiyo kila mmoja atapatiwa koti la Mvua, kipaza Sauti, gumboot pamoja na kofia kwa ajili ya kuwarahisishia kazi pindi wanapotekeleza majukumu yao kwenye mitaa na kata.
"Tunasema hakuna kufanya kazi kinyonge Mhe. Rais ametuheshimisha CHW mnakumbuka miezi iliyopita alisema ataenda kuhakikisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii wanaenda kuwa na amana, furaha kwa kwenda rasmi kuajiliwa na Tanzania inakua ya mfano na hii sisi kwetu ni faraja kubwa sana" ameongeza Dkt. Zaitun
Naye Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Jamii kwenye jiji hilo Mhe. Saad Khimji amesema kutokana na ubora wa kazi mnazozifanya kwenye mitaa na kata zetu mnastahihili kupata vitendea kazi hivi na mtaendelea kupata vingi zaidi ya hivi kwani mnanusuru mambo mengi kwenye mitaa.

Пікірлер
SUMAJKT GUARD LTD YAJA NA MBINU MPYA ZA KIULINZI.
10:58
SUMAJKT TV
Рет қаралды 3,1 М.
Миллионер | 2 - серия
16:04
Million Show
Рет қаралды 1,5 МЛН
HIVI NDIVYO MADAKTARI WALIVYOTUMBULIWA ZANZIBAR
11:57
KTV TZ ONLINE
Рет қаралды 27 М.
NUNUA NDEGE KWA DOLA 225,000 TANZANIA
8:53
Daily News Digital
Рет қаралды 22 М.
USITAMANI MAFANIKIO YA MWINGINE - PASTOR SUNBELLA KYANDO
10:00
Pastor Sunbella Kyando
Рет қаралды 5 М.
Posta Yatakiwa Kuhakikisha Mifumo Yake ya Utendaji Inasomana
3:11