Рет қаралды 3,468
Serikali imesema imejipanga kuanza ujenzi wa barabara ya mzunguko wa ndani wa Jiji la Dodoma utakaokuwa na urefu wa kilometa 16 kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo linaloendelea kukua kwa kasi kutokana na shughuli za Serikali kuhamia huko.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya wakati akikagua ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 112.3 ambao ujenzi wake unaendelea vizuri.