Рет қаралды 2,503
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA EVENING GLORY (THE SCHOOL OF HEALING) 10/02/2025
UJUMBE WA LEO: SIRI ZA KIBIBLIA KUHUSU KUCHUKUA HATUA
2 Wafalme 4 : 3 - 6
Isaya 11 : 2
Mwanz 13 : 2
Mithali 16 : 9
Zaburi 85 : 13
1Samweli 17 : 32
2 Wafalme 4 : 3 - 6
3 Akasema, Nenda, ukatake vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usitake vichache.
4 Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge.
5 Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina.
6 Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma.
Isaya 11 : 2
2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;
Mwanzo 13 : 2
2 Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu.
Mithali 16 : 9
9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake.
Zaburi 85 : 13
13 Haki itakwenda mbele zake, Nayo itazifanya hatua zake kuwa njia.
1Samweli 17 : 32
32 Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu.
Mhubiri : Mwl. Andrew Bartimayo
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
KZbin: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe: Kijitonyamalutheran@gmail.com