Рет қаралды 4,265
Wakulima nchini wameshauriwa kulima vyakula vinavyostahimili ukame kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo utafiti unabainisha iwapo kiwango cha joto itaongezeka miaka 30 ijayo uzalishaji wa mazao ya chakula nchini utaporomoka hali itakayoathiri upatikanaji wa chakula nchini.
Dkt. Omary Mponda ni mtafiti kiongozi wa mbegu za mafuta nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utfiti wa Kilimo Naliendele, anasema iwapo kiwango cha joto kitaongezeka basi miaka 50 ijayo kizazi kitakosa chakula kutokana na kuwa na ukame na hivyo kuwataka wakulima kuanza kutumia kilimo cha njugu mawe ambacho kina uwezo kustahimili ukame