Рет қаралды 1,173
Mkulima Harrison Randu aliamua kuacha biashara ya boda boda na kuingilia kilimo mseto katika eneo la Misufini-Kitengwani, Kaunti ya Kilifi. Kwa sasa anakuza kila aina ya mboga, matunda na kufuga mifugo mbalimbali ikiwemo bata, kuku, mbuzi na hata ng'ombe. Ukumbi huu wa UNTOLD FARMING SEGMENT ulimtembelea na kufahamu jinsi anavyojikimu maisha yake kupitia shughuli za ukulima.