LULU ATOA MACHOZI MAHAKAMANI, HUKUMU YAKE NOVEMBA 13

  Рет қаралды 24,895

Dande Tv

Dande Tv

6 жыл бұрын

DAR ES SALAAM, TANZANIA
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya kuuwa bila kukusudia inayomkabili Muigizaji wa Filamu Elizabeth Michael 'Lulu' November 13,2017.
Hatua hiyo inatokana na Wazee watatu wa Baraza kutoa ushauri wao kwa mahakama kwamba Lulu' ameua bila kukusudia.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kuuwa bila kukusudia, ambapo anadaiwa kumuuwa Msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba, Aprili 7/2012.
Awali kabla ya wazee kutoa maoni hayo, Jaji Sam Rumanyika alisoma maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili kisha kusikiliza maoni hayo.
Kabla ya kutoa maoni hayo, Jaji Rumanyika alisema kimsingi ushahidi wa upande wa mashtaka umejikita kwenye ushahidi wa kimazingira kwa sababu Lulu ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kanumba.
Alisema kuwa ushahidi wa kimazingira unakuwa sio wa moja kwa moja, licha ya kuwa una vipande mithili ya nyololo ambavyo vimeshikana.
"Hivyo waungwana mkumbuke katika utoaji wa maoni yenu sio lazima mthibitishe makosa, pia kama mkiona mshtakiwa hausiki basi msisite kuieleza mahakama,".
Akitoa maoni yake, Mzee wa Baraza Omary Panzi amesema Lulu ameua bila kukusudia.
Amesema kuwa hatua hiyo inatokana na ushahidi wa mdogo wake Kanumba, Seth Bosco ambaye alielezea ugomvi uliotokea baina ya Lulu na marehemu.
"Maoni yangu ni kwamba marehemu alikufa kwa sababu ya kuteleza ikizingatiwa ilikuwa ni usiku na kulikuwa na giza, na chanzo cha kutekeleza ni ugomvi wake na Lulu,".
Pia Mzee wa pili, Bi.Sarah amesema Kanumba alikufa kutokana na ugomvi ambapo ushahidi pia umetueleza kulikuwa na Giza.
" Hivyo Lulu hakuuwa makusudi bali aliuwa bila kukusudia, ".
Naye Mzee wa Tatu, Rajabu Mlawa ametoa maoni yake alisema kutokana na sababu zilizosomwa anaridhika na hakuna ubishi kuwa Lulu ana kosa la kuuwa bila kukusudia.
" Ameuwa bila kukusudia na nimeridhika na kilichosemwa, kwani Kanumba alikuwa na mwili mkubwa na alikuwa katika hali ya kulewa, hivyo inaonekana katika heka heka za ugomvi inawezekana Lulu alitumia nguvu kidogo ya kumsukuma Kanumba hadi kudondoka,".
Baada ya kutoa maoni hayo, Jaji Rumanyika amesema kuwa anatarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo November 13/2017

Пікірлер: 9
@mzembemakini3532
@mzembemakini3532 Күн бұрын
Pole mwaya
@veronicasarvatory9516
@veronicasarvatory9516 6 жыл бұрын
Inauma Sana jamani pole Sana eriza Mdogo wangu. Mungu akutie nguvu
@sophiamgaya2814
@sophiamgaya2814 6 жыл бұрын
da moyo wangu unaumisana da pole dada mungu atakujaalia utatoka tuu
@rabieshamed7670
@rabieshamed7670 6 жыл бұрын
Pole sana mdogo wangu
@asiajuma5784
@asiajuma5784 6 жыл бұрын
Pole swty be strong ni miaka michache tu utakuwa nasi uraiani
@phaustaemma3327
@phaustaemma3327 6 жыл бұрын
Dah mungu awe naww manka wangu
@niitescorpion
@niitescorpion 8 ай бұрын
😢
@sawanjema4166
@sawanjema4166 6 жыл бұрын
bora ungeendelea kuigiza na senga mstaarabu kuliko kanumba.ona sasa alivyokufanyia duu!"
@teddyjaneth9078
@teddyjaneth9078 6 жыл бұрын
Hiyo ni mitihani ila itakwisha
HUKUMU YA LULU INATOLEWA LEO!!! MTAZAME ALIVYOTINGA MAHAKAMANI!
2:39
Global TV Online
Рет қаралды 272 М.
Salama Na Shikana Ep 17 | DYNAMITE Part 1
29:48
YahStoneTown
Рет қаралды 337 М.
Why You Should Always Help Others ❤️
00:40
Alan Chikin Chow
Рет қаралды 128 МЛН
Китайка и Пчелка 4 серия😂😆
00:19
KITAYKA
Рет қаралды 3,8 МЛН
I CAN’T BELIEVE I LOST 😱
00:46
Topper Guild
Рет қаралды 15 МЛН
HAPA NDIPO LULU ANAPO LALA GEREZANI
6:22
GSengo
Рет қаралды 525 М.
Mtazame Lulu Akiondoka kwa Masikitiko Mahakama Kuu, Kesi ya Kanumba
5:52
Global TV Online
Рет қаралды 500 М.
Mkasi - SO2E08 With Lulu
28:49
MkasiTV
Рет қаралды 696 М.
KESI YA LULU: Kanumba alikua na sumu mwilini - Shahidi
3:11
Millard Ayo
Рет қаралды 154 М.
LULU: "Majizo amenipa upendo kama Baba, tumepitia wakati mgumu"
1:05