Ooh!Mume usinielewe vibaya!Nachelewa kwenye foleni mpenzi! Toma toma asante kwa burudani murua!
@yakaramayaka14567 жыл бұрын
Asante Eddie, ninavyosikiliza sasa napata maana ya nyimbo. Nilikua naziimba kama kasuku bila kujua maana, hata baadhi ya maneno nilikua nakosea kwa kua nilipenda muziki katika umri mdogo nazikumbuka zote. Keep it up brazs
@AnthonyKisondella10 жыл бұрын
One the best number with Orchestra Toma Toma - this song is called "Stendi ya Basi" and not "Macho Yau Yau". Featuring the following in vocal line up: Francis Lubua, (Later on went to Muslim and called Nasri Lubua), Adamu Bakari a.k.a Sauti ya Zege and Thomas (owner and leader of the band) - their style "Tamba Tamba" was superb. Thanks for posting Eddie Nassor
@eddienassor48010 жыл бұрын
Anthony,ahsante sana kwa marekebisho.Niliusahau jina.Nimeshughulika kidogo lakini nitakuwa napost nyimbo zetu za zamani kila ntakaponafasika hivyo kuwa unachungulia mara kwa mara tafadhali.
@AnthonyKisondella10 жыл бұрын
Tupo pamoja baba - kama dhana ya timu Liverpool ya Uingereza ilivyo "you will nerver walk alone"
@kennethbahebenginilla16575 жыл бұрын
Kaka hii nyimbo nimeisikiliza juzi ktk mechi ya Liverpool vs Barcelona(Mei 7 mwaka 2019) 4-0,mimi ni shabiki wa Man Utd,sasa itakuwa inanikumbusha huzuni maana siipendi Liverpool niliwaita You'll Never Win Anything(YNWA) lol ila hongereni Liverpool na msemo wenu never walk alone.
@twilamtumbi26479 жыл бұрын
daah kaka eddie heshima ikufikie muda wote, mhh hii ngoma hata nilikuwa nishaisahau
@kennethbahebenginilla16575 жыл бұрын
Nachelewa stendi ya basi,nakumbuka mbali sana hii nyimbo wakati huo,imenikumbusha watu wengi kuanzia shule ya msingi na wote walio hai niliokuwa nao na RIP marehemu Bibi maana aliipenda sana hii nyimbo na hasa nikichelewa kurudi nyumbani ananikumbushia hii nyimbo,na wengine wote waliotangulia mbele ya haki mpumzike kwa amani peponi.
@josephsawe44264 жыл бұрын
Moto fire🙏
@gombera110 жыл бұрын
RIP. Sauti ya Zege, Nasri Lubua na Abuu semuhando.
@siamekellah75286 жыл бұрын
stand ya basi, enzi hizo utakutana na UDA tu!
@kennethbahebenginilla16575 жыл бұрын
Tumetoka mbali ndugu yangu,hasa ukisikia nyimbo hizi bado unarudisha maisha ya nyuma kukumbukia ndugu ,jamaa na marafiki,inakumbusha mengi mazuri na mengine huzuni labda tumewapoteza,na nzuri zaidi inaburudisha ni jinsi unavyosikia midundo,na kama unavyosema unakumbukia zamani stendi ya basi unakutana na UDA.
@suleimanjabir82710 жыл бұрын
This was the second edition of Orchestra Toma Toma. The first edition of Kaaloo, Kawalee and Skaisy Kasambula came with the likes of Mwanaidi, Kasambula Baba wa Ukoo and a Nyamwezi one .. I can't remember the name I call it "Uwilisiwe kisa cha wisinvi". The drums in the "Stendi ya Basi" were played by Mbwana Kox.
@eddienassor48010 жыл бұрын
Duuh! ahsante kaka
@saadmazen452810 жыл бұрын
Muziki unavyoweza kubadili maisha ya mtu...Tim Thomas mmiliki wa bendi alikuwa baharia. Alipopata fursa ya likizo akaja tanzania na vyombo na kuanzisha bendi hii ya Toma Toma hata baada ya likizo kukamilika hakurudi tena baharini....naomba tu mnifahamishe yeye ni mwenyeji wa mkoa gani?
@shukurukoll72698 жыл бұрын
Timmy Thomas alikuwa akifanya kazi nchini Botswana. Baadaye aliweza kununua vyombo vyake vya muziki na kuja navyo Tanzania. Alianzisha Bendi hiyo akiwatoa wanamuziki wengi wakati huo walikuwa kwenye bendi iliyoitwa Sola Tv. Waanzilishi hao ni pamoja na Banza Tax,Nasri Lubua@Francis Lubua, Adam bakari hiyo ilikuwa safu ya waimbaji wa wimbo huu. Wengine ni Solo hapo Mbwana Cocks, Rythm ni Uvuruge sasa yupo Msondo. bass Ernest Mkango na Drums ni Abuu Semuhando wakati huo akiitwa Abuu Lokasa(jina la utani) miaka hii alijiita Baba Diana akiwa Twanga pepeta. Naam kwa muziki wa kinyamwezi walioimba unaitwa" Kesa chane" utafute Eddie huo ni mzuri sana. Kwa ujumla Timmy Thomas ni Mtanzania na Kabila yake ni Mkwele wa Chalinze. Hivi karibuni alirudi Tanzania alikaa kwa miaka michache lakini aliamua kurejea tena nchini Botswana alipokuzoea. Bendi iliweza kusafiri nchi nyingi na wanamuziki hao waanzilishi kama Zambia,Zimbabwe,Botswana na Lesotho. Baadaye baadhi ya wanamuziki walitoka hasa waimbaji akabaki Banza Tax na wakongo walioingia kina Skasy Kasambula,Kasaloo kyanga...Awamu nyingine hiyo.
@eddienassor4808 жыл бұрын
Kaka Shukuru ahsante sana kwa maelezo yako,kwenye ukurasa huu tunayathamini sana