Рет қаралды 11,740
#Nitakushukuru, wimbo wa nne katika IBADA YA THE NIGHT OF PRAISE iliyofanyika 13 OCT 2023 katika ukumbi wa JC HALL jirani na kanisa la AICT Mbezi beach Dar es salaam.
Ndani ya wimbo huu wa NITAKUSHUKURU, AICT Mbezi beach choir tunamshukuru sana Mungu kwa baraka zake alizotukirimia tangu tulipoanzisha huduma hii ya kumsifu na kumwabudu MUNGU katika madhabahu yake.
Tunaamini wimbo huu utakuwa baraka na mwongozo wako katika kumshukuru MUNGU kwa mambo makuu aliyokutendea katika maisha yako.
SPECIAL THANKS
AICT Mbezi beach church
CREDITS
Audio production, mixing & mastering Engineer - Quillian Kilago
Video production - GLC MEDIA PRO (Director Sumuni)
Sound system, backline and stage - Mch. Mshana
Lighting - Hans company
Project Manager - Flora Shindika
SONG LYRICS
Zaburi 9:1-8 & 24:4
Nitakushukuru Bwana kwa moyo wangu wote
nitayasimulia matendo Yako yote ya ajabu
nitafurahi na kukushangilia wewe
maana ni Mungu wangu
Umeketi kitini pa enzi
ukihukumu kwa Haki
nao wakujuao jina lako
watakutumaini wewe siku zote
Maana Mungu hukuwaacha wakutafutao
mwimbieni Bwana akaaye Sayuni
yatangazeni kati ya watu wote
matendo yake yote ya ajabu
Bwana ni Nuru yangu na Wokovu wangu
nimwogope nani
Bwana ni ngome ya uzima wangu
nimhofu nani mimi?
Jeshi lijapojipanga kupigana na Mimi
moyo wangu hautaogopa
vita vijapoonekana kati yangu Mimi
tumaini langu liko kwa Baba
Nikae nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu
nitazame uzuri wa Bwana, uzuri wa Bwana hekaluni mwake
MUNGU AWABARIKI WOTE