Рет қаралды 51
Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema licha ya kupitia kipindi kigumu cha Ugonjwa wa Korona (Covid 19), lakini uchumi wa nchi umeendelea kuwa imara na pato la mtu mmoja mmoja linazidi kupanda.
Profesa Mkumbo ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma leo April 17,2024 wakati akizungumza na Watanzania kupitia vyombo vya habari kuhusu miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Waziri huyo amesema katika kipindi cha mapambano dhidi ya Korona, uchumi wa nchi ulishuka hadi chini ya asilimia mbili kabla ya kuanza kupanda ambapo kwa sasa umefikia asilimia 5.2 jambo linalotia matumaini makubwa.