Рет қаралды 406
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji ameliomba bunge lipitishe bajeti ya wizara hiyo kiasi cha Sh110.8 bilioni yenye vipaumbele vikuu sita ambavyo ni kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kielelezo na kimkakati
.
Kijaji wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024 / 2025, jijini Dodoma leo, Mei 21, 2024 amevitaja vipaumbele vinginine ni kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma kwa kuimarisha miundombinu na mazingira wezeshi, kuboresha mazingira ya uwekezaji viwandani na ufanyaji biashara, kuchochea maendeleo ya watu kwa kuboresha miradi na programu katika sekta za kiuchumi na kijamii inayohusisha elimu na mafunzo ya ujuzi.
Pia kufanya intelijensia ya masoko ya bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini kwenye masoko ya kimkakati na ya kimataifa na kuchochea ukuaji wa Sekta binafsi nchini.