No video

Salama Na OMMY DIMPOZ SE6 EP31 | ELEGANT PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

  Рет қаралды 70,201

YahStoneTown

YahStoneTown

Күн бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Kama kukiwa kuna mkutano wa Chama cha Watanashati hapa Africa na pengine Duniani basi Ommy Dimpoz anaweza kuwa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa Chama hiko na pengine anaweza kuwa hata Mwenyekiti. Hakuna swali juu ya utanashati wake kuanzia vivazi hadi nywele na hata kuongea. Anakumbuka utanashati wake ulianza toka alipokua mdogo sana, na wakati anakua si kama kila kitu alichokua anakitaka alikua anakipata ila alihakikisha vile vile vichache alivyokua navyo alihakikisha vinakua visaaafi na vinamkaa kweli kweli. Na tabia hiyo ya kujipenda na kuvaa vizuri ndo inamtambulisha Ommy Dimpoz kuwa ni mmoja wa wasanii wanaovaa vizuri zaidi hapa barani Afrika.
Omary amekua analelewa na Bibi yake baada ya Mama yake kufariki akiwa mdogo. Anakumbuka mapenzi ambayo amekua akimuonyesha toka zamani, ni kweli kama mtoto lazima utakua unamkumbuka Mama yako, ila Bibi yake alihakikisha anapata vile vyote ambavyo mtoto anakua anahitaji.
Mimi na Omary ni mtu na Rafiki yake kwahiyo mazungumzo haya zaidi yalikua ni kwaajili yako, uweze kumuelewa na kuifahamu milima na mabonde ambayo ameyapitia mpaka leo hii unamuona kasimama imara.
Kama mtoto siku zote unakua unataka kumjua Baba yako na haikua tofauti kwa Ommy pia. Shuleni watoto huitwa na wazazi wao, ukiwaona wenzako wanawaleta Baba zao na wewe hujawahi kumuona au pengine ni kwa nadra sana lazima likutie unyonge. Anakumbuka Mama yake alivyofariki na jinsi ambavyo Mzee wake alikata mawasiliano ki lazima kabisa, anakumbuka kwamba Mzee wake tayari alikua na familia nyengine lakini kama mtoto anaamini na yeye pia alikua na haki ya kupata mapenzi hata kidogo tu kutoka kwake.
Miaka ya hivi karibuni Mzee wake ameonekana kuutaka ukaribu nae kwa kasi kubwa sana ila kwa Omary huo umekua kama mtihani hivi, ana kinyongo nae bado na anaamini kwamba Mzee wake anataka kuwa karibu na yeye kwasababu tu ameona mwanae amekua maarufu na pengine anaonekana mambo yake mazuri. Hapo ndo panapo mtatiza yeye maana anaamini huo si upendo wa dhati, na hiyo ni sababu ya yeye kuendelea na maisha yake bila ya Baba yake. Pengine kuna siku itafika wawili hawa wataacha tofauti zao zipite na pengine watafahamiana vizuri na kuyafanya mahusiano kama Baba na mwana yastawi.
Pia tunafahamu kwamba miaka miwili na nusu au mitatu iliyopita Ommy aliumwa sana, na baadhi ya watu walithubutu kusema pengine hata kuimba inaweza isiwezekane tena ila kwa Rehma za Mwenyezi Mungu alimponya na kazi yake ya muziki anaendelea kuifanya kama kawaida. Nimekua nikispend nae muda mwingi kipindi ambacho tumekua tukifanya Bongo Star Search msimu wa kumi na mbili mimi na yeye, na kwasababu tumekua tukifahamiana kwa muda nimemuona kabisa hayuko 100% ila mimi na yeye tunamshkuru Mungu kwa hali alonayo sasa maana mitihani aliyopitia ni mingi sana. Haya maisha ambayo anaishi sasa ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na hatuna budi kumshukuru yeye kwa kumpa watu kwenye maisha yake ambao walihakikisha anapata matibabu yote ya hali ya juu ili maisha yake yaweze kurudi kama zamani.
Huku hilo hatukulizungumzia sana maana limeshaongelewa sana, ila tume ongea suala la ukuaji wake na mahusioano yake na familia. Urafiki wake na TID na jinsi walivyokutana. Urafiki wake na Ally Kiba, maisha yake ya shuleni na jinsi alivyokua. Urafiki wake na Diamond Platnumz na nini kilitokea kati yao. Muziki wa kizazi kipya na faida ambazo watu wana pata sasa na mahusiano yake na Chriatine ‘Seven’ Mosha na nini ambacho kimemfanya yeye afanye nae kazi. Pia tumezungumzia kutofahamiana kwake na meneja wa Diamond Platnumz Bwana Sallam Sharaff na Ommy emetuambia pia wawili hao maneno hasa yalianza kutoka wapi.
Yangu matumaini uta enjoy maongezi haya na utaokota mawili matatu pia ambayo yatakusaidia kwenye maisha yako ili mambo yazidi kuwa mswano.
Tafadhali Enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
‪KZbin Link bit.ly/KZbinS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Пікірлер: 80
@susannesusie3217
@susannesusie3217 2 жыл бұрын
😂😂😂😂😂😂 nilivyoona tuu salama na ommy nilijua leo nikuchekaaa saana na kujifunza saanaaa one love ❤️ salama❤️❤️❤️❤️❤️
@FAHAMKA192
@FAHAMKA192 2 жыл бұрын
Salama naomba siku moja umhoji joel nanauka motivational speaker 🔊 👏
@abdulraazzaqshamsan6482
@abdulraazzaqshamsan6482 2 жыл бұрын
Hapo hata me nakuunga mkono tutapata mengi sana ya muhimu
@sayeedmash6928
@sayeedmash6928 Жыл бұрын
Salama thanks so much for inviting him actually he is a very nice guy very handsome and Ana kaa mpele na heshima zaka ata the way he talks he is very polite person I like him so much he is one of celebrities na mkubali sana👌🔥🔥🔥🔥🥰🥰🥰🥰❤️♥️💋🌹🌹❤️♥️🥰🥰
@xasaxuma9835
@xasaxuma9835 2 жыл бұрын
One thing Salama Gonna do is keep her Notes!!!
@thebeneficialknowledge3399
@thebeneficialknowledge3399 2 жыл бұрын
The best podcast in East Africa, no cap. Salute 😊
@leaherasto929
@leaherasto929 2 жыл бұрын
Mungu nimwema Sana nimeuona ukuu waMungu kupitia Ommy nakuombea usimuache Mungu endelea kumuamini kila siku nakumtumikia
@jonahbirgen6946
@jonahbirgen6946 2 жыл бұрын
Ommy Dimpos much love from Kenya
@tanm2122
@tanm2122 2 жыл бұрын
For sure salama muda hautoshiiiiii..............tuongezee muda wa interview jmn...we need moreeeee
@AfiSoul103
@AfiSoul103 2 жыл бұрын
Salama naomba ombi moja.. naomba umlete Joel Arthur Nanauka.. mwandishi na mhamasishaji, anamengi ya kutujuza... Much love.. Afi.. from Spain 🌻
@fathumramadhan7567
@fathumramadhan7567 2 жыл бұрын
napenda sana vipindi chako sana watching from Qatar Doha nakubali sana
@ziyandamhlana8776
@ziyandamhlana8776 2 жыл бұрын
Jah bress you mungu akubaliki
@stevewanga957
@stevewanga957 2 жыл бұрын
huko pande gani Fatma...mm niko Wakra
@athmanrajab7740
@athmanrajab7740 2 жыл бұрын
Kwangu Pia From Doha
@fathumramadhan7567
@fathumramadhan7567 2 жыл бұрын
@@stevewanga957 mi niko umm salal Muhammad Al kheesa
@sulleyally5040
@sulleyally5040 2 жыл бұрын
Mambo vp
@arleneilunga9202
@arleneilunga9202 2 жыл бұрын
Kweli nimeanza ku kupenda kupitia nai nai 😍 na mpaka leo iko kati ya nyimbo zangu pendwa duniani🤗🇨🇩🇨🇩🇨🇩
@msafirimsafiritraveller8392
@msafirimsafiritraveller8392 2 жыл бұрын
Salama na haujawahi niangusha big up sana madam 👊👊👏
@amsiabbas3809
@amsiabbas3809 Жыл бұрын
😂🤣🤣🤣 Omi anazingua sana ujue
@violetsangamysongs1815
@violetsangamysongs1815 2 жыл бұрын
Uko vzr sana dada, dada, Yesu anakupenda sana na anakuita uje kwake
@yolamshaban4387
@yolamshaban4387 7 ай бұрын
😮😮😮
@christianshayo1797
@christianshayo1797 2 жыл бұрын
More appreciation to you salama....
@mkaapwekekariakoo6417
@mkaapwekekariakoo6417 2 жыл бұрын
Mungu Amrehemu "napenda sana Salama anavojali"
@godwinbayda133
@godwinbayda133 2 жыл бұрын
Rockeeee
@abdallahyombe4434
@abdallahyombe4434 2 жыл бұрын
Napenda sana kipindindi chako I love you Salama
@salimbazmul5806
@salimbazmul5806 2 жыл бұрын
Salama Binti Jabir Show Zako Hazijawahi niangusha Big Up Kila Hatua Zaidi#Bigup
@bakariomary5781
@bakariomary5781 2 жыл бұрын
Ni yeyeeeeee watoto wadogoooo hahahahaha napenda sana vibweka vya T.I.D
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 2 жыл бұрын
*Dimpoz* umenichekesha😀😀😀, na kutembea pia nikujifunza
@desderyanatory6671
@desderyanatory6671 2 жыл бұрын
Nakuona bwana LAVEES
@aminanamoyo83
@aminanamoyo83 2 жыл бұрын
🤣🤣🤣🤣🤣 ati Testar 😉❤ 🇹🇿🇨🇭
@Hassanchora
@Hassanchora Жыл бұрын
Great interview salama from zanzibar
@irenejohn6909
@irenejohn6909 2 жыл бұрын
nimpendae
@bongoklan274
@bongoklan274 2 жыл бұрын
Hiyo ya Pele v Neymar.. binafsi naona tofauti .. Pele alifanya yale maajabu kwenye mfumo duni; ingekua sasa hivi, with all stuff related to soccer, angekua even better .. way better than Neymar
@Alex25Mapesa
@Alex25Mapesa 2 жыл бұрын
Watching from Seychelles
@sabanajr6455
@sabanajr6455 2 жыл бұрын
Shangazi naomba mlete na p funk majani
@Bbwaoy
@Bbwaoy 2 жыл бұрын
Swali la Neymar na Pele. Ommy kali jibu kisomi naki technical zaidi… safi. Exposure nzuri.. angekua mwingine hapo ange leta tantalita nyiiingiii.
@fatmaabdallah7709
@fatmaabdallah7709 2 жыл бұрын
Hiyo juice ya baridi vipi nawe una tatizo la Koo?!
@SamirBSam
@SamirBSam 2 жыл бұрын
uyu demu mzuri mashaallah, nipeni number plz nitowe mahari kwa uyu mtoto wakizanzibar💙💙
@evancetarimo900
@evancetarimo900 2 жыл бұрын
Maliza kwenye lipa namba hapo juu tukale pilau mwanangu
@siyamanda7073
@siyamanda7073 2 жыл бұрын
I SEE THAT OMMYDIMPOZ IS IN BIG RISK OF HIS HEALTH. I DONT DEE HIM IS IN GOOD CONDITION
@malolo_tv1243
@malolo_tv1243 2 жыл бұрын
Pozi kwa pozi
@pena_tz
@pena_tz 2 жыл бұрын
dimpoz hiyo album unaanda miaka sita 😂😂
@yusuphwilliam5343
@yusuphwilliam5343 2 жыл бұрын
Kipindi kizurii sana🇹🇿❤
@muniramunira9941
@muniramunira9941 Жыл бұрын
🔥🔥🔥
@jamillahshabani7961
@jamillahshabani7961 Жыл бұрын
Salama fight basi tuwe tunakuona na Azam kipindi chako ni kizur sana
@gracejosephy2242
@gracejosephy2242 2 жыл бұрын
Mlete abby chams
@ziyandamhlana8776
@ziyandamhlana8776 2 жыл бұрын
Is true this is interview Doctar dre alihangaika
@kamilagwajuma8384
@kamilagwajuma8384 2 жыл бұрын
Ana jua kuimba ila sio mwandishi mzuri
@yusufmalangu9797
@yusufmalangu9797 2 жыл бұрын
mchiz ana unyama
@user-sp3gg7id8q
@user-sp3gg7id8q 2 жыл бұрын
Ommy dimpoz aliposema diamond ananunuwa views diamond alipanic nakumtuka ommy matusi ya laana but ommy twajuwa kuwa ulikuwa unatetea mziki wa tanzania na east African one day watu wengi watakupa respect unayo deserves huyo diamond ni mwizi wa views na subscribers feki ni times ya basata kumwita huyu mwizi maana anakandamiza wanamziki watanzania na east African yeye mondi anajibostia views wamilioni 50,00000+ karibu kila video na wasanii wake anawabostia 20,000000 na hizo views humpelekea apate nomination kwenye awards za nje ya nchi na kualikwa kwenye vile vitamasha lkn shows zake huko London or marekani anaparfome kwenye kitchen party kama harmonize.
@saidjumasaid3924
@saidjumasaid3924 2 жыл бұрын
Usikubali kubebeshwa chuki, chuki maisha yote humiathiri mtu aliokuwa nayo Kwanini diamond akipata views kidogo hausemi kitu,akipata nying kanunua, akikosa tunzo husem kitu,akipata nyingi kanunua, akijaza show show sio yake, Mungu amempa diamond na nafas yake anaitumia vizuur Punguza chuki NB Jambo lolote unaloliona linakuletea maslahi kwa maisha yako basi lifanye Kama kweli anafanya hivo kwa kuona maslahi basi mwache afanye na hao wengine kama wanataka kufanya basi wafanye
@user-sp3gg7id8q
@user-sp3gg7id8q 2 жыл бұрын
@@saidjumasaid3924 sasa wewe brother una IQ ngapi ? Maana haujiulizi huyo mondi ana views kuliko burna boy, wizkid, davido hata uwaunganishe watatu hawamfiki kwa views na kama hiyo haiku surprised anampita hata Kanye West kwa views 😀 but show zake huko marekani na London anaparfome kwenye kitchen party lkn hao wenye views na subscribers kidogo wanaparfome kwenye o2 arena London siku 3 mfululizo watu 20,000 tena tickets dakika 2 zishaisha, na unaposema wasanii wengine wanunue nao ! are you serious? Au unajipumbaza? Wasanii watanzania wengi kupata ile pesa ya kushoot video ni tabu alafu umwambie atoe pesa nyengine ya kuboost views ili nyimbo na video yake iyonekane imeenda mjini! Suluhisho ni hao wizi wa views wakatazwe kuiba.
@saidjumasaid3924
@saidjumasaid3924 2 жыл бұрын
@@user-sp3gg7id8q huna kingine zaid ya chuki kaka Hicho sio kipimo cha kusema kuwa ananunua views Hoja hizi ndio unajiona una IQ kubwa Hizi hata mtoto mdogo anakujibu ati
@Hez_madona
@Hez_madona Жыл бұрын
🚀
@zulekha2007
@zulekha2007 Жыл бұрын
🤣🤣🤣🤣🤣
@kazkaz1943
@kazkaz1943 2 жыл бұрын
Salama ni mmoja
@yusufmalangu9797
@yusufmalangu9797 2 жыл бұрын
salama tuongeze muda
@justinmganiwa2790
@justinmganiwa2790 Жыл бұрын
mlete nanauka
@egnokapinga16
@egnokapinga16 2 жыл бұрын
Ommy akili kubwa.
@ramseyjissah5030
@ramseyjissah5030 2 жыл бұрын
My favourite ❤ yahstone town
@tausonsamwel8736
@tausonsamwel8736 2 жыл бұрын
Ommy dimpoz guy never disappoint
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 2 жыл бұрын
🌟
@rahyakikoti9537
@rahyakikoti9537 2 жыл бұрын
Ommy😅😅😅🤣🤣🤣
@binkhalidame2754
@binkhalidame2754 2 жыл бұрын
🤩🤩🙏🏻
@mimiummie
@mimiummie 2 жыл бұрын
💯
@rashidsuleiman2641
@rashidsuleiman2641 2 жыл бұрын
Kipindi nikizuri
@muniramunira9941
@muniramunira9941 Жыл бұрын
🤣🤣
@mrmweusi592
@mrmweusi592 2 жыл бұрын
Mlete nanauka
@rashidsuleiman2641
@rashidsuleiman2641 2 жыл бұрын
Kipindi nikizuri
大家都拉出了什么#小丑 #shorts
00:35
好人小丑
Рет қаралды 77 МЛН
The FASTEST way to PASS SNACKS! #shorts #mingweirocks
00:36
mingweirocks
Рет қаралды 12 МЛН
КТО ЛЮБИТ ГРИБЫ?? #shorts
00:24
Паша Осадчий
Рет қаралды 4,3 МЛН
大家都拉出了什么#小丑 #shorts
00:35
好人小丑
Рет қаралды 77 МЛН