Salama Na MAJIZZO SE6 EP17 | MPIMAJI PART 1| SendTip MPESA LIPA NO 5578460

  Рет қаралды 130,760

YahStoneTown

YahStoneTown

2 жыл бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
MPIMAJI
Francis Ciza that’s the name, anastahili heshima yake kwa ujasiri mkubwa ambao ameuonyesha kabla hajafika hapa alipo leo. Njia yake kwa mujibu wa haya maongezi yetu ilikua ya kulazimisha sana na yeye hakuwahi kukata tamaa, au tuseme neno au wazo la kukata tamaa halijawahi kuwa mawazoni mwake.
Majay ndo jina la umaarufu wake, Dj Majay au RDJ Majay au Majizzo moja ya ma Dj walokua wakiunda kundi la ‘Kwa Fujo DJ’s’ akiwa pamoja na Abubakar Sadique na ma Dj wengine wakati huo. Jinsi gani walikutana na nini kiliwafanya wawe na umoja huo? Tulimuuliza Majay kwenye maongezi haya na akaniambia waliona kitu ambacho hakuna mtu mwengine alikiona wakati huo na kweli kilifanya kazi.
Nini sasa kilisababisha umoja wao kuvunjika? Nini special kwake ambacho anadhani kinamfanya aendelee kuwa mwenye mafanikio na relevant kuliko wenzake? Huku sasa anatuelezea rasilimali yake aliyopewa na Mwenyezi Mungu, ya KUTOKATA TAMAA. Ambayo ndo imemfanya yeye anendelee kubaki kuwa nahodha wa boti yake ambayo imeweza kupambana na dhurba nyingi za baharini na nchi kavu lakini bado inaendelea na safari.
Majay alianza kutafuta kwake kama fundi nguo, wengi tunawaita fundi cherehani, anatuambia mtaani kwake kulikua na MC mmoja wa harusi ambaye yeye ndo alikua anamshonea nguo zake na siku ambayo alimchukua Majay kwenye moja ya kazi zake ndo siku ambayo maisha ya Majay YALIBADILIKA.
Sasa ni CEO wa moja ya Radio zenye nguvu hapa Tanzania na mpambanaji ambaye anahakikisha vijana na mziki wetu wa kizazi kipya unazidi kwenda mbali, yeye ni mtu ambaye anawavutia vijana wengi kwa kuwapa matumaini kwamba kuna siku mazuri yatakuja tu, at least hiyo ndo vibe ambayo mimi naipata kwake. Ashakataliwa sana. Ashakosea sana, ashafungiwa milango sana, ashakimbiwa sana na marafiki ambao walikua hawaamini kwenye ndoto yake na amesha anza upya mara kadhaa kwa kuamini kwamba kama aliweza kukipata mwanzo, basi inawezekana kukipata tena, na hivyo ndo jinsi ambavyo ilikua na inaendelea kuwa mpaka leo hii.
Kama unahitaji inspiration au mtu wa kumtazama ndoto zake ili na wewe uweze kuzitimiza za kwako basi Francis Ciza anaweza kukusadia sana.
Tafadhali enjoy mazungumzo yetu haya ambayo yamejaa safari ndefu ya kuanzia kwenye kupima watu viuno na kifua mpaka kuwapangia watu burudani isiyochosha.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪KZbin Link bit.ly/KZbinSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Пікірлер: 156
@fefenailsandmakeup1353
@fefenailsandmakeup1353 2 жыл бұрын
Nnachojifunza Mungu anatuinua kupitia watu, cha msingi ni kumuomba atusaidie watu sahihi wanaotakiwa kutushika mkono tufikie destiny zetu in Jesus name🙏❤
@cindyakiki6623
@cindyakiki6623 2 жыл бұрын
Amen love🙏 caption🔥👌🏻
@leecode6135
@leecode6135 2 жыл бұрын
Uko poa dada kwa ujumbe wako
@DanielIsaack-mx4fc
@DanielIsaack-mx4fc Жыл бұрын
Thats true❤️🔥
@johnkalage2914
@johnkalage2914 25 күн бұрын
Amen. 🙏
@JustArkon
@JustArkon 2 жыл бұрын
Sio bahati mbaya, yote ni ya Mungu sema bahati nzuri sehemu yenyewe ipo!!
@winifridambilinyi8043
@winifridambilinyi8043 2 жыл бұрын
Wooow Inawezekana kuanza ulipo na kufikia unatamanikuwa💪🏾
@Adeen.1
@Adeen.1 2 жыл бұрын
Ni kitu kizuri kujivunia kijana ka wewe majizo ila kwa usikivu wangu na experience yangu historia yako ingeweza kuwa inspirational than that kama ungeiweka wazi huenda ingetu inspire zaidi.
@Adeen.1
@Adeen.1 2 жыл бұрын
Hau sound comfortable with what you are saying...ka una edit vitu hivi ila big up kwa hapo ulipo🙌🙌🙌🙌
@editatairo9667
@editatairo9667 2 жыл бұрын
What an Inspiration. Congrats Majjizo for the 'Never give up and hustling attitude'. Congrats Salama Jabir for such a program. Unatuletea life stories za watu mbalimbali ambao wanakuwa inspiration kwetu sio zile siasa za motivation speakers
@lydiathomas2905
@lydiathomas2905 2 жыл бұрын
I never listen to you before but your life is inspirational to many young people out there.
@Swahili_Finance
@Swahili_Finance 2 жыл бұрын
Ukiwa Mtu Mwenye Maono Makubwa, Ukiwaelezea Watu wako ukawaona Hawakuelewi Jua Hao Unatakiwa Kuwaacha, The way Unavyo fikiria kwa Ukubwa Sio Kama wao cz Upeo wao Mdogo. So lazima ujiondoe kwenye Hilo Group, This is the spirit of Visionary guys who change the world and systems. Disrupt everything
@medyamon
@medyamon 2 жыл бұрын
This is inspiring, a man that says i will do something and they do it or work on it....this thing is rare! I have learned to never settle for small minded people/people who can't take a risk because they are scared to fail. He believed in himself and he did what he wated to. Congratulations sir! Nlijuaga tu there is more to that ukimya wako and ofcoz we seeing your wife today! Ungeniuliza nikutafsiri kwa neno moja then I would say wisdom with no hesitation 👏🏼👏🏼
@saraphinakabubi3725
@saraphinakabubi3725 2 жыл бұрын
Exactly 🙌
@loiceamugune6711
@loiceamugune6711 2 жыл бұрын
He is one of my favorite,Majay you are a determined man na mchakarikaji sana God bless you man.
@abduly.snootie
@abduly.snootie 2 жыл бұрын
Aseee, BONGE MOJA LA INTERVIEW S/O TO SALAMA, KWA HILI PINDI LA KIBABE, BIG UP CHAMP MAJIZZO.✨👑💪🏾👊🏾✊🏾 🎥🎬🎞️📽️🔥🔥🔥🔥🔥
@mwarahsemor6301
@mwarahsemor6301 2 жыл бұрын
jizzo nakubali sana haso zako broo kumbe sijachelewa ✊
@aivanandrea2160
@aivanandrea2160 2 жыл бұрын
Thanks sisy for being incredible..
@salomewandya7257
@salomewandya7257 2 жыл бұрын
Dah kweli maisha ni safari ndefu na hakuna kukata tamaa
@ziyandamhlana8776
@ziyandamhlana8776 2 жыл бұрын
Congrats salama is best interview u do big up
@jembeMahiri
@jembeMahiri Жыл бұрын
Hii ndo interview ya kwanza Salama ameachia mhojiwa kutiririka na stori yake mwenyewe bila kuuliza maswali. Majay kama mtu hawezi kuwa motivated na story ya majizo huwezi kuwa motivated na chochote.
@Tatizofficial
@Tatizofficial 2 жыл бұрын
Anaongea kiupolee,mm nampendaga majizoo na radio yake na hasoo zake,keep it up bro♥️
@jujo_master
@jujo_master 2 жыл бұрын
show kalii salama tuletee D.knob tafadhali👐👐
@bahatirngulika4493
@bahatirngulika4493 2 жыл бұрын
So inspiring kwakwel,let me go for part2
@babyhamisi1437
@babyhamisi1437 2 жыл бұрын
Napenda sana salama anavyoanza kuuliza maswali yaani huwezi tarajia
@yousramutwale2463
@yousramutwale2463 2 жыл бұрын
Asante majizo kwastoria Yako n'a Asante kwakumuoa lulu
@nancepallangyo8805
@nancepallangyo8805 2 жыл бұрын
Nakupenda bure salama ❤️
@MRiki03
@MRiki03 2 жыл бұрын
Vary humble Man Salama Leo maswali sijayaskia but nimejifunza sana sana Mwenyezi Mungu anitunzie ❤️❤️❤️❤️❤️
@CHITUS
@CHITUS 2 жыл бұрын
Wooow Inawezekana kuanza ulipo na kufikia unatamanikuwa💪
@veronicapotas5706
@veronicapotas5706 2 жыл бұрын
Dah Boss luge apumzike tu kwa amani kwakweli yule ameokoa TANZANIA
@partnersah8802
@partnersah8802 2 жыл бұрын
Sure. Sikujua kama kila.kijana anayeshaini now ametoka kwake aseee. Allah ampunzishe kwa aman 🤲
@veronicapotas5706
@veronicapotas5706 2 жыл бұрын
@@partnersah8802 yaan sijui ni kwann wazuri ndo hutangulia😓😓
@sashaemmilz1468
@sashaemmilz1468 2 жыл бұрын
Aisee sikati tamaa jamani mweeh MUNGU nisaidie,namkubali sana baba G
@MrSABYY
@MrSABYY 2 жыл бұрын
Huyu jamaa yuko makini sana 🗝🗝. Big up Tajiri Majizooo 🔥🔥🔥
@gutalemohammed5043
@gutalemohammed5043 2 жыл бұрын
Definition of genius =respect, hard-working,and manners
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 2 жыл бұрын
Awesome 👌🏽
@sulehimanhabibu6046
@sulehimanhabibu6046 Жыл бұрын
Mleten diamond siku moja au Harmonies salama
@edgahendi1949
@edgahendi1949 Жыл бұрын
Hahahaaa majizo amefanana na yle mchungai wakenya aliewauwa watu kwakufunga enway majizo namkubali sana
@flavourboyke
@flavourboyke 2 жыл бұрын
Huyu ndio mume wa lulu
@esabelfadhili8432
@esabelfadhili8432 2 жыл бұрын
Sizza ni kaka🙌🙌🙌🙌🙌
@ireneamanimusician9635
@ireneamanimusician9635 2 жыл бұрын
Salama hii description sasa mm hoooooiiiiiii😃😃😃😃😃mbavu zangu jama
@mussamushi6958
@mussamushi6958 Жыл бұрын
Anaongea kwa Sauti ya chini hatumsikii fresh
@vicentjulio9337
@vicentjulio9337 2 жыл бұрын
Respect Majizzo
@aminiismail3371
@aminiismail3371 2 жыл бұрын
Dada Salama tuletee Vunjabei na Mo dewji
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 2 жыл бұрын
Duh! Mafanikio sio rahisi kwakweli 😢
@salomewandya7257
@salomewandya7257 2 жыл бұрын
Saaana aiseee
@businesstanzania
@businesstanzania 2 жыл бұрын
Sauti Ya Maj Ipo Chini, Asikiki
@jujo_master
@jujo_master 2 жыл бұрын
😄 😄 😄 ila tid mnyama ni mtundu bana
@asiaashraph4227
@asiaashraph4227 2 жыл бұрын
❤️❤️❤️
@mrfashion1687
@mrfashion1687 2 жыл бұрын
Nasubir SALAMA NA ADAMU MCHOMVU
@nemestesha7784
@nemestesha7784 2 жыл бұрын
respect🤛
@unitedtune_tz5369
@unitedtune_tz5369 2 жыл бұрын
Ya jux! Hamjapost jmn! Wengine hatuna mda wa kukaa sana kweny TV tunaomba ziwe znatumea na huku
@fatumamkini1652
@fatumamkini1652 2 жыл бұрын
❣️❣️🙏
@makalani4759
@makalani4759 Жыл бұрын
Karibu kinyope kaka
@babyhamisi1437
@babyhamisi1437 2 жыл бұрын
Watu tunatoka mbali kwa kweli
@NyehuDaudi
@NyehuDaudi Жыл бұрын
Haki maisha nikupambana hakuna kukata Tama
@preatyarhaan1190
@preatyarhaan1190 2 жыл бұрын
Interview na wema sepetu plz
@chikotosammy3891
@chikotosammy3891 2 жыл бұрын
Madam Boss naomba kama yawezekana tupate Mr Blue #Nyanizee
@hastomatumla5017
@hastomatumla5017 2 жыл бұрын
Alaf kasome history ya majizo Kwa mangeapp
@sashahauke2032
@sashahauke2032 2 жыл бұрын
But nakupenda buuuure salama hata hivyo nimreeeeeembo
@giftmalema5032
@giftmalema5032 2 жыл бұрын
Sijutii kusubscribe hii Chanel..... asante majizzo
@dcampafrica
@dcampafrica 2 жыл бұрын
tuletee young killer
@coffeetable5683
@coffeetable5683 2 жыл бұрын
tunamuhitaji Oscar oscar
@albogastmselejr4583
@albogastmselejr4583 2 жыл бұрын
Jesca Kumbe Ana Mafutaaa Jamani 🤣🤣
@catenzeki678
@catenzeki678 2 жыл бұрын
😂😂😂😂😂
@ARAFATVSHOW
@ARAFATVSHOW 2 жыл бұрын
❤️❤️❤️❤️❤️❤️
@minaakimwaga5073
@minaakimwaga5073 2 жыл бұрын
Hy sauti majizo
@saidzola7905
@saidzola7905 2 жыл бұрын
Amani karume pls
@ramlaamiri5601
@ramlaamiri5601 2 жыл бұрын
Show show
@anikaanikaa7617
@anikaanikaa7617 2 жыл бұрын
Tuletee kajala please
@Epicmarkmedia
@Epicmarkmedia 2 жыл бұрын
Tunamwomba John Joo
@hafidhfaridjuma5938
@hafidhfaridjuma5938 2 жыл бұрын
Ajee kwelii plz salama
@davidmachange7186
@davidmachange7186 2 жыл бұрын
Salama episodes nyingine uendelee kuziweka google podcasts kama ulivyokua unafanya b4....Ila shows are delicious 😋 🔥
@kwandusamson
@kwandusamson 2 жыл бұрын
Q
@salmaluhasi2986
@salmaluhasi2986 2 жыл бұрын
Waooooo, kwenye maisha hakuna kukata tamaaa!!
@viwawashanganionlinetv1601
@viwawashanganionlinetv1601 2 жыл бұрын
Diamond ndio tunaemtaka
@deusdedit789
@deusdedit789 2 жыл бұрын
Sasa mimi naogopa nini lazima ndoto zangu zitimie
@msabahaali758
@msabahaali758 11 ай бұрын
salama mualike Ismaili Jussa Ladhu apo
@ziadaakida2743
@ziadaakida2743 2 жыл бұрын
Majizo wewe ni mpole,Harafu umwelewa mno Kama ndivyo hata ndani kwako basi Lulu amepata mume sahihi,
@prettyh7509
@prettyh7509 2 жыл бұрын
Upele anaujua mkunaji
@waltergodwin2529
@waltergodwin2529 Жыл бұрын
Kama uhai upo, hakuna uchawi kijana.
@selemanimsangi7805
@selemanimsangi7805 2 жыл бұрын
Tunaomba umlete Mzee Chrissant Mhennga Aliyekuwa mkuu wa kundi la kaole enzi za kanumba
@nyamkamawanjara29
@nyamkamawanjara29 2 жыл бұрын
tuleteee mwijaku siku moja
@veronicapotas5706
@veronicapotas5706 2 жыл бұрын
Yule ataongea mpaka muda uishe na hakuna cha maana alichokisema hahaaaaaa
@winnieevarest3634
@winnieevarest3634 2 жыл бұрын
tunamuomba wema please
@irenemakene7219
@irenemakene7219 2 жыл бұрын
I am here to learn and be inspired....
@renatuskasula259
@renatuskasula259 2 жыл бұрын
Rado kiraka
@naaalovee3910
@naaalovee3910 2 жыл бұрын
Dj majizo kwa fuuuujooooo
@kassimiddi1663
@kassimiddi1663 2 жыл бұрын
wadeiii
@mangetz2835
@mangetz2835 2 жыл бұрын
Sauti ndogo
@josephkavindi3666
@josephkavindi3666 Жыл бұрын
Kwa Fujo Djs ❤
@johannahakim8470
@johannahakim8470 2 жыл бұрын
Tuleteye paula
@zenadaudzena2849
@zenadaudzena2849 2 жыл бұрын
Majizzo nawe kiswanglish chako
@bettymwigune8150
@bettymwigune8150 2 жыл бұрын
🤣🤣🤣🤣
@khadijahali4837
@khadijahali4837 Жыл бұрын
🤣🤣
@sumayasumaya6455
@sumayasumaya6455 2 жыл бұрын
Mtengeneze wa kwako..then muweke mbele yako' akupendeze..eehh.!? unaweza kumkuta katoboa kwa mungu anakula kuku pepon., unaingilia mamlaka ya kuumba toka mungu.!? kulea tu mtoto anaweza kukushinda..ije kutengeza binaadam.?¿ Shetan wahed.! mkubwa
@meislive5234
@meislive5234 2 жыл бұрын
Radio gani ? Magi kimagi no that and she is now that gay!
@ahmadifataha6677
@ahmadifataha6677 2 жыл бұрын
Mbona husemi kwenu lutamba lindi jina lako halisi hutaji unataja jina la janja janja
@housnayousif780
@housnayousif780 2 жыл бұрын
😳😳😳
@Blakybraun_3
@Blakybraun_3 2 жыл бұрын
Hivi jaman kila celebrity hakuna aliyetoka kwenye familia ya matajiri mbona kila mtu ametoka kwenye familia masikini tu
@wardamzuka3997
@wardamzuka3997 2 жыл бұрын
Wapo ,wema ,hemed PhD familia zao hazikuwa maskini 😀😀😀😀😀
@NS-ru1yf
@NS-ru1yf 2 жыл бұрын
Mo
@magdalenayinza1418
@magdalenayinza1418 2 жыл бұрын
Jux, zuchu,
@Rosepeter001
@Rosepeter001 Жыл бұрын
Madam Rita
@mrmweusi592
@mrmweusi592 2 жыл бұрын
Afuate nikki wa pili
@zuenahamoud1532
@zuenahamoud1532 2 жыл бұрын
Madawa yakulevya ndo yaliyokutoa sema ukitumia akili
@arafaomari1832
@arafaomari1832 2 жыл бұрын
Wewe zuena kweli hiyo
@vickydan2869
@vickydan2869 2 жыл бұрын
Mmmh
@prettyh7509
@prettyh7509 2 жыл бұрын
Nawe fanya hivyo
@mbux7443
@mbux7443 2 жыл бұрын
Kabisa
@bernadetamodest6170
@bernadetamodest6170 2 жыл бұрын
Nawe kauze ili uwe nazo,unafanya nini kwani?
@johnmwandu2116
@johnmwandu2116 2 жыл бұрын
TUNAOMBA YA ZEMBWELA na DANIEL KIJO, TAFADHALI
@queenmilan2024
@queenmilan2024 2 жыл бұрын
ILA LULU ANAVUMILIA.SANA KULALA NA HUYU MWANAUME CHAI HATA BURE SIMUONESHI UCHI WANGU.
@salomewandya7257
@salomewandya7257 2 жыл бұрын
Kwann my?
@Burner_Acc
@Burner_Acc 2 жыл бұрын
Uchi wako unanuka hata hivyo
@maryamtan682
@maryamtan682 2 жыл бұрын
Ttz mnaenda waramba lipsi ndo maana,.
@esterdoriye4780
@esterdoriye4780 2 жыл бұрын
Dada anachuki binafsi huyu
@deboraezekiel784
@deboraezekiel784 2 жыл бұрын
Mbona kaka yuko vzr tu jaman
@smfkingdom9944
@smfkingdom9944 2 жыл бұрын
kzbin.info/www/bejne/e6C4f61-j9SqfLs Balaa la kamti pombe
@kwinyajohn
@kwinyajohn 7 ай бұрын
D.nob
@richardcastromzena5136
@richardcastromzena5136 2 жыл бұрын
Shout out to TMK representative sir kassim. 11:36 12:46 13:43 14:20 15:28 17:24 18:22 19:06 20:33 21:02 21:32 23:19 23:59 25:20
@hanihaadamuhanifaadamu4125
@hanihaadamuhanifaadamu4125 2 жыл бұрын
Kumbehuyu kakanimbayahivi
@maryamtan682
@maryamtan682 2 жыл бұрын
Wala hn ubaya wwt, acha chuki, kwenye list ya wabaya uwezi kumueka kamwe.
@dianamdaku9802
@dianamdaku9802 2 жыл бұрын
😂😂😂umeandika mwenyew au?
@zuenahamoud1532
@zuenahamoud1532 2 жыл бұрын
Kiukweli mbayaaaa hata Eliza kafuata marundo tu
@bahathmuro7145
@bahathmuro7145 2 жыл бұрын
Anaongea vizuri
@hidayakisensi2747
@hidayakisensi2747 2 жыл бұрын
😀
@queenmilan2024
@queenmilan2024 2 жыл бұрын
HE KUMBE HUYU BABA NI LI BAYA HIVYO.
@salomewandya7257
@salomewandya7257 2 жыл бұрын
🤣🤣🤣jmn
@maryamtan682
@maryamtan682 2 жыл бұрын
Wee mwenyewe mbaya.
@deboraezekiel784
@deboraezekiel784 2 жыл бұрын
Wewe sio Mungu huluhusiw kumkosoa mtu
@keifatuke99
@keifatuke99 2 жыл бұрын
Baba yako akiwa mzuri yatosha
@rahmasoliman489
@rahmasoliman489 2 жыл бұрын
Unataka awe mzuri ili iweje. Kenge we!
@nantaembanusurupia5674
@nantaembanusurupia5674 2 жыл бұрын
Sio bahati mbaya, yote ni ya Mungu sema bahati nzuri sehemu yenyewe ipo!!
@zainabcosmas6961
@zainabcosmas6961 2 жыл бұрын
❤️❤️❤️
gabo Zigamba
0:38
Eric Gabriel
Рет қаралды 38 М.
Amazing weight loss transformation !! 😱😱
00:24
Tibo InShape
Рет қаралды 59 МЛН
Secret Experiment Toothpaste Pt.4 😱 #shorts
00:35
Mr DegrEE
Рет қаралды 19 МЛН
Useful gadget for styling hair 🤩💖 #gadgets #hairstyle
00:20
FLIP FLOP Hacks
Рет қаралды 8 МЛН
Salama Na MR BLUE SE6 EP69 KHERI PART 1 SendTip MPESA LIPA NO 5578460
25:09
BEHIND The GRAM (MOM & DAUGHTER) Ep 1| kajala amlilia paula kuhusu Harmonize|
3:51
Feysal Daudi Films. 457k views.5hrs
Рет қаралды 14 М.
Mkasi | S13E10 with Ruge Extended Version
40:28
MkasiTV
Рет қаралды 532 М.
Difference of girls and boys when eating sweets 😂😬
0:35
VovaLika Family
Рет қаралды 7 МЛН
A young mother couldn't calm down her baby at the lesson #shorts
0:32
Fabiosa Best Lifehacks
Рет қаралды 7 МЛН
настоящий чемпион
0:59
QorabogTV
Рет қаралды 8 МЛН
GiGaMoN! 5 🗿 #gigachad #sigma
0:53
The Logan Chitwood
Рет қаралды 9 МЛН
ПОМЕНЯЕМСЯ? 🥺😬😵‍💫 #funny #comedy
0:12
Fast Family LIFE
Рет қаралды 1,2 МЛН