Рет қаралды 1,968,001
Simba SC imepokea kichapo kizito cha mabao 5-1 kutoka kwa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC #NBCPremierLeague kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Yanga walianza dakika ya 3 kwa goli la Kennedy Musonda kabla ya Simba kuchomoa dakika ya 9 kupitia kwa Kibu Denis.
Kipindi cha pili Yanga ikashindilia kwa mabao ya Maxi Nzengeli aliyefunga mawili dakika ya 64 na 77, Stephane Aziz Ki dakika ya 73 na Pacome Zouzoua dakika ya 87 kwa mkwaju wa penati.
Tazama highlights....