TAHARUKI GEITA WANANCHI WAVAMIA KITUO CHA POLISI, WAGOMA KUFUNGUA MADUKA

  Рет қаралды 9,859

Mwananchi Digital

Mwananchi Digital

Күн бұрын

Eneo la Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita asubuhi ya leo Alhamisi Septemba 12, 2024 hadi sasa (Saa 4:10 asubuhi) wafanyabiashara hawajafungua maduka wakidai kuhofia kukamatwa na polisi.
Chanzo cha hofu hiyo ni vurugu zilitokea jana baina ya wananchi na polisi na kusababisha watu wawili kuuawa huku kituo cha polisi kikishambuliwa kwa mawe.
Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi jana Jumatano, David Misime imesema katika vurugu hizo waliopoteza maisha ni mwanaume mmoja ambaye jina lake halijafahamika anayekadiriwa kuwa na miaka 18 -20 na mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Lulembela, Theresia John (18).
Mwananchi Digital imefika eneo la tukio na kushuhudia maduka zaidi za 50 katika eneo hilo yamefungwa.
Baadhi ya wananchi ambao wameogopa kutaja majina yao wakihofia kukamatwa na polisi wamesema kutokana na vurugu zilizotokea jana wafanyabiashara wana hofu.
"Hapa siyo maduka tu hata nyumbani vijana wameondoka wanaogopa, wanaume nao hawapo kila mmoja anahofia kukamatwa, kama hivi tunashindwa kupata huduma maduka yamefungwa, bodaboda hazifanyi kazi kwa kweli ni mateso," amesema mmoja ya wakazi wa eneo hilo kwa sharti la kutotajwa jina wala kupigwa picha.
Hata hivyo, Ofisa Mtendaji Kata ya Lulembela, Frank Gonyo amesema hawajazuia wafanyabishara kufungua maduka lakini hali iliyopo sasa imetokana na hofu baada ya vurugu zilizotokea jana.
Katika taarifa ya jana, Misime amesema chanzo cha vurugu hizo ni baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa kwenye mnada wa Lulembelea kuwadhania kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambulia.
“Walipokuwa wanawashambulia alitokea ofisa mtendaji wa kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Lulembela. Hata hivyo, wananchi wanaokadiriwa takribani 800 walifika kituoni na kuwataka polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue," amesema Misime kwenye taarifa yake.

Пікірлер: 17
@emmanuellupiga
@emmanuellupiga 5 күн бұрын
Hiki kituo cha polis hiki du
@agustinoezekiel
@agustinoezekiel 5 күн бұрын
Hilo jengo la kituo litaleta gumzo
@amedeusfredrick1614
@amedeusfredrick1614 5 күн бұрын
Hii nchi sahivi ni nje ndani
@trendings1293
@trendings1293 5 күн бұрын
Yani siku hizi ukiskia vurugu lazima polisi waue watu afu serikali iko kimya tu,mama samia katulia kabisa hana shida wala sio shida zake
@twalibulomy-cd4zd
@twalibulomy-cd4zd 5 күн бұрын
Bado hamjasema.
@Hamy1109
@Hamy1109 5 күн бұрын
Hicho kituo kifanyiwe maboresho mbona kipo kama banda!?
@abdihq4228
@abdihq4228 5 күн бұрын
kwa ujinga wao HAO WATU WAJENGE KITUO KIPYA CHA POLISI
@twalibulomy-cd4zd
@twalibulomy-cd4zd 5 күн бұрын
Kamata hawa Machadema wote. Wanapandikiza chuki dhidi ya police. Hawa wasenge ni wabinafs sana, Wanatak kushinda uchaguz hata kwa kumwaga damu za watu wengine. Watoto wao wapo nje wanasoma ili badae waje waendelee kusumbua Mazwazwa yote ya Chadema.
@Ushauri235
@Ushauri235 5 күн бұрын
Wewe umeona chadema hapo akitekwa mtoto wako hautaongea chadema kuwa makini wewe
@helencyprian8745
@helencyprian8745 5 күн бұрын
Chadema watakuwa wamfundishwa na nyie mloanza zamani kumwaga damu
@twalibulomy-cd4zd
@twalibulomy-cd4zd 5 күн бұрын
@@Ushauri235 nljua kuna Zwazwa atkurupuka Kama ngiri.
@twalibulomy-cd4zd
@twalibulomy-cd4zd 5 күн бұрын
@@helencyprian8745 yule Mbweha toka umezaliwa ni Mwenykit anaongoza mapongo
@halimamasai2234
@halimamasai2234 5 күн бұрын
@@twalibulomy-cd4zdyani upo sawa kabisa ni chadema ndo wanao leta hiyo mihemuko kwa wananchi lakini watakufa kama kuku hakuna mtu juu ya sheria polisi wafanye kazi yao watu washambulie kitu cha polisi halafu polisi waangalie tu hiyo si kweli
这三姐弟太会藏了!#小丑#天使#路飞#家庭#搞笑
00:24
家庭搞笑日记
Рет қаралды 124 МЛН
小丑妹妹插队被妈妈教训!#小丑#路飞#家庭#搞笑
00:12
家庭搞笑日记
Рет қаралды 35 МЛН
Bend The Impossible Bar Win $1,000
00:57
Stokes Twins
Рет қаралды 48 МЛН
Wananchi wavamia kituo cha polisi kusaka watuhumiwa,wawili wafariki dunia
4:58
A Chakwera Agendewdwa Ku Chikwawa
4:15
Nyasa VoiceBox
Рет қаралды 15 М.
这三姐弟太会藏了!#小丑#天使#路飞#家庭#搞笑
00:24
家庭搞笑日记
Рет қаралды 124 МЛН