Рет қаралды 875
@Mtangazaji #Africanfood #Ugali #Unga
Moja ya vyakula vinavyopendwa na raia kutoka Afrika walioko ughaibuni ni Ugali, chakula kinachopikwa kutokana na unga ambao waweza kuwa umetokana na kusagwa kwa nafaka ikiwemo mahindi,mtama,uwele,na zinginezo.
Ugali unamajina mengi kutokana na makabila mbalimbali afrika ikiwemo sima vuswa, bogobe, fufu, gauli, gima, isitshwala, kimnyet, kuon, mieliepap, ngima, nshima, obokima, ovuchima, (o)busuma, oshifima, oruhere, pap, phutu, posho, sadza, ubugali,na umutsima
Sule Kisaka ni Mtanzania aishie Marekani hapa anaeleza namna rahisi ya kutengeneza unga wa ugali nyumbani unaotokana na nafaka zaidi ya moja kwa ajili ya chakula hicho.