SHAKA HAMDU KUTOKA KATIBU wa ITIKADI na UENEZI HADI MKUU wa WILAYA - "MPIGANAJI ASIYESHINDWA VITA"..

  Рет қаралды 6,609

Global TV  Online

Global TV Online

Күн бұрын

SHAKA HAMDU KUTOKA KATIBU wa ITIKADI na UENEZI HADI MKUU wa WILAYA - "MPIGANAJI ASIYESHINDWA VITA"
Januari 25, 20923, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan alifanya uteuzi wa wakuu wapya wa wilaya wapatao 37, kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 48 na wengine 55 kubakia kwenye vituo vyao.
Katika wakuu wapya wa wilaya yumo Shaka Hamdu Shaka. Kwa siku kadhaa kwenye Mtandao wa Twitter jina hilo limekuwa gumzo mno.
Hii ni baada ya kuteuliwa kwenye nafasi ya ukuu wa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro siku chache tu baada ya kukabidhi madaraka ya Katibu wa Itikadi ya Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa MNEC Sophia Mjema.
Baadhi ya wajuzi wa mambo kwenye Twitter wanadai kuwa, cheo alichokabidhi kwa Sophia ni kikubwa mno kwa sababu kinampa mamlaka kufanya kazi nchi nzima na siyo wilaya moja tu ya Kilosa.
Kutoka Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi hadi ukuu wa wilaya na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya wanasema ni mbingu na ardhi.
Lakini je, umepata kumjua huyu Shaka Hamdu Shaka ni nani? Ni jukumu la Global TV kukujuza usiyoyajua juu ya kiongozi f’lani;
Shaka Hamdu Shaka ni mzaliwa wa Mwambao wa Bahari ya Hindi katika Visiwa vya marashi ya karafuu; yaani Zanzibar.
Ukiachana na mambo ya shule na vyuo ambapo amepita sehemu mbalimbali, lakini Shaka Hamdu Shaka amepata mafunzo kutoka kwenye Chama chake cha CCM na viongozi wakongwe wa Taifa hili na kupitia tanuru la kuoka viongozi la UVCCM ambalo ni Taasisi ya Umoja wa Vijana wa CCM.
Shaka Hamdu Shaka amepita kwenye nyadifa mbalimbali ndani ya chama akianzia Chipukizi akiwa Ikulu Zanzibar, UVCCM Taifa na CCM Mkoa wa Morogoro.
Huko kote alipigana vita nyingi na aliibuka mshindi, hata kule Mikumi aliwaheshimisha wana CCM katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Global TV imehudhuria mikutano na vikao vya Shaka Hamdu Shaka ambaye amekuwa hasiti kusema kuwa anaamini katika kufanya mambo mema zaidi kwa watu kuliko jinsi watu wanayomfanyia yeye na ndiyo tafsiri yake ya mafanikio.
Kwa mujibu wa Shaka Hamdu Shaka, yeye haamini katika kusubiri fursa, anaamini katika kutengeneza fursa.
Shaka alikaa muda mrefu akiwa ni Kaimu Katibu Mkuu Jumuiya ya Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa bila kuthibitishwa rasmi kuwa Katibu Mkuu UVCCM Taifa lakini hakuwahi kusikika akilalamika juu ya jambo hilo na badala yake alipambana vilivyo na kufanikiwa kumudu vyema majukumu yake na kuisimamisha vyema UVCCM na kufanya iwike vizuri kuliko Jumuiya nyingine yoyote ya chama hicho.
Hata wakati akiwa Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro alipita kwenye misukosuko mingi kutokana na upekee wa siasa za Morogoro, lakini kwa utendaji wake Mkoa wa Morogoro ulipata nafasi za ubunge na udiwani nyingi za kupita bila kupingwa na kura nyingi za Urais CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: ndstream.net/gl...
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:apple.co/38HjiCx
⚫️ VISIT COMEDY PLAYLIST: • GLOBAL COMEDY/MOVIES
⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 657 693 210), ( +255 713 750910)
⚫️ Email: globaltvonlinenews@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com
⚫️ OUR PLAYLISTS:
⚫️ MICHEZO na BURUDANI: • Habari zote za michezo...
⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: bit.ly/mikasa_y...
⚫️ GLOBAL RADIO TV: bit.ly/255globa...
⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: bit.ly/exclusiv...
⚫️ Subscribe Global TV bit.ly/globaltv...

Пікірлер: 8
@globaltv_online
@globaltv_online Жыл бұрын
SUBSCRIBE NOW NA BONYEZA ALAMA YA KENGELE🔔 UWE WA KWANZA KUONA👉 bit.ly/3MraYdQ
@AlenKinyina
@AlenKinyina Жыл бұрын
Praise team
@noelbryson7840
@noelbryson7840 Жыл бұрын
Dada me nadhani utatuletea watu watakaokuja na suluhisho la mfumuko wa bei kinyume chake unakuja na habari za Shaka.. kweli??? Umetukosea sana..
@wazirally1791
@wazirally1791 10 ай бұрын
Asitupange hapo alifeli haswwaaaaaaaa
@nabillkhamis8188
@nabillkhamis8188 Жыл бұрын
Hana lolote
@Atmospherec3
@Atmospherec3 Жыл бұрын
Hana elimu au alifeli? Kwa mujibu wa wanaoelewa mambo umeficha kitu apo.
@evaristmbuya6220
@evaristmbuya6220 Жыл бұрын
🤣🤣🤣🤣
HISTORIA: RAIS Aliyekatwa Masikio Akiwa Hai, Na Yeye Aliwakata Wengine
18:44
Angry Sigma Dog 🤣🤣 Aayush #momson #memes #funny #comedy
00:16
ASquare Crew
Рет қаралды 50 МЛН
Как подписать? 😂 #shorts
00:10
Денис Кукояка
Рет қаралды 5 МЛН
Самое неинтересное видео
00:32
Miracle
Рет қаралды 2,6 МЛН
Charles Hilary wa Ikulu Zanzibar afunguka Kuhusu kwao na makuzi yake
4:00
Zanzibar Kamili TV
Рет қаралды 82 М.
HAYAWI HAYAWI YAMEKUWA ZANZIBAR, KWEREKWE & JUMBI IKO HIVI
9:15