Рет қаралды 51,270
Mpasuko katika muungano wa Azimio la Umoja one kenya umeendelea kuibua cheche huku baadhi ya vigogo wa chama hicho wakipinga mazungumzo yoyote na serikali ya kenya kwanza. Akizungumza katika mkutano wa chama cha wiper jijini nairobi, kiongozi wa chama hicho kalonzo musyoka, amesema kwamba hatatumika kusafisha jina la kenya kwanza ambalo limechafuka.