Рет қаралды 288
Wanafunzi 73 Kati ya 82 waliojeruhiwa na radi jana Januari 27, 2025 na kulazaa katika hospitali mbalimbali wilayani Bukombe - Geita wameruhusiwa kurejea nyumbani.
Kwa sasa majeruhi tisa (9) bado wanaendelea na matibabu katika hospitali ya St. Paul na hali zao zinaendelea kuimarika huku Mkuu wa mkoa huo, Martine Shigela ametembelea eneo la tukio, wazazi wa walioathiriwa kutoa pole kwa niaba ya serikali na kutoa maagizo ya tahadhari zinazopaswa kuchukuliwa.
#AzamTVUpdates
✍ Ester Sumira
Mhariri | John Mbalamwezi