No video

Maisha Ya Zuchu Kabla Ya WCB : "Nilitaka Kuwa Mwanasheria" | SALAMA NA ZUCHU PART 1

  Рет қаралды 288,752

YahStoneTown

YahStoneTown

Күн бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Kuna usemi mmoja unaenda kama hivi, kulea mimba si kazi ila kazi ni kulea mtoto, tafsiri yangu naamini mhenga hapo alikua anatuambia kazi pengine inaanza baada ya kupata kazi, tunaelewa jinsi gani ambavyo kupata kazi huwa ni kazi. Tena kazi yoyote, haijalishi kama ni ya upishi au ulinzi au ufundi au hata u daktari, mi nawajua madaktari kadhaa ambao nao pia wanapata shida kupata hizo kazi. Na baada ya kupata shida zote hizo wakati wa kutafuta kazi basi kazi halisi huanza pale unapoipata sasa hiyo kazi yenyewe.
Kazi ya Zuchu ilianza kabla hajaipata hiyo kazi yenyewe na ilikua kazi haswa kuipata na Mama yake Bi Khadija Kopa ndo alikua kinara kwenye hiyo connection ambayo Binti yake alikua anaitaka ili aweze kuwa msanii wa Diamond, na hayo ndo yalikua maneno yake hasa, toka alivyorudi kutoka Nigeria kwenye mashindano ya kusaka vipaji na alikua hajielewi elewi kwa kiasi flani ni kitu gani alikua anataka kufanya na kama basi kutakua na la kufanya inabidi liwe kutoka WCB na sio sehemu nyengine yoyote na agulia nini kilitokea? WCB aliipata na kilichokua kinatakiwa baada ya hapo ni UVUMILIVU wa HALI YA JUU.
Kwenye vitabu vyangu vyote Bi Zuhura Othman Soud ndo muandishi wangu BORA wa KIKE kuwahi kutokea katika kizazi chetu hiki cha Bongo Flava, na naweza sema hivyo wakati wowote iwe usiku au mchana, kipaji hicho ndicho kilichonifanya mimi nistaajabu sana na kutaka kuongea nae na kumuuliza yote yale ambayo nilikua nataka kumuuliza, ingawa humo humo nilikua nishajijibu kutoka kwenye historia ya familia atokayo ingawa hiyo haikutakiwa ndo iwe lazima, lazima mtoto wa Khadija Kopa na Othman Soud awe muandishi mzuri maana wazazi wake wamejaa vipaji tena na Baba yake ndo muandishi mkubwa wa nyimbo nyingi za Mama yake zilizowahi kuvuma.
Kwa umri wake wakati mwengine hujiuliza kajuaje haya maneno yote, anajua maana yake hii? Kasikia wapi hili neno au pengine je huwa anamfikiria Mama yake (ambaye ndo kipenzi chake na ndo amemlea) wakati anaandika hii? Anaona aibu? Je huwa wanaongelea hayo mashairi wanapokua wawili tu? Mazungumzo huendaje?
Sasa turudi kwenye kazi hiyo ya kuanza kuifanya baada ya kuipata sasa WCB, ukiachana na msoto mrefu alopitia, WCB wenyewe walikua waangalifu sana kwenye mipango ambayo ilikua ikiandaliwa kwaajili yake, yeye ndo msanii wa KWANZA wa KIKE kuwahi kutokea kwenye label kwahiyo ukichana na kipaji pia uwekezaji wa hali ya juu ulitakiwa ufanyike and boy they did that. Toka single yake ya kwanza mpaka wakati naandika hii Zuchu hakuwahi kuwa na kazi chafu, album yake ya kwanza alotoka nayo ya I am Zuchu ilikua na nyimbo 7 ambazo zote zilienda kufanya vizuri, na mpaka leo kila wimbo ambao anaachia ni wa moto, tukisema namba moja nadhani namba zake pia zinasema hivyo za kila sehemu, hakuna chumvi yoyote ndani yake.
Vipi sasa anaweza ku maintain hii schedule yake ilojaa mambo kuanzia asubuhi mpaka usiku? Kutoka Jumatatu mpaka Jumapili? Je ana muda kwaajili yake? Ana mpenzi? Mipango yake je? Endelevu? Vipi hizi title ambazo tunampa anazichukuliaje? Kuna pressure yoyote? Na kuhusu familia je? Kuna pressure yoyote kwenye baadhi ya mambo na maamuzi? Na kwenye label nako? Watu na furaha na kazi yake?
Kwa kuanzia msimu wetu wa TANO nadhani introduction ya Ms Zuchu inatufaa sana na yangu matumaini uta enjoy pia.
Asante kwa support ya toka siku ya kwanza ulipoanza kutupa macho na masikio yako.
You’re the best, nakukumbusha tu kwamba mengi yajayo yatakufurahisha In Shaa Allah maana kazi ndo kwaanza imeanza.
Love,
Salama

Пікірлер: 246
@kanyamaladembelesacko2812
@kanyamaladembelesacko2812 Жыл бұрын
Zuchu kuolewa na Simba ni inshu Kali Sana kwasababu zuchu anaakili kdg, anaweza kuongea anaweza kuelezea in shot anajitaidi Sana anafaa kuwa mke wa boss, blessed.
@fathiyaomar9009
@fathiyaomar9009 Жыл бұрын
Omar aliumwa sana na alikuwa rafikiyangu sana na mara ya mwisho aliimba gofu lakini alikuwa tayari anaumwa mwenyezi mungu amsameh makosa yake na sisi pia amin
@rosemahenge9071
@rosemahenge9071 Жыл бұрын
Marehemu anasamehewaje jamani kama hakutubu angali hai ndiyo basi tena ila sisi tulio hai ndio twapaswa kutubu makosa yetu na Mungu mwenye rehema atatusamehe🤲
@ukhtyzainab7254
@ukhtyzainab7254 Жыл бұрын
Aamiin
@alwatansharyf9294
@alwatansharyf9294 Жыл бұрын
@@rosemahenge9071 sisi waislamu tunayo nafasi ya kuwaombea dua watu wetu waliokwishaondoka duniani ni zawadi pekee Mola wetu alotujaalia kuwatunuku watu wetu
@rosemahenge9071
@rosemahenge9071 Жыл бұрын
@@alwatansharyf9294 Kumbe!!
@salomewandya7257
@salomewandya7257 Жыл бұрын
@@alwatansharyf9294 kabisaa na ndiyo maana uwa wanasomewa dua marehemu
@user-hl4zm2kc6o
@user-hl4zm2kc6o 10 күн бұрын
This has to be the best interview ever
@catenzeki678
@catenzeki678 Жыл бұрын
Mimi nakupa SHADA LA MAUA na pongezi nyingi ukiwa hai kwa kazi nzuri.Naomba umlete Harmonize,Roma na Stamina
@yakobomsafiri692
@yakobomsafiri692 Жыл бұрын
Salama mungu akubariki na akutie nguvu katika kazi yako bado uturetee daimond platnumz
@janethmihayo6337
@janethmihayo6337 Жыл бұрын
Nimekupendq zuchu wew mara ya kwanza leo❤️❤️❤️❤️Nakupenda
@salamwagilo
@salamwagilo Жыл бұрын
Amazing interview..Zuchu anaongea vzur sana n yuko real yaan
@charliestyles5535
@charliestyles5535 Жыл бұрын
Bonge la interview! Please we also need interview ya salama na sky tanzania,itakuwa balaa 🙌
@aminaomary5567
@aminaomary5567 Жыл бұрын
Huyu mtoto namkumbuka toka akiwa mdogo anakuja na MAMA yake Ushirika Club Mtwara 93.Zuchu anaimba vibaya sana.👍👍👍😁😁😁
@AfiSoul103
@AfiSoul103 Жыл бұрын
Nampenda Salama jamani.. she's natural
@athumanahmadramadhan9220
@athumanahmadramadhan9220 Жыл бұрын
Natamani napenda na nataka sana siku moja umlete Alhaji Dr Sule kwenye interview hii nzuri inayonipa elimu pia ktk maisha haya
@wakisawakisa5455
@wakisawakisa5455 Жыл бұрын
ckutegemea kama Zuchu angezungumza vzr namna hii, kuna vitu vya msingi ktk tasnia yetu ya muziki na maisha kwa ujumla amevizungumza cjui kama watu wamevinote...anyways, asilimia kubwa ya wanaokuja hapo huwa wanafanya hvyo ila kuna muda hutegemei sana kwa mtu huyo but hii imenifurahisha coz ckutegemea, it's good...Love u Zuu
@kantai737
@kantai737 Жыл бұрын
Zuchu is very intelligent na mature, listen to all her interviews and u will be impressed, it’s only that she has a bubbly personality and petite body so ppl think she is childish.
@joysarah
@joysarah Жыл бұрын
You can't get tired listening to her interviews..our smart queen 🔥🔥
@productivityprogressprince5156
@productivityprogressprince5156 Жыл бұрын
She’s soo smart and soo real.
@victoriamkumbo5866
@victoriamkumbo5866 Жыл бұрын
Zuchu nakupenda sana kwani uko lmakini hakiwewe mtotowa mtani usiyumbishwe nakupenda asante mwanangu
@somaliandnorway
@somaliandnorway Жыл бұрын
Zuchu i understand your pain my grand ma dies and i was not told and i was also in bording school..it hapoened the same to me and now i lost my mum 4 months ago …death is painful😢😢😢
@mrishojumaamrisho3212
@mrishojumaamrisho3212 Жыл бұрын
S0 sorry brother its god way
@niyonkurufadhoulillah4916
@niyonkurufadhoulillah4916 Жыл бұрын
You know what ? Mimi nazani wawekezaji wawekeze kwenye club ya ma star iwe VIP yani isiw fasi ya show no iwe fasi yao ya ku enjoy tu afu kingilia kiwe ju sana kwa watu wasio kuwa marufu so then wa sani munaweza kua muna enjoy maisha yale munayo ya miss kama watu wangine wote sababu sizani kama msani kama msani ni rahisi kutoka kwenda club ao kwenye migahawa
@yustayusuph9101
@yustayusuph9101 Жыл бұрын
Daaa! hadi mimi nimelia story ya omari 😭😭
@theodoreconstantine2565
@theodoreconstantine2565 Жыл бұрын
Huyo ndo salama banna lazima akulize alaf akuchekeshe you are the best salamaa I appreciate your work .
@diva_20162
@diva_20162 4 ай бұрын
I like her voice jaman Mungu fundi asee ❤❤
@sarahlondo7597
@sarahlondo7597 Жыл бұрын
Was really waiting for this one😂😂❤️‍🔥❤️‍🔥
@edgardevis8152
@edgardevis8152 Жыл бұрын
🙌🙌🙌👌👌👌👌🙏 aunt salama respect Sana naomba umlete na marioo plz
@ibrahimhumanamicroscopic6515
@ibrahimhumanamicroscopic6515 Жыл бұрын
First time to listen zuchu voice 🥰🥰 that's was nice
@sistersade9039
@sistersade9039 Жыл бұрын
Lovely interview and it's wonderful to get to know zuchu closer. Salama wewe ni bigwa wa watangazaji unajua ivyo sio? All the best 🥰
@melangachikubati9253
@melangachikubati9253 Жыл бұрын
Salama please, if posible find time for sky worker a real jita man with wonderful voice ever, i am watching all the way from Ukerewe the sunshine ground.
@modysaid8439
@modysaid8439 Жыл бұрын
Hy zuu Mimi ni fan wako but kuna kitu naomba urekebishe,ukiwa Kwa interview usionge wakati unaulizwa swali just wait untill swali liishe ulielewe coz sio Kila interviewer ni anakupenda so anaweza kutumia weakness yako ya ku interrupt swali na ku kufanya ujibu kitu ambacho sio sawa so jaribu kuwa calm coz your a superstar my dear
@anthonym2542
@anthonym2542 Жыл бұрын
Sijaskiza interview lakini Akili Yako IPO sawa kaka
@hawasaid7151
@hawasaid7151 Жыл бұрын
Good 👏👏
@awatifalghanim1106
@awatifalghanim1106 8 ай бұрын
Ni kweli umesema👍
@sifasiraji2903
@sifasiraji2903 Жыл бұрын
Zuchu kama Zuchu❤️
@sporttv9449
@sporttv9449 Жыл бұрын
Hapo pa "aaaahaa mimba".hiyo nimeipenda ha ha ha
@irenevicky4656
@irenevicky4656 Жыл бұрын
Zuchu you are 👌👍a star lots of love❤❤❤💖💖
@eliassanga6907
@eliassanga6907 Жыл бұрын
Joelnanauka na MaxRioba fanya ivi vichwa vidondoke studio vina madini
@msafirimbeya3329
@msafirimbeya3329 Жыл бұрын
Umetisha
@jamaalsaleem2926
@jamaalsaleem2926 Жыл бұрын
Wakwanza kucoment🔥🔥
@shuu62
@shuu62 Жыл бұрын
Finally, it's here‼️ Keep up the great work girls 😊
@mahmoudaziz4717
@mahmoudaziz4717 Жыл бұрын
Big up salama. Nime enjoy interview mzuri kiswahili safi. Safi zuchu.
@maliamjuma9376
@maliamjuma9376 10 ай бұрын
nawapenda sana munguawabariki lnshallah
@emanuelkiwanuka578
@emanuelkiwanuka578 Жыл бұрын
Asanteni nimeisubili kwa Hamu sana hii
@mwasitihamisi8421
@mwasitihamisi8421 Жыл бұрын
Ur my best interviewer ❤
@princessiyalicious4185
@princessiyalicious4185 Жыл бұрын
Salama unafnya kaz nzur sna....
@saluShop-jm5ku
@saluShop-jm5ku 20 күн бұрын
Munguu akuzidishiiiiee. Badooooo. Simbaaaaaa tuuuu
@hildahwangari4337
@hildahwangari4337 Жыл бұрын
She is doing good congrats
@judithjulius5993
@judithjulius5993 Жыл бұрын
Hivi watu wanaosemaga zuchu ana sura mbaya Wana Nini! Mbona Binti mrembo hivi
@EugeneUroki
@EugeneUroki 2 ай бұрын
Kwasababu anamakali😅
@hamedabashir9
@hamedabashir9 Жыл бұрын
Niliisumbilia sana 💋🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿♦️❤️😍
@mwabiawahadi6247
@mwabiawahadi6247 Жыл бұрын
Nakukubali Sana Zuch
@samilaamlli3474
@samilaamlli3474 Жыл бұрын
ilove you zuchu
@SultanDean
@SultanDean Жыл бұрын
I love your interviews. They are so deep and informational
@supertal2943
@supertal2943 Жыл бұрын
Awesome interview ever👌
@samtelah7578
@samtelah7578 Жыл бұрын
Mlete Diamond
@wardatkhamis3703
@wardatkhamis3703 Жыл бұрын
Mtihani eti mungu jaman kweny balaa hili pia mung anashirikishwa??? Au ni bilisi ndio mwenyw jmn
@piusphilip307
@piusphilip307 Жыл бұрын
You are really cofident, yaani huigizi, I like you
@browngennestone5979
@browngennestone5979 Жыл бұрын
GOOD WORK
@Nzirubusaabudara-nb1bm
@Nzirubusaabudara-nb1bm 8 күн бұрын
Ongera sana dada
@remybuyenzi1856
@remybuyenzi1856 Жыл бұрын
❤❤❤❤❤❤ nimekua naisubiri kwa ham kubwa
@kantai737
@kantai737 Жыл бұрын
Finally was really waiting for this
@paulonjozi1638
@paulonjozi1638 Жыл бұрын
Naitaman nakuisubr salama na young killer msodok
@marymsaid3540
@marymsaid3540 Жыл бұрын
Nampenda sana zuchu ❤❤
@foodbasiccourt2028
@foodbasiccourt2028 Жыл бұрын
Hata mimi ila kuwa na mahusiano na kiruka njia diamond i am worried for her career
@SAVPTVOnline
@SAVPTVOnline Жыл бұрын
good girl
@radjabreezy5564
@radjabreezy5564 Жыл бұрын
🇷🇼🇷🇼🇷🇼Salama asante kwaku tuletea Mzee wetu 🇷🇼Sheikh Kipozeo Asante kwa elimu 😊😊😊 ila sijapenda huja mkirimu Sheikh sijapenda lol tumependa kipindi next Time tutapenda kumuona Sheikh Mazinge mbele ya camera love from Rwanda🇷🇼
@florencekaranja8736
@florencekaranja8736 Жыл бұрын
Everyday I was checking on this interview en now here it is
@mochakeno9123
@mochakeno9123 Жыл бұрын
My own girl
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 Жыл бұрын
Tuli kata tamaaa kabisa eeh🙄🙄🙄😢😢
@isharsalim454
@isharsalim454 Жыл бұрын
😆
@bintykigan7309
@bintykigan7309 Жыл бұрын
Niliisubiri Sana hii❤️❤️❤️❤️🇰🇪🇰🇪🇰🇪
@kristofuraha3369
@kristofuraha3369 Жыл бұрын
Nimefurahi sana aisee!!🔥❤👊
@vanessakiwia7890
@vanessakiwia7890 Жыл бұрын
Zuchu we comedian ila ujijui wallay 🤣🤣🤣 yani mwanzo mwisho nacheka wallay
@lulu-xd7to
@lulu-xd7to Жыл бұрын
Na story ya Omar umecheka
@jokhaaliy3720
@jokhaaliy3720 Жыл бұрын
Music na law bora dhambi kubwa ipi
@RuzoOwzy
@RuzoOwzy Жыл бұрын
00:50 Subira yavuta kheri. Haraka haraka haina baraka. Hizi si zinashabihiana, ziko fresh tu. Au kachanganya na Ngoja ngoja huumiza matumbo!!!
@rosenamilia4140
@rosenamilia4140 Жыл бұрын
Zuchu ingefurahisha zaidi kutoa heshima, hasa kwa wale waliokuzidi umri kwani Kiafrika ni hekima na busara na hutapungukiwa na kitu. "SHKAMOO DADA SALAMA".Ingekuheshimisha zaidi.Lakini hukuliona hilo.Pole sana 😢
@allytauka8196
@allytauka8196 Жыл бұрын
Zanzibar chei chei inasimama on behalf of shikamoo and she used it
@kantai737
@kantai737 Жыл бұрын
😂😂😂😂 shikamoo tena salama hataki uzee.binadamu acheni gubu. Such a lovely interview hujaona lengine.
@prettypretty9745
@prettypretty9745 Жыл бұрын
Hapo washirazi wamekutana chechei imekaa mahala pake👌👌
@kenty101
@kenty101 Жыл бұрын
Rosena nini buana... Kssema chei chei. 🤣🤣🤣🤣
@isharsalim454
@isharsalim454 Жыл бұрын
Chei chei kwetu ni heshima
@jamilamasoud3800
@jamilamasoud3800 Жыл бұрын
Baada yakuisubiri kwa muda mrefu
@mammymammy997
@mammymammy997 3 ай бұрын
Zuchu Allah amubariki nampenda sana
@queenlinda255
@queenlinda255 Жыл бұрын
Amevaa viatu gani jamani huyu binti 😂😂😂
@fortunatemushi4943
@fortunatemushi4943 Жыл бұрын
Yaani mpaka nimecheka! Hayo maviatu hapana hata kama fashion mmh mi hapana
@mariammariam6356
@mariammariam6356 Ай бұрын
Kwanza hivi viatu ni vya ndani sio vya out😂😂​@@fortunatemushi4943
@jennytugara9470
@jennytugara9470 Жыл бұрын
Go for it girl. elimu haikomi hata kina Kardashian wanafanya urembo na kasoma Sheria juu yake. Music ni era inafika mahali inaisha.
@alhamdullilla5108
@alhamdullilla5108 Ай бұрын
Amebarikiwa kwa kufanya Haramu😢😢😢
@stevennyondo2215
@stevennyondo2215 Жыл бұрын
Kweli mlikuwa closer hadi unamwambia kaka nimevunja ungo!!😂
@siaammo1104
@siaammo1104 Жыл бұрын
Haswaaa duh
@saudahassan6667
@saudahassan6667 Жыл бұрын
Nakupenda sana salama na zuchu
@chaneldici4083
@chaneldici4083 Жыл бұрын
My salama jabir❤❤ from🇧🇮
@rogersodero3897
@rogersodero3897 Жыл бұрын
Pls bring Esha Buheti
@zizahissa8642
@zizahissa8642 Жыл бұрын
I was really waiting for loooooog 🙌🙌🙌🙌❤️❤️❤️
@user-wv7ft8tm3z
@user-wv7ft8tm3z Ай бұрын
Voice is👌
@winfridangoloke1916
@winfridangoloke1916 Жыл бұрын
Hatimaeeeeee
@stellah3844
@stellah3844 Жыл бұрын
Zuchu💓💓💓💓
@esthermusanga8118
@esthermusanga8118 Жыл бұрын
Hongera zuchu kazi smart
@user-ql7wu9vm5s
@user-ql7wu9vm5s 4 күн бұрын
I can't watch this. Am an emotional person. That story touch me. I love both of u.
@loganpoul
@loganpoul Жыл бұрын
Salama lakini wajua nakupenda Sana?mamangu pia anaitwa salama so nikikuona naburudika Sana kama namuona mamangu,
@japhtv9858
@japhtv9858 Жыл бұрын
Oya kingereza kingi bhana
@evanathings9554
@evanathings9554 Жыл бұрын
I love Zuchu ❤
@JumaKasikile
@JumaKasikile 2 ай бұрын
Hello zuchu❤❤❤❤❤
@EugeneUroki
@EugeneUroki 2 ай бұрын
🎉🎉🎉
@hamisamsimbe4613
@hamisamsimbe4613 Жыл бұрын
Mm mwenyewe nilimpenda sana omary kopo mungu amsamehe dhambi zake
@zaynabmwanjovu8277
@zaynabmwanjovu8277 Жыл бұрын
Omary Kopa,,not Kopo
@aishambise6529
@aishambise6529 Жыл бұрын
Nawapenda sanaas ❤❤❤❤🙏🏻
@yasintadavid1296
@yasintadavid1296 Жыл бұрын
Thanks
@keyla3641
@keyla3641 Жыл бұрын
Interview nzuri sana
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 Жыл бұрын
Au bi kikalala au mzeee kikalala tuomba
@user-xf9or5cv1d
@user-xf9or5cv1d Жыл бұрын
Tubia nyimbo ni hapa duniani akhera haiko mbali
@lareineminah1353
@lareineminah1353 Жыл бұрын
Tuulisubiriii sana😍😘
@farajavilla2379
@farajavilla2379 Жыл бұрын
Mziki sio masiharaaa na hanstone kapewa uo mtihani wa kustahmili lkn umemshinda
@abenawemubaraka6681
@abenawemubaraka6681 Жыл бұрын
Zucu y Lev u 2 am mubaraka from kanpara
@iddmohammed1086
@iddmohammed1086 Жыл бұрын
Lafudh tamu mno ya kizanzibari baina ya wazanzibari hawa wawili.
@remybuyenzi1856
@remybuyenzi1856 Жыл бұрын
Zuchu wetu
@jamilamasoud3800
@jamilamasoud3800 Жыл бұрын
Baada yakuisubiri kwa muda mrefu
@mahfoudh.official7318
@mahfoudh.official7318 Жыл бұрын
Wa zanzibar 2 🎤🌍
@aishadotto3640
@aishadotto3640 Жыл бұрын
Pole Zuchu
@ismailissa3996
@ismailissa3996 6 ай бұрын
Comment za mungu am,bariki mungu gani uyo anaependa huwo upuuzi wake
@shaluuanthony1836
@shaluuanthony1836 Жыл бұрын
Our zuchu
@user-ki9le1jy8e
@user-ki9le1jy8e 2 ай бұрын
Wanao uliza kuhusu uvaaj miwan sjui nguo sjui viatu jmn hili swal muwaulize mafundi huko viwandan najua wanajua walichokifanya mpk kutengez nasisi kukubali jmn wat mjaj maisha yenu mkuta wengin mnataman kupat alivyo navyo lkn ndo hivyo 😅😅
@rosemahenge9071
@rosemahenge9071 Жыл бұрын
Hahaha ila Zuchu na ucomedian anao🤣🤣
@mwanahawamohammed8540
@mwanahawamohammed8540 Жыл бұрын
Mmh. Hivo viatu tunavaa kwenye mazingira ya baridi, lakini kwenye joto jamani 🤣🤣
@jescakweka7355
@jescakweka7355 Жыл бұрын
Kuna baridi hapo si unajua 😂 kiyoyozi
@mwanahawamohammed8540
@mwanahawamohammed8540 Жыл бұрын
@@jescakweka7355 🤣🤣🤣
Baba Olivia Episode 17 Finale❤️// Single Father Story
31:59
Henry Mwakajumba
Рет қаралды 12 М.
Dad gives best memory keeper
01:00
Justin Flom
Рет қаралды 19 МЛН
WALIMDHARAU KWASABABU YA KINYAGO KUMBE NI MTOTO WA MFALME | MOVIE KWA KISWAHILI
28:46
Mkasi - SO4E01 with Diamond Platnumz
27:57
MkasiTV
Рет қаралды 1 МЛН
Dad gives best memory keeper
01:00
Justin Flom
Рет қаралды 19 МЛН