Zuchu : "Nilipeleka Nyimbo Kama Tano, Diamond Alizikataa Zote" | SALAMA NA ZUCHU

  Рет қаралды 122,921

YahStoneTown

YahStoneTown

Жыл бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Kuna usemi mmoja unaenda kama hivi, kulea mimba si kazi ila kazi ni kulea mtoto, tafsiri yangu naamini mhenga hapo alikua anatuambia kazi pengine inaanza baada ya kupata kazi, tunaelewa jinsi gani ambavyo kupata kazi huwa ni kazi. Tena kazi yoyote, haijalishi kama ni ya upishi au ulinzi au ufundi au hata u daktari, mi nawajua madaktari kadhaa ambao nao pia wanapata shida kupata hizo kazi. Na baada ya kupata shida zote hizo wakati wa kutafuta kazi basi kazi halisi huanza pale unapoipata sasa hiyo kazi yenyewe.
Kazi ya Zuchu ilianza kabla hajaipata hiyo kazi yenyewe na ilikua kazi haswa kuipata na Mama yake Bi Khadija Kopa ndo alikua kinara kwenye hiyo connection ambayo Binti yake alikua anaitaka ili aweze kuwa msanii wa Diamond, na hayo ndo yalikua maneno yake hasa, toka alivyorudi kutoka Nigeria kwenye mashindano ya kusaka vipaji na alikua hajielewi elewi kwa kiasi flani ni kitu gani alikua anataka kufanya na kama basi kutakua na la kufanya inabidi liwe kutoka WCB na sio sehemu nyengine yoyote na agulia nini kilitokea? WCB aliipata na kilichokua kinatakiwa baada ya hapo ni UVUMILIVU wa HALI YA JUU.
Kwenye vitabu vyangu vyote Bi Zuhura Othman Soud ndo muandishi wangu BORA wa KIKE kuwahi kutokea katika kizazi chetu hiki cha Bongo Flava, na naweza sema hivyo wakati wowote iwe usiku au mchana, kipaji hicho ndicho kilichonifanya mimi nistaajabu sana na kutaka kuongea nae na kumuuliza yote yale ambayo nilikua nataka kumuuliza, ingawa humo humo nilikua nishajijibu kutoka kwenye historia ya familia atokayo ingawa hiyo haikutakiwa ndo iwe lazima, lazima mtoto wa Khadija Kopa na Othman Soud awe muandishi mzuri maana wazazi wake wamejaa vipaji tena na Baba yake ndo muandishi mkubwa wa nyimbo nyingi za Mama yake zilizowahi kuvuma.
Kwa umri wake wakati mwengine hujiuliza kajuaje haya maneno yote, anajua maana yake hii? Kasikia wapi hili neno au pengine je huwa anamfikiria Mama yake (ambaye ndo kipenzi chake na ndo amemlea) wakati anaandika hii? Anaona aibu? Je huwa wanaongelea hayo mashairi wanapokua wawili tu? Mazungumzo huendaje?
Sasa turudi kwenye kazi hiyo ya kuanza kuifanya baada ya kuipata sasa WCB, ukiachana na msoto mrefu alopitia, WCB wenyewe walikua waangalifu sana kwenye mipango ambayo ilikua ikiandaliwa kwaajili yake, yeye ndo msanii wa KWANZA wa KIKE kuwahi kutokea kwenye label kwahiyo ukichana na kipaji pia uwekezaji wa hali ya juu ulitakiwa ufanyike and boy they did that. Toka single yake ya kwanza mpaka wakati naandika hii Zuchu hakuwahi kuwa na kazi chafu, album yake ya kwanza alotoka nayo ya I am Zuchu ilikua na nyimbo 7 ambazo zote zilienda kufanya vizuri, na mpaka leo kila wimbo ambao anaachia ni wa moto, tukisema namba moja nadhani namba zake pia zinasema hivyo za kila sehemu, hakuna chumvi yoyote ndani yake.
Vipi sasa anaweza ku maintain hii schedule yake ilojaa mambo kuanzia asubuhi mpaka usiku? Kutoka Jumatatu mpaka Jumapili? Je ana muda kwaajili yake? Ana mpenzi? Mipango yake je? Endelevu? Vipi hizi title ambazo tunampa anazichukuliaje? Kuna pressure yoyote? Na kuhusu familia je? Kuna pressure yoyote kwenye baadhi ya mambo na maamuzi? Na kwenye label nako? Watu na furaha na kazi yake?
Kwa kuanzia msimu wetu wa TANO nadhani introduction ya Ms Zuchu inatufaa sana na yangu matumaini uta enjoy pia.
Asante kwa support ya toka siku ya kwanza ulipoanza kutupa macho na masikio yako.
You’re the best, nakukumbusha tu kwamba mengi yajayo yatakufurahisha In Shaa Allah maana kazi ndo kwaanza imeanza.
Love,
Salama

Пікірлер: 171
@elizabethmapunda
@elizabethmapunda Жыл бұрын
Napenda zuchu anavyoongea very charming😍
@nurutatu4031
@nurutatu4031 Жыл бұрын
One of the best interviews ever. Keep it up Salama and Zuchu👏🏽
@chancystv3138
@chancystv3138 Жыл бұрын
Watu wa Zuchu gongeni like hapa 🙌
@zamzamsharif9776
@zamzamsharif9776 Жыл бұрын
ILike her she’s down to earth. Loove from Ireland 🇮🇪 ❤
@handwatchmaro4124
@handwatchmaro4124 Жыл бұрын
Leo nmejikuta nampenda Zuhura😍 zaidi ya Zuchu
@BigZhumbe
@BigZhumbe Жыл бұрын
Zuu you are great 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥 simba jike umebebwa ukabebeka hadi wasafi waliokubeba wanaijoi na mashabiki tuna have fun.
@hamismkude553
@hamismkude553 Жыл бұрын
Nawakubali sana zuchu na salama kila mtu ana play party yake vzr yaan salama anajua kuuliza maswali na zuchu anajua kujibu maswali
@rosemahenge9071
@rosemahenge9071 Жыл бұрын
Hakuna kitu kizuri kama kuangalia interview ya mtu mchangamfu kama Zuchu 🥰🥰🥰
@kantai737
@kantai737 Жыл бұрын
For real her interviews are always a vibe Na she is really intelligent everytime ukiskia interview zake u can’t help but love her more.
@BigZhumbe
@BigZhumbe Жыл бұрын
Mimi interview hata iwe masaa kumi naimaliza.... Yeye na Simba they are great kwenye interviews
@MrTop-wj7no
@MrTop-wj7no Жыл бұрын
@@BigZhumbe umepatia kabisa
@isharsalim454
@isharsalim454 Жыл бұрын
🥰🥰
@mamananga2849
@mamananga2849 Жыл бұрын
@@BigZhumbe sanaaa
@sarahlondo7597
@sarahlondo7597 Жыл бұрын
Aaaaw i love the way she is real❤️‍🔥🥰
@SultanDean
@SultanDean Жыл бұрын
Salama be asking all the right questions
@keyla3641
@keyla3641 Жыл бұрын
Zuchu akili nyingi usibadilike u are a good girl
@maijamtoso5673
@maijamtoso5673 Жыл бұрын
Interview Nzuri mno.. inafurahisha na kufunzaa
@mohamedrajab358
@mohamedrajab358 Жыл бұрын
Huyu binti yupo vizuri mno kwenye kichwa chake
@nyanziratatou5404
@nyanziratatou5404 3 ай бұрын
Ici kibindi nakipenda kwasababu hakina ushabiki kwata kwenye masali maswali yanaoulizwa yanajitosheleza . Kwakweli napenda da Salama.❤
@rehemaothman2475
@rehemaothman2475 Жыл бұрын
Majibu ya ukomavu nakukubali zuchu🥰🥰🥰🥰😍
@hadijasalim7769
@hadijasalim7769 7 ай бұрын
Zuchu hadi umeniliza mamy nakupenda❤❤❤❤
@mariammbaruk8034
@mariammbaruk8034 Жыл бұрын
Niliisubir xanaa hii zuchu love u😘😘
@hopedj275
@hopedj275 Жыл бұрын
one of the best interview i have ever seen in my life
@diva_20162
@diva_20162 2 ай бұрын
Her voice God waoooh so wonderful 😊😊
@deborahcharles4916
@deborahcharles4916 3 ай бұрын
I love you zuchu haulingi dada
@elizabethotieno7270
@elizabethotieno7270 Жыл бұрын
Best interview ever,,,this girl is beautiful and wise
@hadiadaoman1981
@hadiadaoman1981 Жыл бұрын
Exactly even me I love her much more ♥️❤💖🥰
@eveodera6676
@eveodera6676 Жыл бұрын
Salama this is one of the best interviews. I love the way your calm and Zuchu is just awesome.
@goodlucksway1456
@goodlucksway1456 Жыл бұрын
👏👏👏yuko positive sana zuchu kama zuchu
@fortune3502
@fortune3502 Жыл бұрын
Interview nzuri sanaaa! Daa nimekapenda bureee katoto ka watu jaman
@violetandisi
@violetandisi 8 ай бұрын
i just love salama for some strange reason she is so real i mean she asks the correct questions in a polite manner and zuchu love the energy girl and the wisdom
@djibrilheradi8291
@djibrilheradi8291 Жыл бұрын
Happy for you zuchu,may Allah protect you
@estherjackson6038
@estherjackson6038 Жыл бұрын
Jamani mi naona maneno hapo juu nyuma ya Zuchu,KumaNoko Kula, au sioni vizuri.
@dayannahkopellah8396
@dayannahkopellah8396 Жыл бұрын
She is clever😇
@africanbeauty6556
@africanbeauty6556 Жыл бұрын
Proud of you Zuchu!! Keep it up don’t change 🥰
@kantai737
@kantai737 Жыл бұрын
You just can’t stop loving her❤
@sebastianmwakulya8146
@sebastianmwakulya8146 14 күн бұрын
Nimeangalia tena na tena hongereni sana kwa interview
@stellah3844
@stellah3844 Жыл бұрын
Nakupenda Zuchu💓💓💓
@jacintabati6238
@jacintabati6238 Жыл бұрын
ZUCHU my love🥰😘😍❤❤❤
@lulumalima1739
@lulumalima1739 9 ай бұрын
Nice much love and prayers from fellow Tanzanian women both you ladies
@allymakangana6450
@allymakangana6450 Жыл бұрын
salama ni muwazi sana sio mnafiki
@loiceamugune6711
@loiceamugune6711 Жыл бұрын
Salama you are one of the best interviewer
@MrTop-wj7no
@MrTop-wj7no Жыл бұрын
Interview nzuri Sana Kwa kweli,
@jessicahjohnstone7229
@jessicahjohnstone7229 Жыл бұрын
Best interview
@monicajohn2515
@monicajohn2515 Жыл бұрын
Yani salama ana bonge la interview saaaana big up salama
@claricejoshua820
@claricejoshua820 Жыл бұрын
She is very humble nimempenda
@kellymutabesha1876
@kellymutabesha1876 Жыл бұрын
Katoto kana akili mingi njomana simba kadata
@lynawamahoro3465
@lynawamahoro3465 Жыл бұрын
I like … wise one 👏
@princessiyalicious4185
@princessiyalicious4185 Жыл бұрын
Yeeee wakwanza mm leo
@salimdibundile4872
@salimdibundile4872 Жыл бұрын
Salama you are the best... Tunakuomba utuletee kipenzi chetu mbosso khan
@keyla3641
@keyla3641 Жыл бұрын
Hahaha nimeinjoi sana asante salama
@jabirsuleiman26
@jabirsuleiman26 Жыл бұрын
I like it 🎉
@Jaycollection
@Jaycollection Жыл бұрын
Interview nzuri sana
@gknifeboy9435
@gknifeboy9435 Жыл бұрын
Gud interview
@zhaujiakashindi6617
@zhaujiakashindi6617 Жыл бұрын
🥰😘Love you Salama❤️
@johariasanimatu2732
@johariasanimatu2732 Жыл бұрын
Zuchu my blood 🥰🥰🥰
@yvespungu3611
@yvespungu3611 Жыл бұрын
Nice interview
@kimah9461
@kimah9461 Жыл бұрын
Ikitajwa diamond platnumz zuchu ni mgin🙈🤣👏🤣🤣🤣Is all❤️ beautiful MashaAllah Keep going sis
@kantai737
@kantai737 Жыл бұрын
😂😂😂😂😂
@matanohassan9667
@matanohassan9667 Жыл бұрын
Nakupenda zuchu
@esthermusanga8118
@esthermusanga8118 Жыл бұрын
Also me I wish you all the best
@shilahshilah6136
@shilahshilah6136 Жыл бұрын
Mie ni mkenya lakini nampenda zuchu sana,,,,ningepewa nafasi nimuone tu ningeshukuru
@rosemarysiame8443
@rosemarysiame8443 Жыл бұрын
Jamn jaman this was funny jamn if you have crush with someone ooooh my god it's very jamn kafeeling kale duu
@vanessaphamarcy2134
@vanessaphamarcy2134 Жыл бұрын
Nimekupenda buleee unahekima kaza but
@ismailebani5262
@ismailebani5262 Жыл бұрын
Safi Zuchu
@remybuyenzi1856
@remybuyenzi1856 Жыл бұрын
❤❤❤❤
@TheMullins830
@TheMullins830 Жыл бұрын
This girl just has some good energy in her. She sounds so sincere when she speaks.
@blandinamyinga9489
@blandinamyinga9489 Жыл бұрын
Salama with her trick questions eti kwa vile SIMBA aliruka na wanawake wengine ukiwa na mimba 🤣🤣🤣🤣
@suroorAlafifi-ve8pk
@suroorAlafifi-ve8pk Жыл бұрын
Will see beautiful woman and I amazing thang 🥰 the best way to be careful about it and nice 🙂
@abdulraufmohammedsalum6806
@abdulraufmohammedsalum6806 Жыл бұрын
Salama🙌
@dilipdab3714
@dilipdab3714 Жыл бұрын
English.ipo.poa.lakini.salama.yupo.fresh
@aslayhassan2283
@aslayhassan2283 Жыл бұрын
I like it
@arnoldmangi2407
@arnoldmangi2407 Жыл бұрын
Iko poa sana
@marianusrutagwelera3013
@marianusrutagwelera3013 4 ай бұрын
Nice sr zuchu😮
@vincentmushi1247
@vincentmushi1247 Жыл бұрын
Ukisikia watu wanalalamika kuwa eti Mtu Anaongea kiingeeza wakati wa interview... Ujue hao watu hawajaenda shule...hahahaaaa, Kama unaelewa hauna muda wa kulalamika.. Ndio kiswahili ni lugha yetu na kiingeeza ni lugha pia... Nendeni tuition mkavunje yai jamani
@jasmineedamu6089
@jasmineedamu6089 Жыл бұрын
Achana na sisi😏
@fatmazullu4933
@fatmazullu4933 Жыл бұрын
@@jasmineedamu6089 🤣🤣🤣🤣
@minzamariamcasmir189
@minzamariamcasmir189 Жыл бұрын
Kweli kabisaa….watu wanabidi waelewe she’s an aspiring international artist if not one already so she needs to be accessible to everyone
@oxtinho159
@oxtinho159 Жыл бұрын
Wa kwanza
@mwanatz5980
@mwanatz5980 Жыл бұрын
😍😍😍
@nyotakaminkya714
@nyotakaminkya714 Жыл бұрын
J'aime tes paroles ina saidia mipango iliko kichwani
@mariamandambike5013
@mariamandambike5013 21 күн бұрын
Zuchu🔥🔥
@veronyanganda179
@veronyanganda179 Жыл бұрын
Mafanikio ya zuchu nyuma yake kna watu sahihi wa kwanza mama yake, na mpenzi wake daimondi.
@mohamedjuma1878
@mohamedjuma1878 Жыл бұрын
Ma Ami Leo mmekutana
@lareineminah1353
@lareineminah1353 Жыл бұрын
Mme kawiza kuyitowa La simba lisha kuwa waziiii🤣🤣🤣
@stephanocyprian2892
@stephanocyprian2892 Жыл бұрын
Pamojasana zuch
@NabakiZanzibar
@NabakiZanzibar Жыл бұрын
Kuipata hii ni bahati sana,
@maulidmalik5364
@maulidmalik5364 Жыл бұрын
Jaman sjaona msosi leo
@esthermbike3300
@esthermbike3300 Жыл бұрын
Wema sasa
@esthermusanga8118
@esthermusanga8118 Жыл бұрын
👋👋👋👍
@fatmasaid3536
@fatmasaid3536 Жыл бұрын
Kwajili ya kiki, she's been trained ili atakapo ulizwa kama anam date simba ajifanye shy ili ionekane kuna something kwa mtazamo wangu hamna lolote ila kiki tu.
@khadijahali4837
@khadijahali4837 Жыл бұрын
Weee hamna lolote kwl hy?
@KSJ6569
@KSJ6569 Жыл бұрын
Iyi nimarudiyo sio mpya
@vincentmushi1247
@vincentmushi1247 Жыл бұрын
Interview nzuri... Na hongereni wote... Zuchu Aka chuchu... Hapo kwenye ku date na simba... Hahahaaaa. Ni Swali gumu sana... Biggest mistake... Zuchu ni mtulivu lkn simba wetu bado ni kicheche.
@AfricaYangu
@AfricaYangu Жыл бұрын
All went well until u ask her about Diamond that's when she started behaving like a little girl
@successconcious703
@successconcious703 Жыл бұрын
😂😂😂😂💔💔
@nelialomnyaki
@nelialomnyaki 2 ай бұрын
Nimependa kingereza cha zuchu
@donraykiko4243
@donraykiko4243 Жыл бұрын
Kwaiyo kiswahili mpemba kinampiga chenga au ndo tunakomoana tu
@husseynomar9523
@husseynomar9523 Жыл бұрын
Salama tafadhali tuleteeni SHEIKH MUHIDDIN MAALIM SIASA NA SABRA MACHANO WATU ZANZIBAR
@mvponlinetv
@mvponlinetv Жыл бұрын
Ivi nyinyi wa sanii wa tanzania ndio hamuwezi kuongea bila yakuongea English au inakuwa nihashuo tu
@kidungweshaaban9317
@kidungweshaaban9317 Жыл бұрын
hujampa hat juice why!?our zuchu!!
@damariszuckschwert9489
@damariszuckschwert9489 Жыл бұрын
Hawa mababa wengi ni nyoko kabisa.
@mosah2851
@mosah2851 Жыл бұрын
Zuchu anasauti huyu mtoto!!
@judithjulius5993
@judithjulius5993 Жыл бұрын
Kato kadogo lakini kanaongea point tupu
@ZuwenaZuwena-oe9kk
@ZuwenaZuwena-oe9kk 2 ай бұрын
Jamani.mmeonavia2.vyadadae2.zuhura😂😂😂😂
@AllyForyour
@AllyForyour 6 ай бұрын
Lafudhi ya zuchu❤❤❤
@ashahamisi5884
@ashahamisi5884 Жыл бұрын
Leo sema no no lakini ipo siku utasema yes . Huwezi kuzuia mahusiano kamwe kua siry ficha social media tu.
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 Жыл бұрын
Mh😜
@anitakamene4656
@anitakamene4656 Жыл бұрын
Nice
@Dotto-hp3qf
@Dotto-hp3qf 6 ай бұрын
Ni nyimbo alikuwa anaipenda..na aliiagwa nayo. Ni nyimbo ya kumbukumbu kwako
@lissaseif4744
@lissaseif4744 Жыл бұрын
Weeeeee mbn umeliwa sasa
@yusternyirenda7231
@yusternyirenda7231 6 ай бұрын
Dalili zote zinaonyesha zuchu analala na diamond tena kwa asilimia elfu niko paleeeeeee! mapenzi! huwa hayajifichi ipo siku watashindwa kuendelea kuficha 😂😂😂
Who has won ?? 😀 #shortvideo #lizzyisaeva
00:24
Lizzy Isaeva
Рет қаралды 63 МЛН
50 YouTubers Fight For $1,000,000
41:27
MrBeast
Рет қаралды 161 МЛН
That's how money comes into our family
00:14
Mamasoboliha
Рет қаралды 12 МЛН
ZUCHU ALIVYOMLIZA MANAGER WAKE KWA KUMPA GARI MPYA YA KIFAHARI/BMW
9:30
Aibu/Sababu za luludiva kumkana mume wake
15:19
Dizzim Online
Рет қаралды 36 М.
え、、、!
0:11
美好秋人
Рет қаралды 8 МЛН
Три с половиной в дюймах, ууу..😂
0:56
Жаз бітетін болдығой😂
0:33
NNN LIFE TV
Рет қаралды 6 МЛН