No video

ZABURI 31: NIMEKUKIMBILIA WEWE BWANA NISIAIBIKE MILELE Inspirational Bible Quotes by Frank Masembo

  Рет қаралды 4,545

MASEMBO GOSPEL LIBRARY

MASEMBO GOSPEL LIBRARY

Күн бұрын

ZABURI 31: NIMEKUKIMBILIA WEWE BWANA NISIAIBIKE MILELE Inspirational Bible Quotes by Frank Masembo
1 Nimekukimbilia Wewe, Bwana, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye,
2 Unitegee sikio lako, uniokoe hima. Uwe kwangu mwamba wa nguvu, Nyumba yenye maboma ya kuniokoa.
3 Ndiwe genge langu na ngome yangu; Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge.
4 Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri, Maana Wewe ndiwe ngome yangu.
5 Mikononi mwako naiweka roho yangu; Umenikomboa, Ee Bwana, Mungu wa kweli.
6 Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo; Bali mimi namtumaini Bwana.
7 Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako, Kwa kuwa umeyaona mateso yangu. Umeijua nafsi yangu taabuni,
8 Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha panapo nafasi.
9 Ee Bwana, unifadhili, maana ni katika dhiki, Jicho langu limenyauka kwa masumbufu, Naam, mwili wangu na nafsi yangu.
10 Maana maisha yangu yamekoma kwa huzuni, Na miaka yangu kwa kuugua. Nguvu zangu zinatetemeka kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imekauka.
11 Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Walioniona njiani walinikimbia.
12 Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa; Nimekuwa kama chombo kilichovunjika.
13 Maana nimesikia masingizio ya wengi; Hofu ziko pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walifanya hila wauondoe uhai wangu.
14 Lakini mimi nakutumaini Wewe, Bwana, Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.
15 Nyakati zangu zimo mikononi mwako; Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia.
16 Umwangaze mtumishi wako Kwa nuru ya uso wako; Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
17 Ee Bwana, nisiaibishwe, maana nimekuita; Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni.
18 Midomo ya uongo iwe na ububu, Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi, Kwa majivuno na dharau.
19 Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako Ulizowawekea wakuchao; Ulizowatendea wakukimbiliao Mbele ya wanadamu!
20 Utawasitiri na fitina za watu Katika sitara ya kuwapo kwako; Utawaficha katika hema Na mashindano ya ndimi.
21 Bwana ahimidiwe; kwa maana amenitendea Fadhili za ajabu katika mji wenye boma.
22 Nami nalisema kwa haraka yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya dua yangu Wakati nilipokulilia.
23 Mpendeni Bwana, Ninyi nyote mlio watauwa wake. Bwana huwahifadhi waaminifu, Humlipa atendaye kiburi malipo tele.
24 Iweni hodari, mpige moyo konde, Ninyi nyote mnaomngoja Bwana.

Пікірлер: 4
@floraan4388
@floraan4388 Жыл бұрын
Ooh yes yes lord
@masembogospellibrary
@masembogospellibrary Жыл бұрын
Aaamen
@zamdasalumu9740
@zamdasalumu9740 Жыл бұрын
We bwana usiniache ktk mateso yako maana we ndo msaada wangu was nguvu
@masembogospellibrary
@masembogospellibrary Жыл бұрын
Amen Amen
ZABURI 35 "Ee BWANA UTETE NAO WANAOTETA NAMI" (#Psalms35)
4:33
MASEMBO GOSPEL LIBRARY
Рет қаралды 4,2 М.
Kids' Guide to Fire Safety: Essential Lessons #shorts
00:34
Fabiosa Animated
Рет қаралды 12 МЛН
Yohana 11 "YESU AMFUFUA LAZARO" ▪️▪️ by Frank Masembo
8:07
MASEMBO GOSPEL LIBRARY
Рет қаралды 4,9 М.
KISA CHA KUSISIMUA CHA NABII YONA
45:10
Pastor Lazaro Samwel Kilala
Рет қаралды 4,8 М.
MPIGIENI MUNGU KELELE ZA SHANGWE (OFFICIAL VIDEO)
4:20
RAJO PRODUCTIONS
Рет қаралды 3,9 МЛН
Yona kumezwa na Samaki- (Book of Jonah 1-4)
2:40
Hadithi za Bibilia
Рет қаралды 7 М.
Psalm 118
5:11
Natron Studios
Рет қаралды 3,3 М.