1 Leo nina fikiria nchi nzuri Ninayotaka kuiona; Nisimamapo karibu na Mwokozi, Tajini zitakuwa nyota? Chorus Sijui tajini mwangu kama nyota Zitang`aa kila wakati! Nitakapoamka katika majumba Zitakuwa nyota Tajini? 2 Kwa nguvu za Bwana nitafanya kazi, Nitavuta roho za watu, Ili niwe na nyota katika taji, Bwana anapotupa tunu. 3 Nitakuwa na furaha nikimwona, Kuweka miguuni pake Watu walio vutwa kwa ajili ya Kazi yangu na Roho yake.