Рет қаралды 296
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi iko katika maboresho ya Sera ya Ardhi ili kuwa na sera itakayoleta suluhu kwenye changamoto za Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini.
Hayo yamebainishwa tarehe 2 Septemba 2023 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
Amesema maeneo yanayoenda kufanyiwa maboresho ni suala la umiliki ambapo kwa mujibu wa sheria ya sasa, mwananchi anaweza kumiliki ardhi hata kama hajaitumia au kuiendeleza.