No video

🔴

  Рет қаралды 63,007

Global TV  Online

Global TV Online

7 ай бұрын

🔴#BREAKING: MAPAPA wa DAWA za KULEVYA WAKAMATWA KIGAMBONI -WANATAFUTWA DUNIANI KOTE - "KILO 3,182"..
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Tanzania (DCEA) imekamata jumla ya kilogramu 3,182 za dawa za kulevya aina ya heroin na methamphetamine katika operesheni maalum iliyofanyika jijini Dar es Salaam na Iringa kati ya tarehe 5 hadi 23 mwezi Disemba, 2023. Watu saba wamekamatwa kuhusika na dawa hizo ambapo wawili kati yao wana asili ya Asia.
Kiasi hiki cha dawa za kulevya kinajumuisha kilogramu 2,180.29 za dawa aina ya methamphetamine na kilogramu 1001.71 aina ya heroin zilizokamatwa katika wilaya za Kigamboni, Ubungo na Kinondoni jijini Dar es Salaam pamoja na wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
Ukamataji huu umehusisha kiasi kikubwa cha dawa za kulevya ambacho hakijawahi kukamatwa katika historia ya Tanzania tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya. Hivyo, watuhumiwa waliokamatwa ni miongoni mwa mitandao mikubwa ya wauzaji wa dawa za kulevya inayofuatiliwa nchini na duniani.
Aidha, dawa hizi zilizozikamata zilikuwa zimefungashwa kwenye vifungashio vya bidhaa zenye chapa mbalimbali za kahawa na majani ya chai. Mbinu hii inatumika kwa lengo la kurahisisha usafirishaji wake na kukwepa kubainika.
Ukiacha dawa ya heroin inayotengenezwa kwa mchanganyiko wa kemikali kutoka kwenye mimea ya afyuni (opium popy) inayolimwa katika nchi za Asia na baadhi ya kutoka Amerika, dawa aina ya methamphetamine ni dawa mpya ya kulevya iliyopo katika kundi la vichangamshi sawa na cocaine.
Dawa hii huwa kwenye mfumo wa vidonge, unga au chembechembe mithili ya chumvi ang’avu yenye rangi mbalimbali ambayo huzalishwa kwenye maabara bubu kwa kuchanganya aina mbalimbali za kemikali bashirifu.
Dawa hii ni hatari kwa afya ya mtumiaji, madhara yake ni makubwa na hayatibiti kirahisi kwani mtumiaji hupata madhara ya kudumu kwenye ubongo na hivyo hupunguza uwezo wa kutunza kumbukumbu, kusababisha uraibu na kuathiri mfumo mzima wa fahamu.
Kiasi cha dawa za kulevya zilizokamatwa, endapo zingefanikiwa kuingia mtaani zingeweza kuathiri zaidi ya watu 76,368,000 kwa siku. Hivyo, ukamataji huu umeokoa nguvu kazi ambayo ingeangamia kutokana na madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi.
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa a Kulevya, inatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Mamlaka kwani mafanikio haya yametokana na ushirikiano unaotokana na wananchi wanaotoa taarifa juu ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na weledi na uzalendo mkubwa wa maafisa wa Mamlaka katika udhibiti wa biashara ya dawa za kulevya.
Pia, Mamlaka inatoa onyo kwa wote wanaoendelea kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya hapa nchini kuacha badala yake wajikite kwenye biashara nyingine halali kwani Mamlaka imejizatiti kukomesha biashara ya dawa za kulevya kwa kufanya operesheni katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha,Mamlaka inaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha Mamlaka katika kutekeleza kazi zake kwa ufanisi mkubwa.
Tukishirikiana, kwa umoja wetu tutaweza kuokoa vizazi vyetu na taifa letu dhidi ya tatizo la dawa za kulevya.
⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 739 750910), ( +255 783453136)
⚫️ Email: globaltvonlinenews@gmail.com
⚫️ OUR PLAYLISTS:
⚫️ MICHEZO na BURUDANI: • Habari zote za michezo...
⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: bit.ly/mikasa_y...
⚫️ GLOBAL RADIO TV: bit.ly/255globa...
⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: bit.ly/exclusiv...
⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: ndstream.net/gl...
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:apple.co/38HjiCx

Пікірлер: 190
@globaltv_online
@globaltv_online 7 ай бұрын
JIUNGE KWENYE CHANELI YETU YA WHATSAP ==> whatsapp.com/channel/0029Va7u...
@evodiusmwombeki9247
@evodiusmwombeki9247 7 ай бұрын
Mbona mnawaficha
@user-oc8jo9cj6e
@user-oc8jo9cj6e 7 ай бұрын
Kiukweli tumeelimika sana sio kudanganyana hivyo chamsingi tusapoti mama kz mkazi basi hayo mengine sanaa
@beatrice4780
@beatrice4780 7 ай бұрын
Majina?
@emmysarikiurio6445
@emmysarikiurio6445 7 ай бұрын
Yaani Mungu simama Hawa watu wanaharibu watoto wetu
@EliaoniTerry
@EliaoniTerry 7 ай бұрын
Hongera kamanda, ulinzi wa mungu pekee ndio msaada wako, mungu akulinde na team yako.
@user-xl1kj3om8g
@user-xl1kj3om8g 7 ай бұрын
Kazi yenu ni njema sana,Mungu aliyehai awabariki sana na atulinde watu wake zidi ya hawa wauaji.
@zenj1986
@zenj1986 7 ай бұрын
Mkuu unaweza kupewa taarifa lakini sasa watu wa chini ndio shida. Hao watu wako wa chini wanamaliza ishu chini kwa chini
@newhopeonline5818
@newhopeonline5818 7 ай бұрын
Hongereni kwa kazi njema,hao ndio wanatuharibia vijana wetu, hawastahili kuishi
@henrygodda3314
@henrygodda3314 7 ай бұрын
Mungu awakumbuke na uzao wenu;you're such a sacrifice na Hongera sana Mh. Rais wetu kwa dhamira ya dhati ya kusaidia wanyonge; be protected
@masoudrashidmohammed4124
@masoudrashidmohammed4124 7 ай бұрын
Tunamshukuru Allah kwa hili alilotujaalia kulikamata ila tunawaomba musiwaue tuwakamate ili tuanze na wao ili tufungue mnyororo hadi tuwakamate wote. Shukran zenu sana viongozi wetu
@user-xn1ly2yx7j
@user-xn1ly2yx7j 7 ай бұрын
Hongera sana serikali ya tanzania kwa ufanisi wa hali juu kwa kazi mliyoifanya .Maana hilo shehena kwa kweli tz ingekuwa kwenye hali mbaya kwa Raia wa tanzania. Ujumbe from Malawi.
@rahabnkya8276
@rahabnkya8276 7 ай бұрын
Daaaa! Kiasi kikubwa! Wafanyabiasha wakubwa wa madawa! HISTORIA kubwa toka ! Kahawa majani ya chai! Wazawa wako humo wazuri tu lkn hawasemi sababu ya hela, VIJANA wetu wameshakuwa bunju na mazezeta na hawataoa, hawana maisha marefu! Ee Mungu tuokoe na Misri hii. Mara hiki mara ushoga, wizi, ujambazi na vifo vinatishia Urefu wa maisha yetu. Tusaidie RAIS wetu mzuri sana!
@hamidudigogo5863
@hamidudigogo5863 7 ай бұрын
Waonyesheni hao watumiwa wengine watanzania watoto wa vigogo na vigogo wenyewe
@sabrinaibrahim1127
@sabrinaibrahim1127 7 ай бұрын
Hongereni sana Mungu ibariki nchi yetu na serikali uetu🙏🙏🙏
@abufirdaus4254
@abufirdaus4254 7 ай бұрын
Mola awabariki Kwa kazi yenu njema Madawa ya kulevya yanaharibu nguvu kazi ya nchi..
@ramadhanihudhaifani4376
@ramadhanihudhaifani4376 7 ай бұрын
Hii ni hatari sana kwa hakika! Haya madawa yameleta madhara makubww sana nchini mwetu na hata mataifa mengine. Wengi wanao jarib kutumia madawa hawa huwa ni vigumu sana kuchomoka huko! Mim nina ishauri nchi yetu iwe na hukumu nzito ambayo itakomesha na kutokomeza kabsa janga hili. Wanao kamatwa na biashara hii,WANYONGWE!!! Maana nia yao sio nzuri hata kidogo kwa Watanzania na Nchi kwa ujumla. Tuwe na sheria kama zile za China na nchi nyengine! KIFO TU. BASI!
@salehehemedi8267
@salehehemedi8267 7 ай бұрын
Safi sana kwa kazi nzuri
@mariamfaicalhassan2890
@mariamfaicalhassan2890 7 ай бұрын
Tunashukuru naomba kuuliza wale wenye tan 2 wa kilwa waliishia wapi ? Au hawa mkono wa mkubwa haukuwemo ?
@cleversalbaba-em4jf
@cleversalbaba-em4jf 7 ай бұрын
Daaaaah Mungu saidia kizazi chetu kinaangamizwa maisha yetu yapo hatarini mno.😢😢
@NilahIsmail
@NilahIsmail 7 ай бұрын
Mungu awabariki kwa kazi nzuri na kutunusuru wa Tanzania kwa balaa hii Alhamdulillah. Alhamdulillah.
@mashakhamiskh8880
@mashakhamiskh8880 7 ай бұрын
Daah hatariii, mungu anatupenda sana hichi kiwango kingeathiri watoto na wajukuu zetu
@vishalbsolanki
@vishalbsolanki 7 ай бұрын
Hongera sana kikundi cha kudhibiti dawa za kulevya… Mungu awapeni nguvu za kudhibiti, hizo dawa naa Mungu awabariki kwa kazi nzuri mlioifanya….
@barakamanga5502
@barakamanga5502 7 ай бұрын
Alooh hongereni sana maana kugundua kuwa miguko hii ime wekwa dawa ndani yake sirahisi, Mme tuokolea watotowetu
@omarymbaraj8072
@omarymbaraj8072 7 ай бұрын
Hongereni
@user-rp8vz2yt4j
@user-rp8vz2yt4j 7 ай бұрын
Soo nice.....nguvu kaz ya taifa inateketea kwa matumiz ya dawa za kulevya....mungu haklinde kamanda maana hawa jamaa wana mitandao mikubwa sana na yenye nguvu,,,kwao kujiondole vikwazo hata kwa kuondoa uhai ,,,,hawaoni tabu.... GETBLESSD!!!!
@francisboydmwakyusa230
@francisboydmwakyusa230 7 ай бұрын
Hongera sana Jembe, kazi nzuri. Watajua hawajui. Tunao kujua tunajua uwezo wako mkubwa ktk kutenda kazi. BIGUP brother.
@jonaspatrick2871
@jonaspatrick2871 7 ай бұрын
Kuna yule mkubwa mmoja na mtoto wake ambao ni maarufu sana kwenye haya mambo sidhani kama atakosa humu. Na, I'm sure this story will disappear on the wind as the rest of them ( Ghala la Wizi wa mafuta waziri kakaa kimya mpaka leo).
@lovenessmtei966
@lovenessmtei966 7 ай бұрын
Hongereni Sana kwa kuhakikisha biashara ya madawa ya kulevya Ina koma kabisa
@chachamakenge8367
@chachamakenge8367 7 ай бұрын
Kazi nzuri weledi, uwaminifu na uzarendo Mungu walinde watoto duniani
@festokiswaga9501
@festokiswaga9501 7 ай бұрын
Kazi nzuri sana Kamishna Lyimo! Hongera sana kwa uzalendo!
@IbrahimShan-qu3um
@IbrahimShan-qu3um 7 ай бұрын
Congratulations 👏
@angelanaftael7965
@angelanaftael7965 7 ай бұрын
Hakika wanataka kumaliza watoto wetu, wajue hata majumbani mwao hakutakuwa na amani
@mabondolawrence1812
@mabondolawrence1812 7 ай бұрын
Mnawahifadhi Kwa kuotaja majina Yao laiti mngewataja yumkini mngepata taarifa zaidi, Sasa majina Yao mnayasitiri wakati ushahidi mnao!
@ManaseNassary
@ManaseNassary 7 ай бұрын
Hongereni usalama wetu
@paulinbyonge8478
@paulinbyonge8478 7 ай бұрын
Mungu akubariki sana, pia chunguza sana Hawa tiba mbadala Kila kukicha wanaongezeka eti wanatibu pressure na kisukari
@hawaelymaricca7602
@hawaelymaricca7602 7 ай бұрын
Yaani wanazipitishaje jamani ,Binadamu Mungu turehemu
@bezalelmbijima8182
@bezalelmbijima8182 7 ай бұрын
Mungu awabariki sana sana maafisa wetu. Hayo watakuwa funzo kwa wengine. Mungu ibariki Tanzania na watoto wa Tanzania.
@hamishassan6784
@hamishassan6784 7 ай бұрын
Niwapongeze makamanda wangu kwa kazi nzuri sana , ila nahuzunishwa sana na mipaka yetu yaan shehena kama hio ilipitaje kwenye mipaka yetu.
@Kokafamil
@Kokafamil 7 ай бұрын
Mme wakatata karibu mwezi 1 mbona mnatuambia leo 😡 but Hongereni
@florencejohn6427
@florencejohn6427 7 ай бұрын
Hakuna kitu hapa. Hadithi na siasa tu.
@sr.elizabethmbuligwe5540
@sr.elizabethmbuligwe5540 7 ай бұрын
Ndio mlikuwa mnashabikia bandari yetu iendeshwe na wageni ndio mtajua tuombee nchi yetu
@Boniphaceshayo5
@Boniphaceshayo5 7 ай бұрын
Daah mungu atusaidie tu maana tutaliswa kila kitu
@user-wq6er3ux5r
@user-wq6er3ux5r 7 ай бұрын
Tumuombee sana mtani wetu kamishina lymo
@ritapiusnicolaus7068
@ritapiusnicolaus7068 7 ай бұрын
Hongereni sana kwa kazi nzuri 🙏🙏❤️
@mohamedkisenga6654
@mohamedkisenga6654 7 ай бұрын
Toka age magu ndo Leo nimeckia madawa yamekamatwa Yan watu wanaingiza sana mzigo sanaaaa
@habisnasalum-nz4zo
@habisnasalum-nz4zo 7 ай бұрын
Hata mkate watatoka tu angekua magufuri apo sawa uyo mama mafisadi wezi kawarudisha serikalini wapo kazini na anapandisha nauli na kila kitu Ili tufe ila zanzibari hafanyi hivyo mama wa hovyo hatumtaki kabisa
@abdulrahmansalim9773
@abdulrahmansalim9773 7 ай бұрын
Maneno mengi yote hayo yamepita WAPI WAPI VITU HIVYO VIMEPITA BAHARI CUSTOM IPO WAPI WACHENI UNAFIKI 😊😊😊😊😊😊😊😊😊😊😊😊😊😊😊😊😊
@charlesmwambinga4355
@charlesmwambinga4355 7 ай бұрын
Madawa haya ni Mengi Sana Sana aiseee....Jamani Tani 2😢😢😢😢😢
@MiriamAbdallah
@MiriamAbdallah 3 ай бұрын
Kuna yule jamaaa aliinyoshea kidole kigamboni wengi hawakumwelewa na kufikia kumtukana , lisemwalo lipo waja tuwe na akiba ya maneno,huruma jamii inaangamizwa na wenye nchi wachache kwa maslahi yao binafsi 😢😢😢😢😢
@kabaranamaganga6646
@kabaranamaganga6646 7 ай бұрын
Hongera sna Makamanda wetu, naomba hatua kali zichukuliwe dhidi ya wahusika ikiwezekana Kunyongwa.
@Kidotii
@Kidotii 7 ай бұрын
Hongeren sana , na Mungu awalinde!
@SuleimanKhdija
@SuleimanKhdija 7 ай бұрын
Wanao uza ni wengii saana na ukiona taarifa zinawafiki juwa majirani wamenyimwa maokoto ila niwengi mno
@ziddyziddy2524
@ziddyziddy2524 7 ай бұрын
Umeona hapo wamezulumiana
@mariamfaicalhassan2890
@mariamfaicalhassan2890 7 ай бұрын
Halafu wale wa Kirwa waliishia watu
@SuleimanKhdija
@SuleimanKhdija 7 ай бұрын
@@ziddyziddy2524 jirani yangu hapa anauza bangi ni Business kwakweli majirani wakikosa ugali Hua Wana mtishia anato pesa basi ila niwengi
@sullecom
@sullecom 7 ай бұрын
Nimesema ziteketezwe sasa iv zaweza ibiwa mkawekewa feki
@user-sp6sv3cg9d
@user-sp6sv3cg9d 7 ай бұрын
Mungu awe nanyi na awalinde awatie nguvu na Hao wahusika wasibaki salama wanatuharibia watoto wetu na wao kujidai matajiri kumbe ni wauwaji wakubwa
@ototek8037
@ototek8037 7 ай бұрын
Kesho utaambiwa wameachiwa, ushahidi ulifanana na madawa lakinini mkemka amethibitisha hayakuwa madawa. Hii ndo nchi yangu ninayoijuwa, kututangazia haisaidii wao kufanya magekechee ya maokoto, jawa jaa wanapesa na mtandao mpana..wataachiwa tu! Yupo wapi escoba?
@abdullayahya8717
@abdullayahya8717 7 ай бұрын
Tatizo lenu viongozi manatangaza kwenye vyombo vya habari na kututia hamasa ya utendaji kazi wenu ila ubaya hatuoni washitakiwa wakihukumiwa kisheria kesi nyingi zinamalizwa kinyemela. Hata hivyo hongera kwa kazi nzuri.
@vero57
@vero57 7 ай бұрын
Muchome kabisaaa hazaranii, wanatuumizia watoto wetu, kazi nzuri sana , HIII KALI
@emmanuelkanyela275
@emmanuelkanyela275 7 ай бұрын
hamna kitu hapo siasa tu kazi hyo aliiweza JPM
@mariamfaicalhassan2890
@mariamfaicalhassan2890 7 ай бұрын
Wale wa kimbunga job waliishia wapi ?
@subiramwaka9792
@subiramwaka9792 7 ай бұрын
Hongereni saana. kazi yenu ni njema
@mwanagwakyala3213
@mwanagwakyala3213 7 ай бұрын
Kumbe mnaweza kuwaleta popote walipokimbilia ! Basi hongereni kwa hlo
@mamboshepea8888
@mamboshepea8888 7 ай бұрын
Na tuwaone wakifungwa😢😢 si maneno tumechoshwa na maneno vijana wanaharibika kila uchwao
@jeremiajeremia6436
@jeremiajeremia6436 7 ай бұрын
Mungu ibariki Tanzania amen❤
@mashakhamiskh8880
@mashakhamiskh8880 7 ай бұрын
Ahsanteni jeshi la polisi, Allah atawalinda
@sulwajackson6906
@sulwajackson6906 7 ай бұрын
Jamani awa watu wanauwa vizazi vuetu,nashauli wanyongwe
@wamadoropushthestar4145
@wamadoropushthestar4145 7 ай бұрын
Tatizo Ni Kwamba Mnakamataga Halafu Hatuoni Mtiyateketeza Mwisho Wa Siku Mnagawa Na Mitaa Inaendelea Kupata Huduma Kama Kawaida. Nampaka Mmeyakamata Hivyo Inamaana Wahusika Wekuwa Wagumu Kutoa Kiasi Cha Pesa Mlichohitaji.. Mtu Mzima Ataelewa ila Asie Mtu Mzima Atawaita Mashujaa fc.
@sabihaibrahim143
@sabihaibrahim143 7 ай бұрын
mamaaaaaa sina la kuchangia hongereni mapapa dah
@minicooper9642
@minicooper9642 7 ай бұрын
Inaitwa chumvi hiyo ni noma sanaa South Africa ukikamatwa ni bonge la kesi kuliko unga, hii inatia watu mpaka uchizi
@kamdinindevu5185
@kamdinindevu5185 7 ай бұрын
Saf sana
@user-fl3yl4or3e
@user-fl3yl4or3e 7 ай бұрын
Hatari
@nassercurtis9579
@nassercurtis9579 7 ай бұрын
Tatizo ni moja tu wapo atu wanaaminì kabisa kwa vile Raisi wetu ni mwanamke wanamchukulìa poa sababu mama ni mstaarabu sana kwa watu wotè ila Magufuli ni ķatili kwà watu kama hawa hacheki nao na akijua epata msaada wa kukimbia wànabanwa paka hao wanaotumika kama njia., Kazi nzuri lakini Mungu awalindea na hao mapapa màna wapo wa gizani hao ndio wauwaĵ wakubwa.
@bennylove6021
@bennylove6021 7 ай бұрын
Wanapitisha bandarini kumbe na bandar ni ya kwao
@michaelndilima6210
@michaelndilima6210 7 ай бұрын
Kazi nzuri
@abdirazak1503
@abdirazak1503 7 ай бұрын
Hatariiii😂😂😂
@wardalardhy8669
@wardalardhy8669 7 ай бұрын
Custom ipo wapi ? Imepita Vipi ? Mpaka ikafika stage hiyo custom watu wa bandarini ndio hao wamo .
@danielmakelemo2395
@danielmakelemo2395 7 ай бұрын
Sasa utashangaa watu wakifikishwa mahakamani utasikia tarifa ya mkemia utakuta majibu sio dawa tena bari ni kahawa .maana hata wanaotunza kidhibiti wapo mtegoni kuchukua rushwa kubwa
@zephamandia3958
@zephamandia3958 7 ай бұрын
KAZI NZURI
@johnmwambete6117
@johnmwambete6117 7 ай бұрын
Hongera sana ila tujiulize ni kwa nini sasa madawa hayo yanaingizwa kwa kuwango kikubwa hivyo wapi tumekosea kuimarisha ulinzi
@user-lt1bi5nr1x
@user-lt1bi5nr1x 7 ай бұрын
Ndo maana wameyakamta
@user-fz5dg4ds5l
@user-fz5dg4ds5l 7 ай бұрын
Mmhh hatariiii sana 🙏😢
@peterdeus6093
@peterdeus6093 7 ай бұрын
Cui bono, just black and white we living in world where truth is caught between desires and needs MUNGU ibariki Tanzania 🇹🇿 MUNGU ibariki Africa 😭😭😭
@idrissaissa5607
@idrissaissa5607 7 ай бұрын
Mkuu wanyongwe Hao maana hawataki Amani yetu ya Tanzania🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
@DaudiHamisi-un2uu
@DaudiHamisi-un2uu 7 ай бұрын
Hawawezi hata kufungwa sio kunyongwa tuu biashara hii imekisiri mpaka kwenye nyumba za ibada
@constanciapeter2497
@constanciapeter2497 7 ай бұрын
Aiseee😮😮
@alfinmbilinyi5985
@alfinmbilinyi5985 7 ай бұрын
Yeah big up!
@shabbirbharmal7876
@shabbirbharmal7876 7 ай бұрын
Tunaomba raisi wetu havo watu walio kamatwa wa nyongwe hadharani ili.wajue.sisi TANZANIA TUKO MAKINI NA HIYO
@mariamfaicalhassan2890
@mariamfaicalhassan2890 7 ай бұрын
Nani Samia?
@bahatichombo7209
@bahatichombo7209 7 ай бұрын
Safi kabisa
@yahyahamisi2038
@yahyahamisi2038 7 ай бұрын
Vyombo vya ulinzi na Usalama 👍👍👍👍👍 huu ni mtandao mmoja lkn Angalieni pia Ugaidi 🙏🙏 upo hapa TZ chunguzeni comments za mapoyoyo Wa kiimani 🙏🙏 those guys are potential terrorists here as it was the case with Ahamed Ghailan from Pemba who supported Osama bin Laden in his reigns of terror. Jitafakarini 🙏 jukumu la ulinzi na Usalama ndo UTI wa ngongo wa TAIFA ketu. 🙏🙏
@eshamohamed9833
@eshamohamed9833 7 ай бұрын
Subhanaallah
@GSizetz-if7ri
@GSizetz-if7ri 7 ай бұрын
Hao watu waliokamatwa na hayo Madawa wapewe kwan watumie .kufungwa pekee haitoxh
@batulmohammedkanji544
@batulmohammedkanji544 7 ай бұрын
Hongera sana pls edeliani hatutaki matatizo.
@mabondolawrence1812
@mabondolawrence1812 7 ай бұрын
Mateja wengi sana sana kwenye vituo vya mabasi.
@amriyyahamad3946
@amriyyahamad3946 7 ай бұрын
Tayari wamemalizwa na walio waamini wanyongwe tu
@user-wi3ml4lg5b
@user-wi3ml4lg5b 7 ай бұрын
Nyonga wote Hao. Msituambie wamepewa dhamana
@jayjay4313
@jayjay4313 7 ай бұрын
Wa Assia sio watu wakawaida na hiyo ndio sifa yao duniani kote. Si tumewakarib sha wenyewe! Hilo kwao kama trailer tu, lazima kuna mengi hatuyajui.
@barakakhemedi1250
@barakakhemedi1250 7 ай бұрын
Ingependeza mkawaonyesha hapa na wantongwe tu
@AmosKitunka-xx7cs
@AmosKitunka-xx7cs 7 ай бұрын
Tupambanieni kwa maana mukizubaa nguvu kaz inakufa na wanaweza kutumia njia ambazo si nzuri...Madawa ya maabara cyo mazuri yanatuchanganya ubongo na akili tunashindwa kutimiza malengo.
@kakaemanuelelias6963
@kakaemanuelelias6963 7 ай бұрын
Kamateni na hao wanao tengeneza hivyo vifungashio vya kahawa
@gazzomaster9462
@gazzomaster9462 7 ай бұрын
Wanyongwe
@yussufmohammed9299
@yussufmohammed9299 7 ай бұрын
Zitiweee Moto wananchi n cye tuone😂
@sabihaibrahim143
@sabihaibrahim143 7 ай бұрын
utayasikia tu huyaoni hayo
@batulmohammedkanji544
@batulmohammedkanji544 7 ай бұрын
To be hang no samhane wa uliwe pls
@snetiengineeringltd8246
@snetiengineeringltd8246 7 ай бұрын
Wamechomana hawa
@user-jm7qj6kx8c
@user-jm7qj6kx8c 7 ай бұрын
Kwnn serikali isiunde sheria ya kuuwawa kwa yeyote anaejihusisha na hii biashara
@kenzomgeni7699
@kenzomgeni7699 7 ай бұрын
Nzuri
@demicratia4071
@demicratia4071 7 ай бұрын
😢😢😢jamani jamani ndio maana Arusha inaurushwa rushwa
@bakarimpame3824
@bakarimpame3824 7 ай бұрын
Swali langu baada ya hukumu kutolewa na wahusika kupata adhabu hizo dawa zinapelekwa wapi??
Mohammad bin Salman: Prince With Two Faces
54:00
Show Me the World
Рет қаралды 2,8 МЛН
WORLD'S SHORTEST WOMAN
00:58
Stokes Twins
Рет қаралды 172 МЛН
SPILLED CHOCKY MILK PRANK ON BROTHER 😂 #shorts
00:12
Savage Vlogs
Рет қаралды 42 МЛН
POLISI DSM YAWANASA WAUZAJI WA DAWA ZA KULEVYA DSM
9:55
Millard Ayo
Рет қаралды 125 М.
BSS 2023 SN 14   EPISODE 05 DAR PART 1
1:10:24
BongoStarSearch
Рет қаралды 64 М.
WORLD'S SHORTEST WOMAN
00:58
Stokes Twins
Рет қаралды 172 МЛН