Dizasta Vina - Hatia IV

  Рет қаралды 166,465

Dizasta Vina

Dizasta Vina

Күн бұрын

Пікірлер: 654
@joshmangi
@joshmangi 3 жыл бұрын
"Nilimfanya ndoto, kumbe naye ana ndoto nyingine"
@gerrymainmunisi6677
@gerrymainmunisi6677 2 ай бұрын
Nani anasikiliza hiki chuma August 12, 2024... Dizasta mtu mbaya sana
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
“JASIRI JOHN….. ALIYAANGALIA MAISHA YAKE HAKUONA JINSI ANGEWEZA KUISHI BILA JANE MSICHANA ANAYEMPENDA LICHA YA KUZONGWA NA UMASIKINI ALIJITAHIDI KUMPA JANE MAHITAJI MADOGOMADOGO KADRI ALIVYOWEZA LAKINI ALIFAHAMU SHUBIRI YA KUSUBIRI KUPENDWA HUKU ANAFAHAMU KUSUBIRI KUPENDWA NI MATUMAINI YANAYOUMIZA. KAMA WANAVYOSEMA, MTAFUTAJI HACHOKI AKICHOKA KASHAPATA… .ALIENDELEA KUNGOJA” Ah! Sikuwa na zali sikuziamini ndumba Sikuwa na mali za kufuja Nilijitahidi kuuza mitumba kufuga mipunga Ili siku nimpe gari nimpe nyumba. Nilishindwa… Niliishia kumpa chai, ‘chipsi’ mayai na ‘vocha’ Nywele za kimasai na mkoba Pesa za magauni, majuba na viatu vya kuzuga Nilimpa muda ila bado haikutosha, kwani… Nilipomwambia nampenda hakujibu Akaweka moyo wangu maumivu Na mtima wangu akauweka ‘solemba’ Nikaapia kuwa sitakuja kupenda ‘forever’ Ah! Nilimpa upendo nilimpa sifa Niliweka mitego ya faida, haikuwa shwari Nikabadili mwenendo wa maisha Niliweka malengo sikutimiza, hakunikubali Alikuwa na ndoto kubwa kushinda mimi Alikuwa na misimamo kuipita dini Aliniambia ameomba nije kuokota utajiri Amengoja sana na sasa amechoka kusubiri “JOHN ALIFAHAMU HALI YA JANE, KUWA JANE ALIZALIWA KWENYE FAMILIA MASIKINI, NA ALIUCHUKIA MNO UMASIKINI. ALIFAHAMU UMASIKINI ULIVYOCHUKUA UHAI WA MAMA YAKE KIPENZI, ALIYEFARIKI KWA KUKOSA MATIBABU. ALIIFAHAMAU NADHIRI ALIYOIWEKA JANE YA KWAMBA HATOKUBALI TENA KUISHI KWENYE MAISHA YA KIMASIKINI, NADHIRI ILIYO MWEKA JOHN NJIAPANDA” Ah! Sikuwa na hali ya kuikosha roho yake Nilimwacha aende aufate moyo wake Alipata bwana wa kizungu magharibi Alimwahidi kuishi maisha ya ndoto zake Nilipata uchungu niliishia kuhamaki nilitaka nijiue Nilitaka nimzuie abaki nikakumbuka Ukipenda ua haulikati unaliacha likue Duka langu nilifunga biashara niliacha zote Uchumi uliyumba kwa maana nilianza pombe Niliumwa bado kidogo moyo uzime Nilimfanya ndoto kumbe naye ana ndoto nyingine Alisema anakwenda jiji la Miami Hakuna alichowaza zaidi ya kuishi kifahari Kamtumia picha na ‘mchizi’ kazikubali Na yupo tayari kumlipia gharama za safari Aliondoka na kipande kimoja cha mwili Nilikonda nilipata ugonjwa wa akili Haikuwahi kupita hata sekunde nisilie Nilitamani mpaka ardhi ipasuke niingie “JANE ALIPOONDOKA ALIMWACHIA JOHN KIDONDA KILICHOCHELEWA SANA KUPONA NA YEYE AKAWEKA NADHIRI YA KUTOJIHUSISHA NA MAPENZI TENA MAISHANI MWAKE. ALIKAA KWA MUDA MREFU BILA MAHUSIANO. LAKINI… HAKUNA DAKTARI MZURI KAMA MUDA, JOHN ALIPONA MAUMIVU NA ALIIRUDIA HALI YAKE YA KAWAIDA” Ah! Muda ukaenda nitapata ‘Mwanamwali’ Nikamwomba awe mwenza wa maisha akakubali Nikamvisha pete nikalipia mahari Sikumpenda lakini nilijifunza kumjali Aliuliza kama nampenda, nilimjibu Sikutaka kuweka moyo wake maumivu Sikutaka kuuweka Mtima wake solemba Kiasi aseme hatakuja kupenda ‘‘forever’’ Ah alinikumbatia nikamfunga kwa ishara Akanikabidhi tunda nikala Akaniamini tukajuana nikapanga kumwoa Akaidhisha na tukaanza na mipango ya ndoa “WAKATI KARNE YA 21 INAINGIA, JOHN ALIKUWA NI MIONGONI MWA VIJANA WALIOKUWA ‘FASCINATED’ NA UKUAJI WA TEKNOLOJIA YA MITANDAO YA KIJAMII. ALIJIUNGA NA DUNIA HII MPYA, MARA KADHAA ALIKAA KWENYE UBARAZA, AKIANGAZA SIMU YAKE. AKIPAPASA KILA KITUFE, NDIPO SIKU MOJA AKAPATA UJUMBE KUTOKA KWA JANE” “Habari naamini u bukheri wa afya Unaendeleaje maisha na huyo mpenzi wa sasa .nashukuru nahema ughaibuni si kwema Nakiona cha mtema mpaka naona ni heri nikafa… Ah! Maisha niliyowaza yote ni uongo Nauzishwa madawa nalazimishwa ngono Nafungiwa ndani kama mtumwa ufungwani Roho yangu rehani kiasi sasa naitamani Bongo Ukubwa umekuja kunisafisha jicho Ndoto imeisha na taswira imenionyesha sivyo, ah Naomba unifate uniondoshe kwenye hichi kifo Na hii namba ya msamaria atakueleza nilipo” Sherehe ilikuwa na mipango madhubuti Kabla mimi kuichukua michango ya Harusi Nikatoroka ughaibuni kufuata hisia zangu Kwenda kumfata njiwa wangu mahususi Nilivuka majangwa na majabali Sehemu ya safari anga sehemu nyingine bahari Niliacha kila kitu nyuma upendo na huruma vilinijaa Penzi likanipeleka mbali “JOHN ALIFIKA UGHAIBUNI, AKAMTAFUTA MSAMARIA ALIYETAMBULISHWA NA UJUMBE, MSAMARIA AKAMWELEKEZA NJIWA WAKE ALIPO, NA NIKWELI… HAPAKUWA PEMA” Nikakutana na bopa la kizungu Lenye sura ya kuichachisha mboga kwenye chungu Kiko kwenye mdomo,Tatuu kila kona na wapambe Pamoja na vishoka wenye mtutu Sio siri alizungukwa na wasichana wengi Sikujua umri walikuwa wadogo ka’ “madent” Baadhi walikuwa uchi wanahesabia “chenchi” Wengine masaji huku wengine wanamchezea nyeti “MASIKINI JOHN, ALIDANGANYA KWA KUJITAMBULISHA KAMA KAKA KWA JANE, AKIMSIHI YULE MAFIA AMRUHUSU AONDOKE NA JANE WAKAANZE MAISHA MAPYA, LAKINI… PALIPOSHINDWA SHOKA WEMBE HAUWEZI TAMBA. KWA KUZIDIWA NA UOGA WA KUUAWA… JANE ALIMKANA JOHN KWA KUSEMA HAMJUI…” Hata nilipomuuliza kama ananipenda hakujibu Akaweka moyo wangu maumivu Nilijua hawezi kufa kwa sababu hakunipenda Na ni rasmi nikapoteza shilingi kwenye msitu Nilikiambia kifo kama unakuja njoo Maana sikuwa mtu ilishakufa roho Sikuumia kama alivyoniumiza yeye Kwahiyo sikujali jinsi nilivyoteswa na wale mbwa no Aliambiwa ambusu bosi hakubisha Alipewa bunduki hakusita Aliishika risasi akaiingiza Akaambiwa anipige kwenye kichwa JOHN ALIKUWA NI JINA JIPYA LA WAHANGA WA UPENDO WA DHATI, VIPOFU WA MAPENZI, WAJINGA WA MAHABA... JOHN ALIKUWA ROMEO KWENYE ROMEO AND JULIETH, ALIKUWA SAMSON KWA DELILAH KWENYE WAHUKUMU WA AGANO LA KALE, ALIKUWA JACK KWENYE TITANIC, FRED WEASLEY KWENYE HARRY POTTER.. JOHN ALITUKUMBUSHA KUWA UPENDO NI SADAKA, SADAKA YA MUDA NA PESA, ALITUKUMBUSHA UPENDO NI SADAKA YA DAMU JOHN, ALIPOTEZA UHAI AKIWA KWENYE SAFARI YA KUTAFUTA UPENDO WA MTU ALIYEMHUSUDU NA JANE ALIPOTEZA AMANI NA THAMANI YAKE KAMA MTU AKIWA KWENYE SAFARI YA KUTAFUTA UTAJIRI ALIOUHUSUDU Hatia iko wapi?
@challymchaff374
@challymchaff374 3 жыл бұрын
Daaah dizasta wewe ni vina hivi naanzaje kuchoka kusikiliza nyimbo zako
@wilsontonga3728
@wilsontonga3728 3 жыл бұрын
🤝🏾
@dullywamashairi121
@dullywamashairi121 3 жыл бұрын
Naskiza ngoma mpaka moyo unataka kupasuka. Dizasta vina, MC Mahiri, Mc Katiri. Yaan hauishi kbs katika dunia tunayoishi sisi! Huku kwetu kitaa kizima wanajua n kiasi gani Mwamba unawika, wameacha kuniita jina langu, sikuhizi wananiita Dizasta Vina. Ngoma zako ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri na hana hatia. Ngoma zako zinaweza kumfanya mtu akatishe ktk msitu mnene wenye kutisha na asiogope. Ngoma zako zinamfanya mtu ajifunze kuwa mwenye maamuzi magumu bila kuhofia lawama la mwenye kulaumu! Dizasta vina, katika ulimwengu wa Hip Hop zaidi yako wewe bado sijamuona mwingine. Hata Fareed Qubanda umemtupa kule, kabakia jina tu! Hebu pitia hii ili uone uzao wa tungo zako broo kzbin.info/www/bejne/laeqpmeiZrKig9k
@castorymwaipopo290
@castorymwaipopo290 3 жыл бұрын
Nakukubali sana bro 💪
@sautidawa2222
@sautidawa2222 3 жыл бұрын
Real talent
@emilysaimon481
@emilysaimon481 3 жыл бұрын
Dizasta vina bro we ni mkaliii Sikumpenda lakini nilijifunza kumjali Kama tupo pamoja tia like 25-12-2020
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Thanks.. Please share. Usisahau kuorder my new album
@emilysaimon481
@emilysaimon481 3 жыл бұрын
@@dizastavina pamoja bro nigei no yako
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
@@emilysaimon481 pre order kupitia tigo pesa 0655696811 au Mpesa 0762158871
@msolidwagalilaya6094
@msolidwagalilaya6094 6 ай бұрын
Brother ushaandika HATIA nyingi sana lakini hii hatia IV ni funga kazi brother
@shabannyamsalika
@shabannyamsalika 3 жыл бұрын
Hii ngoma ni zaidi ya albamu nzima ya Weusi, Prof Tungo we ni 🔥🔥🔥🔥🔥
@dullywamashairi121
@dullywamashairi121 3 жыл бұрын
Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha kzbin.info/www/bejne/laeqpmeiZrKig9k
@shabannyamsalika
@shabannyamsalika 3 жыл бұрын
@@dullywamashairi121 Hip hop inahitaj wenye uwezo mkubwa wa kufkr, pole sana kwako mwny uwezo mdogo nkushauri kasikilize waaah!!!
@dullywamashairi121
@dullywamashairi121 3 жыл бұрын
@@shabannyamsalika inaelekea wewe ndo hujanielewa Mimi. Wewe bado mbana pua. Wagumu wakipita wataelewa nimemaanisha nini. Umekurupuka mzee, maana kitaani wamenibatiza jina wananiita Dizasta vina!!💪💪💪
@shabannyamsalika
@shabannyamsalika 3 жыл бұрын
@@dullywamashairi121 We ndo umekurupuka kusema huu wimbo ni wawagumu, hii ngoma anasikiliza mtu yeyote na anaelewa. Tuondoe mawazo finyu ya kudhania kuwa hip hop inasikilizwa na watu wagumu, cjui makatiri km wewe ulivyosema mwanzo...
@obeidjoseph3610
@obeidjoseph3610 3 жыл бұрын
@@dullywamashairi121 mwanangu ww bado Sana na hilo jina la dizasta mwalichafua kitaan kwenu
@camillomakongwa8308
@camillomakongwa8308 3 жыл бұрын
This dude is a script writer, story teller inshort ni Verteller,,, he can compose a movies of 2 hrs in 7 mins,, daaaamn🔥🔥🔥🔥
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Thanks, please share
@dullywamashairi121
@dullywamashairi121 3 жыл бұрын
Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha kzbin.info/www/bejne/laeqpmeiZrKig9k
@mussabutanwa8693
@mussabutanwa8693 3 жыл бұрын
@@dullywamashairi121 yes he's a genius we should support him lol!!!
@dullywamashairi121
@dullywamashairi121 3 жыл бұрын
@@mussabutanwa8693 dats true my blood Dizasta vina: The man one army 💪💪
@mussabutanwa8693
@mussabutanwa8693 3 жыл бұрын
@@dullywamashairi121 yes for really man
@wawesttv
@wawesttv 9 ай бұрын
... nilipo mwambia nampenda hakujibu... 2024
@maishacenter-eastafricatv3976
@maishacenter-eastafricatv3976 3 жыл бұрын
Duuhh nlichelewa😪😪😪 Dizzasta's fan number one from +257🇧🇮🇧🇮🇧🇮
@ashuramuhammed3257
@ashuramuhammed3257 Жыл бұрын
Dizasta hii nyimbo ni funzo tosha yani ww ndo mwalimu wangu najifunza vitu vingi nkasikiliza nyimbo zako$
@winfredykahwili1513
@winfredykahwili1513 3 жыл бұрын
Huu mziki wako ni dawa ya ubongo asee Viva dizasta vina 💪💪💪👊👊💥💥💥
@louiskhan7372
@louiskhan7372 3 жыл бұрын
Hii True story nimesikiza ×10....song imenipeleka mpaka gaibuni ....utahisi mkono wa mungu umeandika Hii✔✔#KingOfRap
@tiktoktv8678
@tiktoktv8678 3 жыл бұрын
Wasanii kama hawa Bongo ni wachache Sana... Big up bro....
@yusuphmyinga
@yusuphmyinga 28 күн бұрын
2024 Tunard kula madin kwa mwamba Ngoma hazichoshi vina Zawad yetu wapenda hip hop🙏
@kelvinshayo608
@kelvinshayo608 3 жыл бұрын
Nilikwambia unajua na ctoacha kukwambia unajua💪💪
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Thanks kev
@ARUSHA_NAILS
@ARUSHA_NAILS 3 жыл бұрын
Dah dizasta umezigusa hisia umenifanya nijione mwenye hatia
@erastompongo8400
@erastompongo8400 3 жыл бұрын
Dah Kama umeniimba mimi vile Haso za mapenzi duniani zinaumiza wengi
@jamesngadaya2791
@jamesngadaya2791 3 жыл бұрын
dizasta unao uwezo mkubwa sana wenye nguvu kama meli ya mizigo aiseee
@legawayz6093
@legawayz6093 3 жыл бұрын
Hii ni movie kabisa bro one day andaa scripts then simama as diirector naamini itakuwa kazi kubwa BIG UP DIZASTA VINA
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Hopefully one day
@BabaNasritz
@BabaNasritz Жыл бұрын
naikubali kinoma hingoma bigp bro
@aloycemaembe8116
@aloycemaembe8116 3 жыл бұрын
Nmekubar bro salut kwa hii kaz
@nassoroally6093
@nassoroally6093 3 жыл бұрын
Bro kuna haja sanaa yako ifike ktk jamii na ipigwe promo.. Kuna ujumbe madhubuti
@jeovangisc7957
@jeovangisc7957 3 жыл бұрын
Daaaa bro unajua mpaka unaboa.. masikio yetu hayalali njaa kila unaposhika kipaza!!
@benyvoice9415
@benyvoice9415 3 жыл бұрын
Kaka hii ngoma naomba niifanyie cover yn nmeikubal Kias kwmb mpk nawaboa watu Everyday nackiliza
@michaelmasanja6343
@michaelmasanja6343 3 жыл бұрын
Verteller ...Dah huwezi amini nimeiona movie yote kichwani mwangu the way Mwamba unavoflow... nilichofeli ni kuipata sura ya Jane.
@alextanzania
@alextanzania 3 жыл бұрын
Dizasta vina ni akina Joh 70. Mtiririko mzuri ,kazi nzuri. Big up brother.
@raymondtsumah6410
@raymondtsumah6410 7 ай бұрын
Ogopa mwanamke💔
@ibuibu5247
@ibuibu5247 3 жыл бұрын
jamaa lnajua sanaaa .....
@peterbenjaminpeterbenjamin9566
@peterbenjaminpeterbenjamin9566 3 жыл бұрын
Aisee dizastar noma Sana mshkaji wangu darasa Hilo namimi napenda Nije nipate mautundu ya asali ya hip-hop
@salehekasangas3291
@salehekasangas3291 Жыл бұрын
Umeshushwa.brooo...yan.unajuaa.brooo
@bonnifacewilly3026
@bonnifacewilly3026 3 жыл бұрын
Daaah huyu jamaa anafanya mziki kwa bongo hakuna tena kama dizasta amani kwako brother
@aaronjohn9518
@aaronjohn9518 3 жыл бұрын
Deep sana hii ni kama movie
@mwajumakarim8520
@mwajumakarim8520 3 жыл бұрын
Wewe wewe weeeeeewe🥺🥺🥺ulishushwa ututeke🇹🇿❤️
@dullywamashairi121
@dullywamashairi121 3 жыл бұрын
Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha kzbin.info/www/bejne/laeqpmeiZrKig9k
@rachelgmartin6850
@rachelgmartin6850 3 жыл бұрын
Sauti yako tu mi hoiiiii🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🌹🥰❤️
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Thank you........
@learntoearn9588
@learntoearn9588 3 жыл бұрын
Muda utafika Inshaallah dizasta utakua jina kubwa na ramani ya maarifa kwa kizazi kijacho
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Hopefully
@emmabelljohn4086
@emmabelljohn4086 3 жыл бұрын
Nomaa sanaa
@hollymore4904
@hollymore4904 3 жыл бұрын
We jamaa. Kuna tamaduni music na Kuna dizasta music... Hakika. Hii sio tamaduni,hii dizasta
@danchalzndyanabo9200
@danchalzndyanabo9200 3 жыл бұрын
Dizasta vina noma sana
@obeidjoseph3610
@obeidjoseph3610 3 жыл бұрын
Unatishaaa yaaaani hiii ngoma mengne live
@sabrisaleh1720
@sabrisaleh1720 3 жыл бұрын
We dizasta fundi ni kweli nikitaka mziki mzuri nimtafute dizasta
@danielmalimi9890
@danielmalimi9890 3 жыл бұрын
Duuuhhh.... hii inabeba sababu muhimu ya muziki kwenye maisha....
@revocatuscharles1512
@revocatuscharles1512 Жыл бұрын
Jamaa unaimba sana aiseh🔥🔥🔥🔥
@chibalevicent822
@chibalevicent822 Жыл бұрын
You are so Genius, asante kwa uwezo wako wa kunifanya niamini kuwa wewe ndie Rapper Bora
@claudekeverenge4404
@claudekeverenge4404 3 жыл бұрын
Oyaah Vina wewe sio wa sayari hii hii umeuwaa.. Hii ndio hip hop
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Thanks bro
@kibafteshadau222
@kibafteshadau222 Жыл бұрын
Yule dogo raptcha akae mbali....ajifunze kuchana, sio fujo nyingi ....dizasta ni disaster balaa🔥
@furahinandrew9704
@furahinandrew9704 3 жыл бұрын
We jamaa nomaa
@boygavana4674
@boygavana4674 3 жыл бұрын
Dizasta ww sio binadamu wa kawaida aseee haijawahi tokea
@deviceboykifaa5985
@deviceboykifaa5985 3 жыл бұрын
nakubali yan huja wahi ikosea nafis yangu kak
@brainfigure94
@brainfigure94 3 жыл бұрын
Dizasta vina saiv umesha convert akili yangu kwenye hiphop naenjoy sana napo usikia mziki wako nakuwa makini ili nielew unachokimaanisha nanukuu kwenye hatia 2 ulisema wanaume wote mbwa ila cjui sasa wewe ni kubwa la ma mbwa mana sioni wa kucompare na mziki unaoimba
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Shukrani sana ndugu, please share na marafiki
@Tobey1988ful
@Tobey1988ful 3 жыл бұрын
New fan from +254 hapa.... Huyu kaka balaa sanaa dah
@dullyhaleem6962
@dullyhaleem6962 2 жыл бұрын
Hii nyimbo itungiwe movie kummmke duuh😓😓🔥🔥🔥
@johnkerrysibomana9062
@johnkerrysibomana9062 2 жыл бұрын
Nimerudi hapa baada ya mistari mingi kunigusa na kuendana na ninachikipitia kwenye maisha ya mahusiano
@oscarsospeter8034
@oscarsospeter8034 2 жыл бұрын
Wewe ni mtunzi Huru Dizasta vina God Abless njia zako
@hassanihanzel
@hassanihanzel 3 жыл бұрын
Wa KUMI kutazama 🙌
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
👏🏾 👏🏾 👏🏾 👏🏾
@KelvinEmersonSteven
@KelvinEmersonSteven 3 жыл бұрын
Aisee hii ni ya moto kushinda jua🔥🔥🔥🔥
@dullywamashairi121
@dullywamashairi121 3 жыл бұрын
Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha kzbin.info/www/bejne/laeqpmeiZrKig9k
@rashidynnungu6775
@rashidynnungu6775 3 жыл бұрын
we jamaa unajua shikamoo sana
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Marahaba 😎 😎 😎
@sayeedally8152
@sayeedally8152 3 жыл бұрын
kazi nzuri bro,,,, nakubali kazi zakoo
@meshack2559
@meshack2559 3 жыл бұрын
Mistar unachora Broo!!! Ni nomah ,we mkali aise,big up
@binyezanch8271
@binyezanch8271 3 жыл бұрын
Wimbo wangu wa mwaka kbsa Asante dizasta 2020
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Apreciate, umeshaweka order ya album
@awetubello5399
@awetubello5399 3 жыл бұрын
Brother unawezaaaaah na xo unaweza 2 we ni MWALIMU
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Thanks bro
@novatusanthony8563
@novatusanthony8563 3 жыл бұрын
Hii goma inatakiwa wasambaziwe wanafunzi Tanzania mzima maana hili ni somo linajitegemea.
@valentinesyekeye6846
@valentinesyekeye6846 Жыл бұрын
Upewe maua yako mzee. Hizi ni zaidi ya tungo
@saimonkimolo5313
@saimonkimolo5313 6 ай бұрын
Dah broda kila siku nasikilza hii ngoma tangu itoke nimwaka watatu huu story flan ilionitokea kabsa lakn si mbele hapahapa bongo
@directorluganongonya7212
@directorluganongonya7212 3 жыл бұрын
Daaah ! Shikamoo tena
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
🙏🏼🙏🏼
@kelvinmzopola5186
@kelvinmzopola5186 3 жыл бұрын
Daaaaah so sad 😌 ila we jamaa unajua kinoma
@saidamour2635
@saidamour2635 3 жыл бұрын
Disasta unaweza sana amini wanakuelewa ila wanabana tu, fans wako tunasubri collabo yako na kaa la moto.
@jumangala
@jumangala Жыл бұрын
Ausio
@nelsonkedmon8534
@nelsonkedmon8534 3 жыл бұрын
Nakubali sana hujawahi kosea the vertller
@dullywamashairi121
@dullywamashairi121 3 жыл бұрын
Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha💪💪 kzbin.info/www/bejne/laeqpmeiZrKig9k
@erickpaschaljr8667
@erickpaschaljr8667 3 жыл бұрын
Ahsante sana Dizasta Vina Kwa Muziki Mzuri unaoacha/utakaoacha Alama ya Milele
@fundi_nyata
@fundi_nyata 3 жыл бұрын
THE VERTELLER!! Wachache watakuelewa na kukusifia!!
@gideonaire_ke
@gideonaire_ke 3 жыл бұрын
kazi safi sana Dizasta
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Sijaona order yako brother?
@gideonaire_ke
@gideonaire_ke 3 жыл бұрын
@@dizastavina order ya nini bro?
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
@@gideonaire_ke the Verteller ALBUM.. Coming up this Sunday
@kangeyg6879
@kangeyg6879 3 жыл бұрын
Master vina fan toka 🇰🇪🔥✅ tumengoja sana umewakilisha kama kawaida
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Thanks, please share
@mosesbond202
@mosesbond202 3 жыл бұрын
Wewe mwamba ni mwehu sema tuu unafikiri sana Yaani movie moja classic
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
😂 😂 😂
@johnmosha8285
@johnmosha8285 3 жыл бұрын
Makini sana mzee
@jofreymfugale4752
@jofreymfugale4752 3 жыл бұрын
Aliondoka na kiungo cha mwili 😃🔥🔥
@IddyKatyawa
@IddyKatyawa 2 ай бұрын
Umetisha
@richardtitus8539
@richardtitus8539 3 жыл бұрын
Daaah black maradona.. home boy unajua
@mwajumakarim8520
@mwajumakarim8520 3 жыл бұрын
Nakuona mbali
@dullywamashairi121
@dullywamashairi121 3 жыл бұрын
Naskiza ngoma mpaka moyo unataka kupasuka. Dizasta vina, MC Mahiri, Mc Katiri. Yaan hauishi kbs katika dunia tunayoishi sisi! Huku kwetu kitaa kizima wanajua n kiasi gani Mwamba unawika, wameacha kuniita jina langu, sikuhizi wananiita Dizasta Vina. Ngoma zako ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri na hana hatia. Ngoma zako zinaweza kumfanya mtu akatishe ktk msitu mnene wenye kutisha na asiogope. Ngoma zako zinamfanya mtu ajifunze kuwa mwenye maamuzi magumu bila kuhofia lawama la mwenye kulaumu! Dizasta vina, katika ulimwengu wa Hip Hop zaidi yako wewe bado sijamuona mwingine. Hata Fareed Qubanda umemtupa kule, kabakia jina tu! Hebu pitia hii ili uone uzao wa tungo zako broo kzbin.info/www/bejne/laeqpmeiZrKig9k
@RamaSwalehe-kc9kr
@RamaSwalehe-kc9kr Жыл бұрын
Unyama sana broo
@tinnohaugustineh6193
@tinnohaugustineh6193 9 ай бұрын
Vina vingi sana humu👑
@octavianmushi928
@octavianmushi928 3 жыл бұрын
Brazaaa umegusa maisha ye2 kwa hii ngoma
@nashonshimba7997
@nashonshimba7997 3 жыл бұрын
Imenitoa machoz hii ngoma mapenz yanauma sana
@dullywamashairi121
@dullywamashairi121 3 жыл бұрын
Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha kzbin.info/www/bejne/laeqpmeiZrKig9k
@ramadhanally138
@ramadhanally138 3 жыл бұрын
My broo really umenitoa mazur kweli VINA NI HAFAHI KABISA
@josephcanizio
@josephcanizio 3 ай бұрын
Muziki unaishi na unajenga na kuponya hakika hii ni dawa kwenye kufkiria kabla ya kutenda❤❤🧠
@shaybumpala2062
@shaybumpala2062 3 жыл бұрын
Daaah We Ni Zaidi ya Binadamu Tulosimuliwa Vitabuni 🤔🤔🤔 Wewe ni Nani Unajua Kinoma Noma Sanaa Imeshibishwa Kabissah
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Appreciate the love brother. Please share
@ommymsomi4362
@ommymsomi4362 3 жыл бұрын
Ningekua baraza la sanaa ngomaa zako kaka zingetumika kujibia mitihan kaka...yan wanafunz ningewataka waskize kisha wachambue kila kipengele cha fasihiiiiiii
@lonely8682
@lonely8682 3 жыл бұрын
Najivunia kua shabiki ako bro...hujawahi kuniangusha🙏🙏🙏🙏🔥🔥🔥🔥
@dullywamashairi121
@dullywamashairi121 3 жыл бұрын
Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha kzbin.info/www/bejne/laeqpmeiZrKig9k
@GerrardTryphorn
@GerrardTryphorn 4 ай бұрын
Daaa hiingom Kali
@ombenedwin136
@ombenedwin136 3 жыл бұрын
Mungu ametupaga disaster vina
@franciscojonja1164
@franciscojonja1164 3 жыл бұрын
Asie elewa kazi ya hiki kichwa aisee hatokuja kuelewa milele @dizasta vina ndio nembo ya hip hop isio vunja nguzo ata moja ya hip hop brother umetisha sana
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Thanks, please share
@balikiabdala823
@balikiabdala823 Жыл бұрын
🤔🤔🤔🤔 Noma sana ngoma kali sana
@brainfigure94
@brainfigure94 3 жыл бұрын
Kuna haja ya dizasta kufungua chuo cha mziki wa hiphop ili vizazi vinavyokuja vielewe maana ya muziki wa hiphop
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
👏🏾 👏🏾 👏🏾 👏🏾
@sylvestermtweve2895
@sylvestermtweve2895 3 жыл бұрын
Dizasta..... you're very UNIQUE broo...Mungu akuzidishe maarifa na afya tele just because unajua kutupa Raha mashabiki zako..GOD BLESS TOUR TALENT
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Thanks bro
@vigangwaya8802
@vigangwaya8802 3 жыл бұрын
The best hiphop rapper kwa sasa nchini, hakuna wa kumzidi Dizasta vina kwa sasa
@boniphacelutusyo9110
@boniphacelutusyo9110 2 жыл бұрын
Hip hop 👍👍👍
@Mchora_tz
@Mchora_tz 3 жыл бұрын
Dizasta we jamaa ni hatarii no kiki no kelele ila mtaani unaleta kile tunachohitaji yaan hip hop ingekuwa hv labda tungeongea mengine mtaani #sioni km una ngoma mbovu
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
Appreciate, please share
@geofreymboyelwa614
@geofreymboyelwa614 2 жыл бұрын
Nyimbo nzur sana
@allymarumbo1088
@allymarumbo1088 3 жыл бұрын
What a lesson..daaaaaah We jamaa ni zaidi ya hip hop bro.
@ernestmajula5143
@ernestmajula5143 3 жыл бұрын
Dizasta ✌.. Mnyama mkali
@rehemaevans75
@rehemaevans75 2 жыл бұрын
Dizasta unajuwa bro nataman one day nikuone
@hon-mlenga
@hon-mlenga 3 ай бұрын
🎶🎶🎶🎶Dizasta nadownlod nyimbo zako zote
@vandiddyy5733
@vandiddyy5733 3 жыл бұрын
Duuh..! sijui nikupe jina gani broh... una hatari kubwa sana. 🙌🙌🙌
@dizastavina
@dizastavina 3 жыл бұрын
👏🏼👏🏼
@robifilosomaniofficialonli4272
@robifilosomaniofficialonli4272 3 жыл бұрын
Waaaaaah... Dizasta vina..tisha sana.. Kenya tunakuaminia.
Dizasta Vina - Hatia V
8:16
Dizasta Vina
Рет қаралды 121 М.
Dizasta Vina - Muscular Feminist
9:05
Dizasta Vina
Рет қаралды 107 М.
小丑家的感情危机!#小丑#天使#家庭
00:15
家庭搞笑日记
Рет қаралды 37 МЛН
Хасанның өзі эфирге шықты! “Қылмыстық топқа қатысым жоқ” дейді. Талғарда не болды? Халық сене ме?
09:25
Демократиялы Қазақстан / Демократический Казахстан
Рет қаралды 353 М.
msabato_ (speaking with my favorite raper) DIZASTA VINA
4:47
Msabato ze son
Рет қаралды 8 М.
Dizasta Vina - Hatia II
5:13
Dizasta Vina
Рет қаралды 115 М.
Dakika 10 Za Maangamizi-  Dizasta Vina | Planet Bongo I
12:06
EastAfricaRadio
Рет қаралды 736 М.
Fid Q x Saida Karoli - Kiberiti (Official Music Video)
7:34
LIVE: XTRA VINA | NI STORY MOB + VINA | DIZASTA VINA ON XXL
39:14
Dizasta Vina - Best Friend
8:28
Dizasta Vina
Рет қаралды 240 М.
Tribulation
11:27
Dizasta Vina - Topic
Рет қаралды 32 М.