Hakuna, narudia tena hakuna kwa wasanii wote wa tz anayefikia kichwa..hakuna
@kilingechasimulizi2072 Жыл бұрын
Nilikuwa namaanisha hakuna wa kufikia hiki kichwa
@kyataonline5262 Жыл бұрын
hakuna ! kwa nini hapati promo akaskika !
@emanuelmasanja8312 Жыл бұрын
Hapati promo wapi nani wapi hajasikika huyu kwa hapa hongo hayupo kama yupo mtaje jina
@emanuelmasanja8312 Жыл бұрын
Kyata! unajua misingi ya hip hop ama ndo whuzu na bonge la nyau
@kyataonline5262 Жыл бұрын
@@emanuelmasanja8312 hapana siijui buda
@dizastavina2 жыл бұрын
LYRICS Yeah Nilimfahamu baba alikuwa jasiri Aliondoa utando ulipodandia kuta Alitoa nyoka makatili alipambana na Majangiri walipovamia nyumba Aliweka paa juu vichwa Hatukuogopa baa la njaa tulishiba Niliona wengine nguo za kuvaa zimechanika Wakati kwetu nyuso ziling’aa migongo ilifunikwa Radi ilipiga wala sikujali Maana baba alikuwa Simba kwenye msitu mkali Wapo waliozijua sifa zake japo Mtaani halikuwika jina lake Halikuandikwa bali Waliona poa ilikuwa jukumu lake Mwanaume jasho kutoa ndio hukumu yake Ajali ya kisu iliondoa ngozi Sikumwona akitoa machozi Nilimwona kama Role model Alikuwa shupavu hakuwa na roho ndogo Mara chache alianguka ali-score zero Alipambana upya kama war Hero mdogo mdogo. Maisha yake yalikuwa ni adventure Alikuwa ni Handyman Carpenter Painter Alinijuza aliyoshuhudia kwa macho Maana Aliisafiri dunia enzi zake kama Vasco Alikuwa so gentle Alimpenda mama kupita maelezo Watu walijadili nini maana ya upendo Waliunda dhana mi niliiona maana kwa vitendo Huh Ugonjwa uliingia mama aliugua maradhi Homa ilivamia ghafla kupumua kazi Baba ali-suffer Hospitali kadha wa kadha Changamoto afya kupigania zikafungua jamvi huh Hali ilileta mtiti Hakuipata nafuu ugonjwa ulimweka kingi Baba aliwapa Waganga wakuu pesa nyingi Mixer kupelekwa majuu zinakoendeshwa ligi Mama alilala hospitali miezi kumi na nane Nyumbani miezi ilikuwa ni kama karne Tulimzoea mama baba hakupagawa Alisimama imara japo mambo hayakuwa sawa kamwe Maisha yalibadilika tukabadilika pia Familia ilipata shida ila baba aliisimamia Ukubwa ulimshika majukumu yalishika njia Yalimkaba shingo ila sikuwahi kusikia analia Bahari ikichafuka inampima nahodha wa meli Kama ataogopa kufa au ataongoza Kweli Lakini si mawimbi samaki waliododosha meli Bali ni rafiki wa karibu wa mama anaitwa Mary Mary alimjali baba alimzidi Rose Alimzidi Rahma alimzidi Shosi Alimletea baba kadi aliniletea chopstick Alifua nguo aliosha vyombo na alipika msosi Aliingia mpaka chumbani kwa mdingi Na udhaifu ukaanza yumbisha misingi Mary alimshawishi baba baba akaingia kingi, Kwa muda akamsahau mama akapitiwa akamsaliti ah Hamu ya tendo ikawazidi maarifa Kijakazi akazibeba taarifa Miezi kadhaa baada ya mama kupona Akasimulia yote aliyoyaona kama picha Mama akatokwa na machozi Baba akasota kwa magoti Mbele yangu mi mwanae mbele ya wazee Wakunga wa ndoa wenye busara waliobeba koki Huh Mama akapata mashoga wakali Walitoka jangwa la Sahara na Kalahari Wenye elimu za kutosha na ajenda kali Wakamwambia talaka ukiomba utazipata mali Mama akiwa na chembechembe za hasira Akashawishiwa na wasomi wenye hira kwa mbali wamezongwa na tamaa za ngawira Akasahau kumsamehe kama ilivyosemwa mila Mama akafungua jarada la talaka Akaandaliwa Majeshi waliojipanga kwa karata Baba aligoma kutoa talaka akiomba wamalizie nyumbani sio mahakamani na mama hakutaka Mji ulifahamu kesi iling’ara Yalipambwa magazeti mengi kwa nakala Wanaume washenzi waliongea wapambe Vijiwe vya uswazi waligawana pande ka masihara Mzee hakukataa mwisho akakili kosa Talaka ikaidhinishwa ndoa ikadondoka Baba akapata uchungu likamshukia rungu Kisha mama akaonyeshwa fungu akachota Afya ya mama ya uchumi na mwili vikanawiri Akawa Malkia mji ukatabiri Baba akawa kama kifaranga kwenye mvua Bado alimpenda mama na mama hakujua Mama aliitwa Superwoman ama soja Aliushinda usaliti aliushinda ugonjwa Baba alimkosa mama kwa starehe ya usiku mmoja Alimpenda mama hivyo kumpoteza maumivu tosha Washiriki wa biashara walimweka kapuni Akafukuzwa kazi asiharibu sura ya kampuni Vikundi vya kina mama walisherekea kombe Dingi aliipoteza kazi akaisogelea pombe Hakuwa sawa kichwani aliishiwa Energy Hakukuwa na counseling hakukuwa na Remedy Zaidi Makala zilizoandikwa na Mafeminist Pesa zilimwisha mtaani alifuga Enemies Magazeti hayakuandika alivyokuwa hero Yaliandika matusi yaliyomzidi kilo Aliitwa Malaya shenzi katili Mwanahizaya mwenye cheti cha ujangili Na yakapiga millions Hakukuwa na vyama vya wanaume kumtetea baba wakasema ana pepo la uzinzi Ustawi wa maisha yetu ulipotea ghafla Wanasheria wakala na pesa za ushindi Aliumia peke yake Dunia ilimweka peku Dhambi ilimwacha uchi hadharani Alifanya mema zaidi ya kumi hayakutosha awe Yesu Ila baya moja aliitwa Shetani Alizubaa Alizubaa na akashikwa na madoa Alikuwa shujaa ila alishindwa kujiokoa Mwamba wa nyenzo ya katikati ulipoondoka Ilimaanisha ni muda wa Safina kudondoka huh Hazikusikika sifa zake njema Machozi hayakusafisha jina lake tena Haiba alizokuwa nazo hazikuvutia kamwe msongo nao wa mawazo ukamvamia Mfalme Aliandika barua ya hadithi yake Akisema kilichomtesa sio dhiki yake Bali ni uzito wa alichokifanya Alijiua kando ya bahari uliokotwa mwili wake
@umodernize41422 жыл бұрын
You
@alphanlukombe37742 жыл бұрын
Hii kali sana hili ni fumbo tuliolielewa watu wachache sana nakubali sana dizasta vina katika uandishi wako mtu akisikiliza juu juu anaweza akaona kawaida lakini hii Ngoma umeimba mambo makubwa sana kwa sisi waelewa dizasta vina on top
@reganmmasi12462 жыл бұрын
Sasa mkuu mbona pale spotify kama umetutenga hiv...😕😕
@decoderhealthusa2 жыл бұрын
Always upo tofauti sana na hawa wasanii wetu, wewe ni sanaa.
@dizastavina2 жыл бұрын
@@reganmmasi1246 ipo njiani
@jolamboi88422 жыл бұрын
Dah dizasta ndio my favorite rapper ebu tupia like kama una mkubali mwamba 🔭
@timothykaiza3272 жыл бұрын
Iko Auto playing saa mbili sasa, ni ngoma yangu ya leo kutwa mzee. Tunaozidi irudia HATIA V tukutane hapa. Nitumie mimi kama kitufe cha kukubali ujumbe huu.
Wimbo wa dakika 8, hauongelei siasa wala mapenzi... Story fulani iliyotilia kuhusu familia. Dizasta Vina is the Legend🔥
@revocatusnzungu65802 жыл бұрын
huwa natamani kila mwezi jamaa atoe ngoma dah ... kuna watu tuna arosto na ngoma zako broo dizasta
@stonestz88152 жыл бұрын
Dizasta dizasta dizasta ndo toleo la mwisho la viumbe aina ykooo
@mtasma19942 жыл бұрын
Mimi huwa simfananishi Dizasta na Rapper yeyote
@millardmbaraka61142 жыл бұрын
Alafu anatokea muhuni mmoja anamlinganisha D vina na makinda dah! Umejua kutufungia mwaka na tafakuri murua kabisa
@reeckstar9312 жыл бұрын
All way from Switzerland 🇨🇭🇨🇭🇨🇭 nnasubili chakula Cha ubongo
@reeckstar9312 жыл бұрын
😭😭 kwanini wa bongo hawaamki kumpa sikio dizasta
@Mr.Kibabu2 жыл бұрын
Dizasta hajawahi niangusha, Kichwa kweli kweli, Huwa na Like kwanza ndio naanza kusikiliza, Msanii wangu Bora wa HIP HOP
@ablemuxic73342 жыл бұрын
Kwa mwaka huu hii ndo nyimbo yangu bora ahsante Sana D 🔥🔥
@dizastavinafanaccount2 жыл бұрын
Sanaa yenye usanii. Mwendazake Mr Magufuli. Akitenda kosa lakini upendo na uzalendo wake kwa hili taifa ulikuwa juu ya maelezo. Dizasta amesymbolise kupenda na kujali ni kama kujiua mwenyewe. Kalamu ya Dizasta si ya kawaida
@joshmangi2 жыл бұрын
Hizi juhudi zinahitaji malipo, weka lipa namba watu wachangie hizi juhudi.
@nillyjos12032 жыл бұрын
Daah kaka Tanzania nsima wew Ndo msani Bora Tanzania nzima
@allysaleh22205 ай бұрын
Huyu ni msanii wa dunia sio tanzania2 jamaa ubongo wake sio wakawaida
@rogathpanga2 жыл бұрын
Yaah Nilimfahamu baba alikuwa jasiri
@kaissalum73642 жыл бұрын
Duh bro sina mengi ebu weka namba Nikutumie chochote kitu nakukubali sana
@petercharles85722 жыл бұрын
Kwenye harakati za kumpandisha mwanamke kuwa sawa na mwanaume zimekuwa harakati za kumkandamiza sana mwanaume na sio tena kumuweka mwanamke awe sawa na mwanaume... Dizasta ametuonyesha jinsi mama alistawi kutokana na dunia nzima kuwa upande wake na baba hakusikilizwa. This man deserve 01, Ni jambo la kujivunia kuwa wakati mmoja na dizasta vina... Bahati mbaya kwa wote waliotamani kumsikiliza msanii kama huyu ila hawakufanikiwa kwasababu waliku past na records hizi mustakabari mzuri kwa kizazi kijacho. We love you Dizasta Vina
@dizastavina2 жыл бұрын
Feeling is mutual, cheers
@shehakudura32432 жыл бұрын
Aisee kwenye taswira ya kifamilia,,,, W,ume tujipe Poole,,, coz hakuna mafanikio ya watoto na family kiujumla bila Baba kusmama vyema,,, Ila aisee shiida ya UMUHIMU WETU kutoonekanwa na kuthaminiwa na KUTENGWA kwa KOSA Moja aisee,,, INAUMAA SANA....
@mbarakamngayunga95582 жыл бұрын
Daaaah,aisee sikutegemea kama ningekutana na idea kali kama hii...wewe brother dizasta ubarikiwe sana...Nyimbo zako zinanifunza sana❤
@octavian542 жыл бұрын
Unafelii wapi huyo ndio Mwenye mziki wa hip hop
@amalillahasante66932 жыл бұрын
Kweli mwanangu.
@babamasakalanga56872 жыл бұрын
Daaah hii ngoma imenitoa chozi nimekumbumbuka mbal sana😭😭😭😭😭
@idrissachisigwa53602 жыл бұрын
Noma sana
@shehakudura3243 Жыл бұрын
@@babamasakalanga5687 for real Yani inaniumiza sana hii ngoma aisee,,,, W,ume thamani yetu mbinguni ila tunavuja Jasho hatari lakin mwishoe tunaambulia kisukari na presha
@richardmloha17622 жыл бұрын
Jamaa n anaumiza ndongaa wazee kwanin lakin ngoma Kama hizi watu wake wanashindwa kuwa na maslahi yanayoendana na hustles zaoo daaah 😓 em sisi mashabiki tuanze na hii ngoma iangalie ata Mara 5 utatisha sanna let's go
@Makavelithedon20862 жыл бұрын
*Dizasta Vina ni moja kati ya best lyrical rapper kuwaikutokea Tanzania*
@renatusmsakula47462 жыл бұрын
Anaetaka kujipima na wewe hatokua SAFE yaani no body is safe!!!
@shariffahmad87052 жыл бұрын
Kama messi alipata alichostahili kwa miaka yote hiyo amini ndugu yangu utapata unachostahili one day keep it on unajua mpaka unajua tena akili mingi mtu wangu
@johannesjoseph74962 жыл бұрын
Hakika unadhihirisha kwamba unaishi kwenye dimensions ambazo miungu ndo inasettle..... Hatia 1-5 zote mwisho wa siku lazima ujiulize nani alikosea zaidi..kila muhusika anakua na excuse ya kutenda makosa ijapokua uwezo wa kuyaipuka unakuepo japo mdogo kulingana na mazingira, I salute you our best storyteller the verteller
@stevenjohn78162 жыл бұрын
Hii ni film iliyokamilika kabisa bongo muvie karibuni
@mathayobmasunzu278Ай бұрын
Kw bongo movie Mary n star w movie 😂😂
@francismasanja55502 жыл бұрын
This talented man should be crowned. What a good music, what a strong message. This is what a literature is and means.
@amalillahasante66932 жыл бұрын
Trust
@johnizoboy2 жыл бұрын
Very true🔥🔥🔥
@selemaniselemani5912 жыл бұрын
Haichoshi kusikiliza Leo hii ni mara ya 16 bado Radha ni ile ile Kama ile Ngoma ya tattoo ya asili bro wewe ni nyoko naomba nikusifie kabla hijafa wewe ni nyokooooooo🔥🔥🔥🔥
@valencepaul46042 жыл бұрын
Uliletwa kwa ajili ya HIP HOP wengi wamefichwa wewe ni nani ila ni zaid ya rapper zaidi ya mwalimuu wa jamii,,,,napo play ngoma zako hadi wazee wanauliza huyu ni nani😀💥💥UNAJUA SANA MIMI NI MFUASI
@alimkumba94592 жыл бұрын
mtu yeyote anamsikiliza dizastar naamini hatoweza kuupoteza mziki wa huyu mwamba kwenye kuta za sikio zake nahisi huyu sio mtu wa sayari hii
@erastompongo84002 жыл бұрын
Duuuh we jama ni mnoma sana wangapi wanailudia rudia
@odiloodilo2 жыл бұрын
Me nishabiki yako sik zote, kaka upo vizuri sana 👍💯💯💯💯🙌
@Zabron_Hongoli2 жыл бұрын
Kweli mazuri kumi hayawezi kufanya uitwe Yesu but baya moja utaitwa shetan The game is in yourself hands prf tungo
@ahmedramadhani12642 жыл бұрын
Binafsi nimeisikiliza zaidi ya mara tano kwenye simu na bado naendelea kuisikiliza. Noma sana hii kitu.
@Sportycorner2 жыл бұрын
Bro una akili Kubwa wewe sio msanii wewe sio Mwana Muziki wewe Ni Legendary wa Maandishi, sauti na Midundo The Story Teller Never Seen Before Keep Pushing Vinna
@isdoryemily5029 Жыл бұрын
Uyu mwamba amejua kunibadirisha sinaga mshauri nyimbo zake nikisikia najifunza na mtaani naitwa Hip Hop culture
@morganmwaikusa81942 жыл бұрын
Genius.... Huyu Edgar anajua mpk anakela yan....
@fourteen_kiid2 жыл бұрын
argentina wana messi bongo tuna dizasta vina the black maradona 👏🏾🙌🏾🔥
@jaymbawal2492 жыл бұрын
Dizasta vina mkali san kam una mfatilia 🔥🔥🔥🔥 sikuping broo
@Jumajing2 жыл бұрын
Hii ni zaid ya Wimbo bora wa Mwaka kaka, Funzo,Vina na 🔥🥂
Huu uandishi ni zaidi ya Hisabati🔥🔥🔥🔥🔥Huu ni zaidi ya Wimbo🔥🔥🔥🔥This Guy deserve a Crown🔥🔥🔥🔥Anafanya Rap ionekane kitu chepesi sana kuisikiliza, Story Complex yenye Flow na Rhythm tanu sana🔥🔥🔥🔥ni zaidii ya Fundisho🔥🔥🔥Kuwaunganisha Fanani na Hadhira kwa Dakika 8 na kuelezea tukio ambalo limetokea zaidi ya 10+ is next level🔥🔥🔥🔥🔥Absolutely Perfect🔥🔥
@choineymar97652 жыл бұрын
Phenomenon lyricist
@decoderhealthusa2 жыл бұрын
Kiufupi tuwe tunafanya malipo kusikiliza hizi tenzi
@johnizoboy2 жыл бұрын
@@choineymar9765 Absolutely
@idmpros2 жыл бұрын
nomaaaa sasa @dizastavina wewe upo mbeleeee sanaaaaa ya Muda Trust me watu ni kama hawakuoni BUT I BELEAVE IN GOD TIME WATU WATAKUZINGATIA KWA KISHINDO
@macberryofficial2 жыл бұрын
Ooh i have been just listening to your song SHAHIDI and NDOA, and i just see this one😊😊😊 man Dizasta i love your songs fasho! Huyu ni Fan wako kutoka 🇧🇮Burundi🇧🇮 hujawai kuniangusha Dizasta Vina😊💪💪💪
@erickpaschaljr86672 жыл бұрын
Ninamshukuru Mungu kwa zawadi ya mziki mzuri wa Dizasta vina yawezekana sisi ni watu wenye bahati sana ila bado hatujatambua thamani ya utunzi usio wa kawaida.
@luganomoses208825 күн бұрын
katika watu ambao siwachoki kuwasikiliza ur the one brother ila sijui hawa wanao imba makelele wanapataje muda wakuwa on top na tuzo kubeba wakati awaitendei haki hip hop
@raymondedson24882 жыл бұрын
Sehem moja ya kuufungua ubongo WA vijana ni kupata hadithi na zimulizi kama hizi Hakika we ni mwalimu WA fasihi na si mwalim Bali mwandishi bora WA muda wote katika game much respect brother
@filbetdaud45972 жыл бұрын
mamaeh aisee iki n kichwa na nusu aiseee Mzee D unaandika sana unaandika sanaaa kaka unaandikaaaa nasemaaa unajuaaa sanaaa D ish sana mflame D
@mkanganails58392 жыл бұрын
Daaa aisee unabalaa zito wewe una hatareeee mwamba
@octavianmushi9282 жыл бұрын
Bro Mungu akubariki kwaelimu ya bure uliyotupatia... Mungu akulinde sana...🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻
I remember 27th December last year i got myself a copy of ‘The Verteller’. I promised myself to keep on buying Dizasta Vina’s art at any reasonable cost. All hail to the King of Underground 🙌💪
@nicky30252 жыл бұрын
We jamaa👐
@hurumamwankuga66632 жыл бұрын
Style yako Ime inspire rappers wengi but hiyo hiyo style Iko tofauti na wao bcz unavyotema na wanavyotema there are so different 👐👐
@braytonedaniely79772 жыл бұрын
Tym yako ndo hii mwanetu utaeleweka tu siku moja✌
@jibrilsheikh99492 жыл бұрын
Huyo jamaa Ni Noma... This is pure talent ❤️❤️❤️. Tunapenda kazi zako Safi Sana kutoka Kenya
@dedeayew96502 жыл бұрын
Ambae hatapenda hizi lyrical aisee huyo hajui music
@MasasiVisionTv2 жыл бұрын
DIZASTA VINA 🙌🏿 usiku mmoja umebadili fomat yoot y maisha duh 😔
@mr.theory58712 жыл бұрын
Oyaaaaa mwamba anaandika hadi anaandika tena,cha ajabu tuzo kwa wanaosifia ngono!
@johnngowi83342 жыл бұрын
Noooma sana aisee , wew ni mkali saaana hapa bongo unandika sanaaaa⭐⭐⭐⭐💥
@yusufuselemani63392 жыл бұрын
Good work kutoka kwa narrator bora wa mda wote, Sema D humu na muona hayati kabisa kazungumziwa 😀😀
@jumazinga9412 жыл бұрын
Ama kweli baba atabaki kuwa hero
@kioochafasihi Жыл бұрын
Dizasta na mimi ni miongoni mwa madini adhimu kabisa kwenye kiwanda cha Hiphop ya Afrika (swahili rap)
@raphaelmwangosi92952 жыл бұрын
Kak daaaaaaaa cjui tusemeje mwanang ila bc wameweka tasnia chino ila tunakuexhmu 💪💪💪🥰😍🥰🥰🔥🔥🔥💥💥💥
@eliamhiro47372 жыл бұрын
Huyu jamaa nilikua simjui asee
@abdulkara23272 жыл бұрын
Kutoka Zanzibar kama unamkubali dizasta gonga like mwanangu kumaanisha huyu jamaa ni mwamba
@ibrahimukasimu33862 жыл бұрын
Kaka shikamoo we unajua mpaka nawaza kuwa haujatoka latina hii planet dah uno amor amigo god bless u on ur evry step of ur lyfe
@MoreWarzone2 жыл бұрын
Kaka we tukujengee sanamu tuu … unajua kuandika
@dickmlawa88432 жыл бұрын
Asante kwa kunipa jibu D ni 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
@ausiissa71552 жыл бұрын
Kuna mda uwa nikisikiliza nyimbo zako nikisema unajua naona Haitoshi inabidi tu niwambie wasio kujua kwamba unajua ili wao pia wakatoe ushuhuda ✨✨Mungu akuweke sana kaka✨✨
@peterbahati9242 жыл бұрын
This is the real meaning of Hip-Hop. He is the real meaning of Rapper, doing things never been done before🔥🔥
@zombiiUpdates2 жыл бұрын
Vina ni dizasta
@kiondosaimon61492 жыл бұрын
Always de Best unajua sanaaa mzeee hakuna wa kushindana na ww Bongo hapa 👊👊👊
@ahmedsdk67362 жыл бұрын
Ya Moto sanaa Hiii... 🔥🔥🔥
@Lukona6392 жыл бұрын
Dah sijui kwanini nimeusikiza...Nimeishi katika hyo mistari kama natazama movie...Umeniacha na Majonzi mjomba but...Yeah Nilimfahamu baba alikua jasiri....Wapo waliozijua sifa zake....Mtaani halikuanzikwa jina lake.....Alifanya mema zaidi ya kumi hayakutosha awe Yesu...Ila baya moja aliitwa Shetani Alizubaa...WOW
@g_eazmusic13292 жыл бұрын
Kosa moja mtu anasaau wema wote
@eugenbaraka2502 жыл бұрын
Duh kaka sikuwezi🙌
@moziidavchonchi33382 жыл бұрын
Bro unajua kichiz🙌🙌🙌🙌
@StimaOfficial2 жыл бұрын
Sijawah kuchoka kuzipakua na kuskilz hizi punch mzee wa Panorama Professor Tungo💪💪💪
@originalnchimbi73602 жыл бұрын
Daaah nyimbo nzuri
@openmindtz2 жыл бұрын
Too pain nais kama ni mm ndo baba... life is so complicated aliitaj faraja pale penye uzito ubinadam ukampoza sasa ana onekana zito... rest in peace baba na ukiangalia in really life ma baba weng wana fight sana bt they would never let a sight on us
@baloziubalozini50742 жыл бұрын
-Hasira ya Mama ilikua ni kuomba Talaka -Hasira ya Jamii ilikua ni KUMHUKUMU BABA -Hasira ya Baba ilikua ni KUJIUA Kwakua Death ni "ABSOLUTE FREEDOM" Japo Msibani mama atalia kwa Uchungu na Jamii itahuzunika(KINAFIKI ZAIDI) ila inapaswa WAFURAHI. Moral of the story-Jifunze kujifunza kusamehe
@macpharaonofficial2692 жыл бұрын
Hiki chombo Cha mistari vina hua nakikubali siku zote🔥🔥🔥 keep shining Brother ✌️✌️✌️
@hassanmakweto62992 жыл бұрын
Yeah hii ndio mind food💪💪💪 afu kweli rapcha abishana na kaka zake kama hawa?
@delymoebright93262 жыл бұрын
Tulio elewa kilicho imbwa tujuane dah🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
@kennethmbilinyi41712 жыл бұрын
Sinachakusemaa Mzee niutamuu tuu great
@joycelugenzi18892 жыл бұрын
Kaka mm cjui ata niseme vp .but nakupenda xana i wish nipate mda wa kukuona hata 2ongee nahisi ningejifunza mengi kuhusu hii dunia .nimeipenda xana nyimbo .😍😍😍
@moureennassoro10482 жыл бұрын
Jamii imeshiba sana ujinga dats why you are not fumes. Dizasta vina ni mmoja tu Dunia nzima. Huwa anazaliwa mmoja tu toleo la aina yako. Dizasta vina, unasikilizwa tu na watu wenye akili timamu. Busara ipo moyoni, hekima ni busara inayozungumzwa. Dizasta vina, naandika jina lako kwa heshma kubwa zaidi ya ninavyolitamka. Dizasta vina, begani mwangu jina lako nitalichola tatuu , najivunia msanii wangu na sio 2pac Shakur Dizasta vina. Usisahau kuwa wakati unasifiwa, bado hauko kwenye njia yako mwenyewe, bali upo kwenye njia ya kupendeza kwa wengine. Hapo namaana kuwa bado nataraji kushuhudia kazi zako nyingi na za hatari zaidi ya tunavyokujua sis Media wanaogopa nyimbo zako
@joshuacharles43132 жыл бұрын
Ongera sana kaka nimeirudia hii nyimbo mara 8 toka ulivyo iachia nihatari sana inahitaji utulivu kuielewa heshima xana kaka nakukubali sana.
@bennyblac0621 Жыл бұрын
Daaah ww dizasta ni mtu wa aina gn na unafikira gn aiseee daaah napata ile ladha ya mziki na fikra ambazo havizungumziwi kwenye mziki huuuu aisee
@pascodickson30522 жыл бұрын
Stoy teller.. Noma sana..
@smigorjunior43512 жыл бұрын
Dah brooo wewe ni 🔥🔥🔥
@xylomyxdisophie20112 жыл бұрын
broo surely ww n msanii ulienitoa kwa life moja kwenda step nyingin......
@rashidiramadhani14202 жыл бұрын
🔥🔥🔥🙏🙏🙏 hatari sana Brother
@sabagumasanja80012 жыл бұрын
Mm namlaumu sana dada wa kazi😥😥😣
@UNIQUEMEDIATZ2 жыл бұрын
Dizasta ww una kichaaaaa so goma hili atare⭐⭐⭐⭐
@mansourabdul39022 жыл бұрын
Keep it up aisee unaandika leo ndio mara yangu ya kwanza kuusikiliza na kukujua ila sasa nihesabu kama shabiki yako sasa