Рет қаралды 177,406
Naweza kusema kila kukicha kazi mpya za Music Video Bongo hutoka na kuwabamba sana watu kwa maana ni kazi nzuri na za kuvutia lakini huwa wanasahau utofauti wa kazi ukiacha quarity.
Hapa nazungumzia utofauti, Music Video hii ya One Minute nimeipenda kwa kuwa ina muonekano tofauti kuanzia Rangi na pia story yake jinsi ilivyopangwa.
Ni kati ya kazi mimi kama mdau nimevutiwa nayo sana kwani inaonyesha jinsi gani Watanzania tunavyojitahidi kufikia walipo wenzetu wa waliotutangulia katika nyanja hii.
Waandaaji au Waongozaji walikaa chini na kujuwa nini kinatakiwa katika kubadiri muonekano tuliozoea.
Emptysoulz Production imeliangalia hilo na sasa imetoa jibu, naamini Watanzania na Majirani zetu watakubali kwa % furani kuwa Video hii ni nzuri na ipo tofauti.
Big Up sana Director wa Video hii bwana Solomon Lamba kazi zako zimesimama na ukaze kamba kwani safari bado ni ndefu.
Artits: Giddy Feat Godzila + Young D
Song: One Minute
Music Studio: 24/7 Records
Producer: Villy
Video Production: Emptysoulz Production
Dir: Solomon Lamba