Рет қаралды 306,501
Mvutano mkali umeibuka bungeni leo Juni 4, 2025 kati ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuhusu kiwango cha sukari ambacho nchi imeagiza kwa ajili kuondoa upungufu uliopo, ambapo Mpina amesema upungufu uliokuwepo ni tani 110,000 na hivyo kuishangaa wizara kuagiza tani 410,000.
Katika maelezo ya Waziri Bashe amesema kuwa sukari hiyo imeagizwa ili nchi inaposimamisha uzalishaji mwakani, kuwepo na sukari ya kutosheleza kwa miezi miwili ambayo uzalishaji utasimama.
Mpina ameliambia Bunge kuwa Waziri Bashe anadanganya, na hivyo Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akamtaka kuwasilisha uthibitisho kuwa waziri amedanganya Bunge, kama ambavyo kanuni zinataka.
Je, Mpina anao ushahidi? Kanuni zinasemaje akikosa ushahidi? Endelea kufuatilia TBC Digital.