HIVI NDIVYO KADA WA CHADEMA ALIVYOTEKWA NDANI YA GARI, MASHUHUDA || KONDAKTA WA BASI LA TASHRIFF

  Рет қаралды 64,665

Mwananchi Digital

Mwananchi Digital

Күн бұрын

Gari mbili zilizokuwa na namba za usajili zisizo za kawaida, ndizo zilizotajwa na mashuhuda kuhusika katika tukio la ukamatwaji wa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema, Ali Kibao Ijumaa ya Septemba 6, 2024.
Kwa mujibu wa mashuhuda tukio hilo lilitokea saa moja jioni, muda ambao tayari giza lilishaanza kuingia na hakukuwa na aliyekuwa na wasiwasi kwa kuwa walidhani wakamataji ni askari wa Jeshi la Polisi.
Kibao, alikamatwa Ijumaa ya Septemba 6, 2024 Tegeta mbele ya Jengo la Kibo Complex na siku moja baadaye mwili wake uliripotiwa kupatikana Ununio, jijini Dar es Salaam akiwa ameuawa huku uso wake ukiwa umeharibika kiasi cha kutotambulika.
Mwili wake ulipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na ulifanyiwa uchaguzi wa kitabibu na taarifa yake bado haijawekwa wazi. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amedai kifo cha Kibao kilikuwa cha mateso na uso wake ulimwagiwa tindikali.
Leo Jumatatu, Septemba 9, 2024, Mwananchi imefika Tegeta alikokamatwa Kibao ambako ni umbali wa takriban mita 20 kutoka Jengo la Kibo Complex, ni eneo ambalo aghalabu mabasi yanayoelekea Tanga, Moshi na Arusha husimama kupakia abiria.
Kama ulivyo utaratibu wa kawaida, basi la Tashriff alilokuwa amepanda Kibao lilisimama kupakia abiria kwa mujibu wa mashuhuda, gari mbili zenye namba nyeupe ambazo zimeandikwa kwenye vibao vyeusi.
Shuhuda huyo ambaye ameomba hifadhi ya jina lake, amesema gari moja iliegeshwa mbele ya basi hilo na lingine liliegeshwa nyuma ya basi hilo, kisha watu wanne walishuka kwenye gari hizo.
“Wanne wote walikuwa na risasi (akimaanisha bunduki) alienda kwenye mlango wa basi na wawili wakaingia ndani, wawili walibaki mlangoni,” amedai.
Alichokisikia shuhuda huyo ni kauli kutoka kwa mmoja wa watu hao kuwa, ‘tumemfuata mtu wetu’ na kwa namna walivyokuwa kila mmoja alidhani ni polisi.

Пікірлер: 45
@shadrackCharlesmaasai
@shadrackCharlesmaasai 5 күн бұрын
Mwenyezi mungu atawalipish walio Fanya hivyo jaman kutoa mtu uhai na sio mpango ya mungu nimbaya Bali tuachie mwenyezi mungu KAZI yake😢😢😢
@ShabanJinga
@ShabanJinga 19 сағат бұрын
inshaa allah mungu atalipa tu kama c duniani akhera kwa wote wanao hucka
@ShabaniMussa-f3k
@ShabaniMussa-f3k Күн бұрын
Wallah mungu hana hongo iposiku na wao vifo vyao vitakua vya kushangaza nch zaidi ya huyo walicho mfanyia ss wa Tanga tunalia na mungu tu.
@MzeeOsama
@MzeeOsama 2 күн бұрын
Munguaywekerohoyakemahalipema
@BakariMussa-to2me
@BakariMussa-to2me 7 күн бұрын
Mwenyezi mungu atalipa kwa zulma iliyo fanyika na amini mwaka hauto Isha inshaallah
@hapynessmichael
@hapynessmichael Күн бұрын
Hv kwn nchi yetu bdo ni ya amani uongooo😢
@SabraSaid-g7i
@SabraSaid-g7i 3 күн бұрын
Hii nchi hinakoelekea lawama kwà serekali tuu haiwezekani mtu hachukuliwe kwenye gari mbele ya watu na kupigwa pingu halafu huseme wasionulikama si kweli
@ilynpayne7491
@ilynpayne7491 7 күн бұрын
Sad 😢
@josephlorri431
@josephlorri431 7 күн бұрын
Kampuni hiyo ishtakiwe kwa kushindwa kumlinda abiria wake... nchi za watu waelewa wangekwenda kituo cha polisi tena wanamkabidhi kwa maandishi.
@DanFlavourTz
@DanFlavourTz 6 күн бұрын
mmh sasa kampuni ina kosa ganiii mzee
@jabiraxmed7898
@jabiraxmed7898 6 күн бұрын
Ni polisi au usalama wa taifa
@josephlorri431
@josephlorri431 6 күн бұрын
@@DanFlavourTz kwa nini waliruhusu mteja wao kuchukuliwa kihuni tena akiwa amekaa tayari na watu ambao hawafahamiki.. wangepeleka gari kituo cha polisi
@DanFlavourTz
@DanFlavourTz 4 күн бұрын
@@josephlorri431 kaka watu wameingia na mashine ndani ya gari na wewe huna hata fimbo hivi utaongea kwelii kumbuka kuna maisha baada ya udriver
@josephlorri431
@josephlorri431 4 күн бұрын
@@DanFlavourTz muhimu tumejifunza jambo... vijijini watu wameanza kujilinda wenyewe..wasipokuelewa unashughulikiwa kisawasawa..
@tatizojoseph8702
@tatizojoseph8702 Күн бұрын
Nchi yangu Tanzania sasa nakua naogopa kesho yangu itakuaje!! Na Mimi sio muda nimuhanga!!!
@OmanOman-bx5du
@OmanOman-bx5du 7 күн бұрын
Sikuizi ukion mtu anamatwa inabidi watu kwa mdauo mupaze sau ti msikae kimya
@kwilasacharles1747
@kwilasacharles1747 7 күн бұрын
Hatari sana 😭😭😭
@BahatiIsangu
@BahatiIsangu 5 күн бұрын
Wanatanga somen albadir
@user-gj7de4xt6z
@user-gj7de4xt6z 3 күн бұрын
Kwenye bas kunakuwaga na Camera ,sidhani kwa muonekana wa bas hilo litakosa Camera kwani na narabarani si kumefungwa kamera za kuangalia mwendo wa mabasi??au ndo zimeshakufa na kuachwa mijegeje??mmmmh hatar sio salama
@nicholauskilosa5336
@nicholauskilosa5336 7 күн бұрын
Kazi ipo
@user-vz8ty1ed5e
@user-vz8ty1ed5e 2 күн бұрын
Tumeisha
@zully756
@zully756 7 күн бұрын
Alikamatwa au alitekwa?
@PiddyMchiwala
@PiddyMchiwala 3 күн бұрын
Hawa ccm kwa namna hii basi watatumaliza.hapa tunalazimishwa kuihama nchi ambayo tuliipenda,R.I.p kibao
@IvanMocha
@IvanMocha 3 күн бұрын
Wamemkatili baba WA watu
@simonIbrahim-hc8vm
@simonIbrahim-hc8vm 7 күн бұрын
Sawa tu 😢
@barumoussa426
@barumoussa426 4 күн бұрын
Hivi ndani ya basa hamna mtu yoyote alipata kurikode tukio hilo??
@FrenkMwaulambo
@FrenkMwaulambo 6 күн бұрын
Hiyo ni hatari Sana tanzania
@HemedMangon-n2l
@HemedMangon-n2l 2 күн бұрын
Duuh
@EvodiusLaurent-ud7ns
@EvodiusLaurent-ud7ns 5 күн бұрын
So Kila mtu aitwaye mama ukadhani wote ni wenye huruma , mungu ndio atahusika na hukumu kwa yoyote alie husika kwanamna yeyote
@livingstonekabantega
@livingstonekabantega 3 күн бұрын
mtu anakamatwaje Bila wenye basi kujua anaenda wapi
@samwelmohonge4573
@samwelmohonge4573 5 күн бұрын
Kukamata sio huko, huu ni utekaji wa kijinga usiokubalika katika ulimwengu wa demokrasia, very shameful 😢
@BilalMuhammad-jt6sq
@BilalMuhammad-jt6sq 7 күн бұрын
Kwaiyo hiyo bus hata kamera haipo
@RizikiMlela
@RizikiMlela 7 күн бұрын
Hiyokambuni yabasi inahisika utakubarivipi abiriawako anachukuriwa naweweunakubari kiuraisi weweunajua wariomchukia
@jabiraxmed7898
@jabiraxmed7898 6 күн бұрын
Ndio ni askari wa police na usala.a wa taifa mbona munaogopa kusema
@salmakirundu2076
@salmakirundu2076 6 күн бұрын
Kwanini watu wa kwenye bus wasichukuwe video
@JacquelineMahumbe
@JacquelineMahumbe 6 күн бұрын
Mama acha kutukejeli
@salmakirundu2076
@salmakirundu2076 6 күн бұрын
Ingesaidia police
@DenisTarimo-bf4zq
@DenisTarimo-bf4zq 7 күн бұрын
Sasa hizo gari ni za nchi gani
@geraldabel8784
@geraldabel8784 6 күн бұрын
wazee wa tanga pigeni albadiri hili haliwezi kupita hivi hivi.
@julianamwamgogwa
@julianamwamgogwa 4 күн бұрын
Muuaji makubwa wewe.we si ndoumeagiza haya mauaji?
@SeverinepauloPeter
@SeverinepauloPeter 7 күн бұрын
Kumamaake hii nchi mtatuuwa wote ilo siku chapati itageuka
@BakariMussa-to2me
@BakariMussa-to2me 7 күн бұрын
Lazima wazee wa tanga tukae kitako hi zulma tumkabizi Allah tunayo imani kila alio husika nahili tukio ajiandae
@mohamedbedui9486
@mohamedbedui9486 7 күн бұрын
Huo ukoo sio mdogo una stori kubwa waliohusika na kushiriki huu mwaka haupinduki
哈莉奎因怎么变骷髅了#小丑 #shorts
00:19
好人小丑
Рет қаралды 34 МЛН
GWAJIMA ATAJA watekaji, BILA UOGA Ataja MAJINAAAAAAAAAAA
13:23
MALAVIDAVI Kenya
Рет қаралды 136 М.