Рет қаралды 93
Huduma za Msaada wa Kisheria zinatolewa bure nane, nane - Dodoma, Wananchi changamkieni fursa
Wananchi wa Mkoa wa Dodoma na maeneo ya Jirani wametakiwa kuchangamkia fursa ya huduma za msaada wa kisheria zinazotolewa bure na Serikali kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid kwenye banda la Wizara ya Katiba na Sheria lililopo katika Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Nzuguni Jijini Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo tarehe 4 Agosti 2024; Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ambaye pia ni Msajili wa Mashirika yanayotoa huduma hizo Bi. Ester Msambazi amesisitiza kuwa huduma za msaada wa kisheria bure kwa Wananchi zitatolewa viwanjani hapo hadi tarehe 8 Agosti 2024.
“Wananchi watumie siku hizi kwa ajili ya kuja kupata huduma za msaada wa kisheria lakini kwa wale walio nje ya Mkoa wa Dodoma wanaweza kufika kwenye mashirika yanayotoa huduma za msaada wa kisheria katika maeneo yao ili waweze kupata huduma hizo kule kule walipo’’ ameongeza Bi. Ester.