Рет қаралды 20,313
Je unajua kupika mkate bila oven? Angalia Jinsi ya kupika mkate KWENYE FRAMPENI hatua kwa hatua. Hii ni njia rahisi ya kupika mkate nyumbani bila oven. Mahitaji yake ni rahisi kwa kila familia.
MAHITAJI;
Unga wa ngano(500g/nusu kilo)
Maziwa ya vuguvugu (250ml/ robo Lita)
Maji ya vuguvugu (100ml)
Hamira (vijiko 2 na nusu vya chai)
Chumvi (kijiko 1 Cha chai)
Pilipili Kali 1
Vitunguu maji (2 vikubwa)
Parsley/mbogamboga
Mafuta ya kupikia (vijiko 6 vya chakula)