KAULI YA UMMY BAADA YA KUKABIDHI OFISI KWA JENISTA MGAHAMA ASESEMA SINA SHAKA...

  Рет қаралды 20,924

Mwananchi Digital

Mwananchi Digital

Күн бұрын

Ummy Mwalimu, aliyekuwa Waziri wa Afya kwenye mitandao ya Kijamii walimwengu wamempa jina maarufu la Oddo leo amekabidhi ofisi kwa Waziri wa Afya Mteule
Ummy anatajwa kama Waziri wa Afya aliyedumu katika utumishi wa Uwaziri katika awamu tatu tofauti kuanzia ya Rais Jakaya Kikwete, Hayati John Pombe Magufuli na ya Samia Suluhu Hassan amekabidhi ofisi kwa Jenista Mgahama jana Ijumaa Agosti 16,2024.
Baada ya kukabidhi ofisi hiyo, Ummy kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika;
Alhamdulillah. Leo nimekabidhi Ofisi
kwa Mhe Jenister Mhagama, Waziri wa Afya.
Awali ya yote, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi
Mungu kwa neema na baraka zake na kwa kila hatua tupitazo kwa kuwa zimezungukwa na neema zake ikiwemo kupata kibali cha kuitumikia nchi yangu
katika nafasi ya Naibu Waziri (2010 - 2015) na Waziri (2015 hadi 2024). Si kwa uwezo au ujanja wangu bali ni kwa ukuu wa Mungu.
Pili, kwa heshma na unyenyekevu mkubwa
ninamshukuru Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini na kunipa heshma ya kuhudumu kwenye Serikali yake katika nafasi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi (March 2021 - January 2022) na Waziri wa Afya (January 2022 hadi 14 Agosti 2024). Asante sana Mhe Rais kwa imani na heshma kubwa uliyonipatia. Nitaienzi na kuitunza heshma hii daima.
Kwa muda niliohudumu katika Wizara ya Afya nimeiona Ari, Juhudi na Kiu ya Rais Samia ya kuwaboreshea watanzania huduma za afya. Tumetoa
mchango wetu katika hili.
Yapo mengi
tumeyasukuma na ambayo yanaendelea kusukumwa.
Pongezi za dhati kwa dada yangu, Mhe Jenister Mhagama kwa kupokea kijiti. Sina shaka na uwezo, uzoefu na kujituma kwake ktk kufikia malengo
tuliyojiwekea pamoja na Maono ya Mh Rais ya
kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watanzania. Namtakia heri katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.
Tatu; Ninawashukuru Viongozi na Watumishi wa Wizara ya Afya, Wadau wa maendeleo, CSOs kwa ushirikiano mzuri walionipatia ambao umewezesha.”

Пікірлер: 17
@Jammie626
@Jammie626 25 күн бұрын
Achana na Roho mbaya ya kuwakosesha wananchi huduma za afya na kuwapelekea wananchi wengine kupokwa haki zao za msingi za kuwalipia watoto wao Bima ya Afya.Mfano Baba wa miaka 60 ambaye ana mtoto wa chini ya miaka 18 hawezi kumkatia Bima ya Afya,kwa masharti na vifurushi vya NHIF ,bali akakatiwe shuleni kwake.Shuleni unaambiwa hadi watoto 100 watimie. Sasa mtoto huyo kwanza hawezi kusubiri mchakato huo endapo ataugua.Pili mfano halisi ni kwamba Mama wa mtoto huyo ni marehemu,na Baba ni mstaafu na katimikia Serikali na taasisi zake zaidi ya miaka 37.Huyo waziri badala hata kuweka sera nzuri za Bima ya watoto kama alivyofanya JPM ya toto Afya,Waziri Ummy akawakinara wa mbele wa kuondoa.This is not fair at all.Ngoja na wewe ukae pembeni uone ugumu wa maisha.Kila lakheri.
@alhajiakida9703
@alhajiakida9703 24 күн бұрын
Mh Ummy Mwalimu, binafsi wewe ni mmoja ya wachapa kazi ktk Serikali hii na awamu zote ulizotumika, uwezo wako ni mkubwa na bado nafasi yako kitendaji ipo. Ni mategemeo yangu kukuona tena siku zijazo. Hongera sana kwa utumishi wako katika Taifa hili. Mwenyezi Mungu akuongoze. Amiin Amiin.
@mohamedally6992
@mohamedally6992 23 күн бұрын
ASALAM ALAYKUM . UCJAL KUWA NA AMAN UMEJITAID KIUPANDE WAKO . UKIWA KIONGOZ U C TEGEME KUPENDWA NA WOTE . KUWA NA AMAN . NINA IMAN MAMBO MZURI YANAKUJA KWAKO KUTOKA KWA MUHISHIMIWA RAIS. SOON UTAIBUKA TENA .INSHALAAH
@OswardMadege-gd7yo
@OswardMadege-gd7yo 25 күн бұрын
Hongera ummy mwalimu umejitahidi sama hasa kipindi cha covid ubarikiwe sana
@yunusimchala6569
@yunusimchala6569 25 күн бұрын
Fedhaa za NHIF ZIMEKUTOA HAPO UMECHEZEA SANA AFYA YA WANANCHI
@EsupatLaiser
@EsupatLaiser 23 күн бұрын
Amefata maagizo
@lisawilliam2491
@lisawilliam2491 25 күн бұрын
Nice worlds
@godfreylyimo4177
@godfreylyimo4177 25 күн бұрын
Umefanya kazi nzuri kwa sehemu yako!! Ni heshima kubwa kwa umri wako kutumika ktk nafasi hizo.
@josephjamesdagharo
@josephjamesdagharo 23 күн бұрын
Hongera kubali matokeo ulikuwa ktk nafasi Bora kama mama ila hukuwajali watoto kula keki ya taifa kwa faa kugawana
@MichaelKingazi-wm7xj
@MichaelKingazi-wm7xj 25 күн бұрын
Congratulations be happy full this is just a normal life.
@hamidabarraball3162
@hamidabarraball3162 25 күн бұрын
Kwahiyo unataka tukuhurumie? Wakati raia wanateseka na magonjwa wanakufa kwa kukosea uwezo wa kulipia matibabu ulikua hujali
@jamesmgendi9418
@jamesmgendi9418 23 күн бұрын
Nimependa unyenyekevu wako Mh. Ummy Mwalimu
@KapamaSaleh
@KapamaSaleh 20 күн бұрын
Apumzike kidogo hospitali zatanga hazina mashiko iyo bombo mmh poleyangu aiseeh
@andreapesambili7981
@andreapesambili7981 25 күн бұрын
kisaikolojia,hapa unaonekana unalalamika kuachwa,hakuna kingine,ulikula kuku kwa mrija subiri uchaguzi,ndo utakuima tena kama unafaa kurudi bima ilikuwa ni changamoto kubwa kwani wewe hukuona?
@DominicaShio
@DominicaShio 23 күн бұрын
Wazazi wanazaa kwa kulipia Kila siku halafu unasema kuzaa Bure Samia jembe bana Wala hajakisea Samia hoyeeeee
@abuuramadhan8093
@abuuramadhan8093 25 күн бұрын
Hapo kabaki kutafutwa aweso
@DavidSemu-gu6wp
@DavidSemu-gu6wp 25 күн бұрын
Ala! Ikiwa na maana Watanga ndio Wana nyofolewa mmoja mmoja? Duh! Kuna mahali niliona mji fulani ikaelezwa viwanda vyote vilivyo kufa vitarejeshwa kwani ulikuwa WA pili baada ya DAR ili Hali Kwa ukakika WA pili ulikuwa mji wa Wagosi hata Kwa maendeleo, nikikumbuka kiwanda cha mbolea,Amboni crates, viwanda vya sabuni mbuni Foma, Gardenia, Hamam, dawa za Meno Tara, na vinginevyo Ila Sawa Tu yote NI Tanzania
Electric Flying Bird with Hanging Wire Automatic for Ceiling Parrot
00:15
English or Spanish 🤣
00:16
GL Show
Рет қаралды 17 МЛН
나랑 아빠가 아이스크림 먹을 때
00:15
진영민yeongmin
Рет қаралды 16 МЛН
Modus males sekolah
00:14
fitrop
Рет қаралды 14 МЛН
TAJIRI WA MABUS  SUPER FEO ATOA SIRI YA KUWA BILIONEA
10:36
Wasafi Media
Рет қаралды 114 М.
DKT. JANABI KAPIGA TENA, WAPENDA SODA WAFIKIWA, AWAONYA !!
4:15
Wasafi Media
Рет қаралды 14 М.
Kinachoendelea msiba wa Askofu Sendoro, kuzikwa Septemba 17
5:04
Mwananchi Digital
Рет қаралды 6 М.
Electric Flying Bird with Hanging Wire Automatic for Ceiling Parrot
00:15