Hoja ya utekaji yaibuka tena bungeni, Spika Tulia, Waziri Mkuu wabanwa kutoa maelezo

  Рет қаралды 117,532

Mwananchi Digital

Mwananchi Digital

Күн бұрын

Hoja ya utekaji, mauaji na kupotea kwa watu ikiwemo watoto imeibuka tena bungeni baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest kutaka mkakati wa Serikali kukomesha matukio hayo aliyodai baadhi yanahusishwa na vyombo vya dola.
Leo Alhamisi, Agosti 29, 2024, hoja hiyo imeibuka bungeni wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, baada ya Anatropia kusema matukio ya utekaji, mauaji na kupotea kwa watu yanaashiria uvunjifu wa haki za binadamu.
Amesema matukio hayo yamekuwa na sura tofauti tofauti ikiwemo wivu wa mapenzi na ushirikina.
“Lakini na matukio mengine ya kutekwa na kupotea kwa watu yanahusishwa na vyombo vya dola. Nataka kufahamu mkakati wa Serikali kuzuia matendo haya lakini kuondoa taharuki ambayo inajitokeza katika jamii,” amesema.
Hata hivyo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kabla ya kumpa nafasi Majaliwa kulijibu swali hilo, amesema juzi Jumanne Agosti 27, 2024 alisimama Mbunge wa Nkasi Kaskazini (Chadema), Aida Khenani akazungumzia suala hilo.
Amesema mambo hayo yanayohitaji uchunguzi:“Leo asubuhi nimesoma kuna mganga amezika watu sijui 10 na ngapi, sasa huyu mganga ni polisi ambaye watu ameuawa na wamezikwa kwake.”
Amesema mambo hayo yakiwa yanasemwa kwa hisia hivyo inakuwa kama mtu hajali wakati kila mtu anajali na kila binadamu ana haki ya kuishi.
“Lakini tusiweke mazingira kwamba kila anayepotea…si kuna mabasi wanapanda kule chini, akidondoka huko chini si nyumbani wanamtafuta utasema ni chombo cha dola kimemchukua.Sisi lazima tuifanye hii kazi kama viongozi ukichukua mihemko hutoi nafasi kwa Serikali kufanya kazi yake wakati huo huo hutoi nafasi kwa jamii kuendelea kushiriki katika jambo,” amesema.
Amesema wao wote ni viongozi na wangependa wananchi wao wawe salama na kuonya mambo hayo yasichukuliwe jumla jumla.
“Na wewe chukua nafasi ya uongozi, unaweza kutoa ushauri lakini usinyooshe vidole kwa sababu huna hakika. Na wengine wanahama nchi si tunakamata hapa kila siku, na wenyewe huko kwao wanatafutwa watasema chombo cha dola kimewachukua kimewapeleka sijui wapi,” amesema.
Amesema huku kwao wanawatafuta wahamiaji hao waliokamatwa nchini lakini kumbe alipofika hapa Tanzania mazingira yamekuwa magumu na hivyo amekamatwa.
Baada ya maelezo hayo ya Spika Tulia, amempa nafasi Waziri Mkuu Majaliwa kueleza akisema jukumu la kulinda nchi ni wajibu wa Watanzania wote kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.
“Tunavyo vyombo vya ulinzi na usalama vyenye jukumu la kupokea taarifa mbalimbali zinazoonyesha uvunjifu wa amani popote pale kwenye meza ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Jukumu lao baada ya kupokea taarifa ni kuhakikisha wanafanya uchunguzi,” amesema.
Majaliwa amesema uchunguzi unapobaini waliotenda makosa, wanawapeleka katika vyombo vya sheria.
Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kujikita kusimamia misingi ya amani katika nchi yetu na usalama kwa kuhakikisha raia na mali zao zinabaki salama.
Amewahakikishia Watanzania kwamba suala la ulinzi na usalama bado liko mikononi mwao pamoja na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
“Jukumu letu ni kuhakikisha tunasaidia vyombo vya ulinzi kwa kutoa taarifa zozote zile ambazo zinaleta tishio la amani ili kuvisaidia vyombo vyetu viweze kuchukua tahadhari na hatua stahiki ili kubaini watu wote wanaotishia kutokuwepo kwa amani katika nchi yetu,” amesema.
Majaliwa amesema lakini pia vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea na wajibu wao wa kuhakikisha kila taarifa inayopatikana lazima ifanyiwe uchunguzi na kubaini wale wote wanaohusika na kama wanapatikana wachukuliwe hatua mara moja.
Amemshukuru Spika kwa maelezo yake ya awali ili kuondoa upotoshaji ambao unaweza kuwa unaendelea na kufanya vyombo vyao vishindwe kufanya kazi yake na kuwavunja moyo watu wanaofanya kazi saa 24 kwa ajili ya ulinzi ambao unawafanya wabaki salama.
MaRC na DC tena bungeni
Katika swali jingine, Mbunge Viti Maalumu, Stella Fiyao amesema nchi inaamini katika uongozi wa kisheria na utawala bora ili kujengwa umoja mshikamano na upendo baina ya wananchi na viongozi wao.
Amesema hata hivyo kumekuwa na changamoto kubwa baina ya baadhi ya wateule wa Rais, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kwa kutumia nguvu na mamlaka yao vibaya kukamata viongozi na wananchi na kisha kuwatupa ndani.
“Moja jambo hili limetengeneza chuki kubwa baina ya wananchi na Serikali yao lakini linafifisha jitihada kubwa za mheshimiwa Rais za kuhubiri 4R na mwisho wa siku jambo hili linakuwa halileti mantiki,” amesema.
Ametaka kujua kauli ya Serikali ni ipi katika kukemea jambo hilo ambalo linatengeneza chuki kubwa baina ya Watanzania na Serikali yao.
“Kauli ya Serikali ni ipi kwa hawa viongozi wanaotumia mamlaka yao kutesa na kunyanyasa wananchi,” amehoji.
Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema swali hilo ni linafanana na alilolisema jana Jumatano Mbunge wa Mlimba (CCM), Godwin Kunambi ambapo Dk Tulia aliwapa kazi Serikali kulifanyia kazi.

Пікірлер: 781
@ShannyBrowntz
@ShannyBrowntz Ай бұрын
Mungu amlinde Hibrahm TRAOLEEE,,Taa ya Africa,,
@rukundorwiza5223
@rukundorwiza5223 Ай бұрын
Na uku tanzania hamuwezi kumpata mtu kama traole 😢😢jeshi lenu vibaraka viya merikani😢😢😢
@jamesrobare522
@jamesrobare522 2 ай бұрын
Huyu mwanamke tulia ni janga la taifa lazima watanzania tuwe waangalifu na matendo yake ya kubomoa
@Aziz-p6s
@Aziz-p6s Ай бұрын
Uchaguzi huu mbeya hapiti labda agawe jimbo mbeya wanaakili
@hajihassan5433
@hajihassan5433 Ай бұрын
​@@Aziz-p6s Ni Mbunge wa Mabunge duniani.
@KandoreHamic-yy6cl
@KandoreHamic-yy6cl Ай бұрын
Yaaani huyu mwanamke analoho mbaya sANAAA
@allyunique2491
@allyunique2491 Ай бұрын
wewe ndo umeulizwa au una jua hayo matukio
@marryfelician1426
@marryfelician1426 Ай бұрын
Kwa kweli dah kuna watu wakiongea unaona kabisa haiwagusi
@abednego3876
@abednego3876 2 ай бұрын
Tunaspika mpumbavu sana shenziii kbs.. Na hao wanaopiga meza ni mbwa.
@amanmalima940
@amanmalima940 Ай бұрын
Yesu Ndiye njia ya kweli na uzima ya kwenda mbinguni hebu MWAMINI Yesu na UOKOKE na ulithi uzima WA MILELE na uende mbinguni.(Yohana14:6, Warumi10:9-10).
@mtakwaelius1094
@mtakwaelius1094 2 ай бұрын
Ipo siku Mungu wetu atashusha kiburi hicho
@SauliBasso
@SauliBasso 2 ай бұрын
Huyu spika ni nyoko sana ila mwisho wa siku naye atakufa tu
@bernadetamushi
@bernadetamushi Ай бұрын
Mnauwa sana watu nyiyi muogopeni Mungu msijitetee kabisa. Mungu anawaona
@davidsimbeye1548
@davidsimbeye1548 2 ай бұрын
Muuliza amefafanua vizuri kwamba matukio ya utekaji yanahusishwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na wivu wa mapenzi, imani za kishirikina na mwishoni amehusisha vyombo vya dola, lkn naona majibu ya spika yamelekezwa kwenye eneo moja tu la vyombo vya dola
@champion-dz6kr
@champion-dz6kr 2 ай бұрын
Yani ndugu ww mwelevu sana , muulizani katofautisha, ila spearker amna kitu kwa kichwa
@LameckNyamsenda
@LameckNyamsenda Ай бұрын
Tulia wewe, tuliatu
@happyfiverickaldo4662
@happyfiverickaldo4662 Ай бұрын
Mimi nafikiri tulia ndio anamhemko ila muliza naona yupo viziri na apite pale makole ale kilaji nakuja kulipa
@YacintaJames
@YacintaJames Ай бұрын
Hapo hatuna Spika, na yeye anajibu kwa mhemuko
@RaymondKilomeye
@RaymondKilomeye Ай бұрын
Upo sahihi ila hii ninjama zakulindana wenyew
@GraceKazi-z8d
@GraceKazi-z8d Ай бұрын
Kwahyo na ww Tulia ukaamua ujibu kwa muhemko!? Ila Daaaaa! Inauma sana 😢
@hajihassan5433
@hajihassan5433 Ай бұрын
Hiyo issue ipo kwenye uchunguzi sio busara sana kulizungumza kisiasa.
@godfuture-t8y
@godfuture-t8y 2 ай бұрын
Mnakera sana ccm
@pauljulius4744
@pauljulius4744 2 ай бұрын
Spika anasema watu wasiwe na mihemuko kwenye maisha ya watu
@amanimlengwa9202
@amanimlengwa9202 Ай бұрын
Vyombo vya ulinzi na usalama hivyo vinavyo wateka na kuwaua watu ndo tunavyotakiwa kuendelea kuviamini? Halafu huyu ndo spika wa mabunge duniani kweli?
@RobatAllaya
@RobatAllaya Ай бұрын
Duh mungu isaidie Tanzania tumeisha
@MbwanaKivava
@MbwanaKivava Ай бұрын
Spika ana mjibia waziri mkuu 😊
@fredrickbaryagati2194
@fredrickbaryagati2194 2 ай бұрын
Yatakugarimu mbeya kwa uchaguzi .sote ni wazazi mungu atajibu tuombe
@MaryMwamwezi-xm3iz
@MaryMwamwezi-xm3iz 2 ай бұрын
Kila sekta inakazi yake. Wapo wanaotakiwa wachunguze. Tuache lawama. Wote tumeumia. Siyo wewe tu. Hakuna anayependa haya matukio.
@westserengeti5608
@westserengeti5608 Ай бұрын
​@@MaryMwamwezi-xm3izLikiwa kwenye sekta, serikali haitakiwi kuulizwa?, ila Tulia Mungu anakuona
@ElneySheddy-is1dv
@ElneySheddy-is1dv Ай бұрын
Turia nimavi kichwani
@AnnaMwanakatwe
@AnnaMwanakatwe Ай бұрын
Umekosea Sana uko upande mmoja. Hayo si majibu ungesema tultalifanyia kazi
@mbegesemwalupani6460
@mbegesemwalupani6460 Ай бұрын
Duh! tulia kweli?
@MwanduMachiya
@MwanduMachiya 2 ай бұрын
Mungu yupo anajisikia jibu lako utalikumbuka
@ibrahimuizack8244
@ibrahimuizack8244 Ай бұрын
Viongozi mtateseka sana kwa marazi kwahaya mungu yupo kwa malipo yenu
@GraceMalley-ly2xn
@GraceMalley-ly2xn Ай бұрын
Tumeumbwa kwa sura na mfano Wa Mungu tambua unapo mtesa mwanadamu unamtesa Mungu tambua ww dada
@adelphinusbikonya8534
@adelphinusbikonya8534 Ай бұрын
Mkono wa Mungu utashughulika na wasio haki
@ariibahati3414
@ariibahati3414 2 ай бұрын
Yaani hata mganga wa kienyeji ana haki ya kuua au kuteka watu bila kuulizwa na serikali??? Ohh Tanganyika yangu.... Una kila kitu lakini uongozi wetu unatufanya tuishi kwa mashaka makubwa. Mungu unatuona watanganyika usituache na uzao wetu tukaangamia. Kumbuka kazi za mikono yako EE Mungu usiyefichwa na chochote. Unayaona yote yaliyo mioyoni mws viongozi uliowaruhusu waongoze kwa kipindi chote hiki.
@lusakaone7782
@lusakaone7782 2 ай бұрын
Wasiwasi wangu hapa Kuna kijambo miongoni mwa wanaotuongoza kwa kweli, majibu ya Spika simuelewi.
@AishaOman-k6f
@AishaOman-k6f 2 ай бұрын
Spika.anaroho.mbaya.nandio.mana.anajibu Anavyojisikia.
@verdianabanabi2205
@verdianabanabi2205 2 ай бұрын
Uumeona ehh huyu spika hajfikwa na ndiyo maana anajubu atakavyo
@SADICKITHOMAS
@SADICKITHOMAS 2 ай бұрын
Uongozi ni dhamana na busara muhimu sana ,,kiburi sio afya kwa nchi yenye amani utulivu
@ephraimkalanje7105
@ephraimkalanje7105 2 ай бұрын
Naye Spika ana maelezo ya kimhemuko na kuashiria ukiburi fulani hivi! Hivi hawa waliopotea mathalani akina Azori Gwanda, Ben Saanane, akina Soka...walidandia mabasi kule chini kwenye chasis na wakaanguka na kufa na ndo kimekuwa chanzo chao cha kupotea? Au wame-stoaway na wapo katika nchi fulani za ughaibuni? Duuuh! Maelezo ya Spika ni maelezo ya ujumla mno na kimhemko pia! Serkali isifunike kombe mwanaharamu apite katika hoja hii. Uchunguzi wa kina ufanyike na vyombo huru ili kubaini watu halisi walio nyuma ya kupotea kwa watu!
@EmiliKigoma
@EmiliKigoma 2 ай бұрын
Mungu Anglia ushetan
@EliaPundugu
@EliaPundugu Ай бұрын
Huyo mama hayuko sawa
@JoctanMufungo
@JoctanMufungo 2 ай бұрын
Sasa hapa spika anajibu au analalamika!
@kefamwakipesile275
@kefamwakipesile275 2 ай бұрын
Mimi ni ccm lakin kuna kiasira kinapanda kufuani mwangu, Mpak nawish ningekuwa jetriii
@prijoseph4665
@prijoseph4665 Ай бұрын
😂😂😅😅😢😢 Nacheka ila naumia sana
@kefamwakipesile275
@kefamwakipesile275 Ай бұрын
Kabisa kaka
@RoseMartine-u2z
@RoseMartine-u2z Ай бұрын
😂😂😂😂 nacheka kama mazur
@msafirindalu122
@msafirindalu122 2 ай бұрын
Maisha ya watu yanafanyiwa siasa mungu anawaona
@josephudoba5563
@josephudoba5563 2 ай бұрын
Kazi kwelikweli
@fadhilimsafiri216
@fadhilimsafiri216 2 ай бұрын
Hatari sana, bungeni hakuna kitu.
@marthadaniel4904
@marthadaniel4904 Ай бұрын
Hakun ziro mwanamke anaongea sipo kweli
@alfanikingwan7174
@alfanikingwan7174 2 ай бұрын
Mbona huyo spiker anahalalisha watu kufa kwa kutekwa na kuona sawa tu,, hivi dini iko moyoni kwako kweli sio sawa please 😊
@muksinimbaruku1233
@muksinimbaruku1233 2 ай бұрын
Ukristo sio dini
@LwingaOsiah
@LwingaOsiah Ай бұрын
​@@muksinimbaruku1233Usiusemee ukristo,isemee dini yako,kama huna dini basi kausemee upagani wako.
@StellahMaulid
@StellahMaulid Ай бұрын
Mpuuzi wew haswa Kama ukristo Sio Dini uo uislamu ambayo ndo Dini mbona ndo mwaongoza katika matukio machafuu Na ubinafsi au Dini yenu ndo imehalalisha Hilo acheni udini ujinga t Na umasikini Wa kukosa fikla​@@muksinimbaruku1233
@hildamkongwa2156
@hildamkongwa2156 Ай бұрын
Ange tekwa mtoto wake ndo Ange jua kua Ni mihemko uyu mama au Ange uwawa
@AthumaniPembe
@AthumaniPembe Ай бұрын
Tunamuomba mungu atulinde sisi viumbe wake maana hatuna ulinzi
@Michaelmollel-bv7qw
@Michaelmollel-bv7qw Ай бұрын
Nyie tunawajua sana.
@HamisMghuna-fj3vz
@HamisMghuna-fj3vz Ай бұрын
La utekaji bungeni n zero, Allah, atusaidie wafe kw Ajali,
@calsenciaLeonard
@calsenciaLeonard Ай бұрын
Aise mungu atajibu hivi punde
@ShabaniMchengia
@ShabaniMchengia Ай бұрын
Ipo siku mungu atakasilika 2 maana ii Hali sio pw
@lamecklainson5989
@lamecklainson5989 2 ай бұрын
Mungu tu ndie mrizi siyo hao makafiri
@antonymomba8185
@antonymomba8185 Ай бұрын
Kimeumana kazi iedelee
@barnaba3037
@barnaba3037 2 ай бұрын
Spika kakasirika kisa kuuliza tena kwa msisitizo kuhusu watu kupotea😂😂
@EBENEZERSikambale
@EBENEZERSikambale Ай бұрын
Watanzania Mungu aketupa manabii na wamesema yanayo kuja nashauri sio wakati sahihi wa kulalamika bali kuomba Omba usichoke kwa ajili ya inchi yako
@SpckLeopord
@SpckLeopord Ай бұрын
Mungu anashuudia yote haya atajib kwa wakat wake
@bernadetamushi
@bernadetamushi Ай бұрын
Kwanini sikunzote wasitekwe ni sasa. Mnajibu very simple
@michaelmagwaza-bc6mk
@michaelmagwaza-bc6mk 2 ай бұрын
Inauma sana kwamajibu haya ya kejeri
@muhammadkhamis5798
@muhammadkhamis5798 2 ай бұрын
Mmmh npo hapa namsubiria ROMA
@TeddyMhando-c6j
@TeddyMhando-c6j Ай бұрын
Aisee tumuogope mungu kwa hii hali L
@ShafiiSaid-v5n
@ShafiiSaid-v5n Ай бұрын
Vijana wenzangu Harakati isikua &vitu 3 1,uchumi 2, Elimu 2 ,nguvu Achaneni nayo hapo Unafiki tyu, Unangia barabani Mwenzk akiona kimenuka Nje' ya nchi we unavunjwa Miguu ujing huo,si? Fanyi, Tumuombe m/mungu Atuongoze kwa amani tz,
@ShabaniMchengia
@ShabaniMchengia Ай бұрын
Yaani ebu mungu tusaidia maana t
@StevenNyanguye
@StevenNyanguye Ай бұрын
Huyu dada Mungu anamuona kwa kweli
@hilarymaulid1903
@hilarymaulid1903 2 ай бұрын
Juzi??? Duh!!
@safaribuganga
@safaribuganga 2 ай бұрын
Tunamwachia Mungu
@tonotvonline3070
@tonotvonline3070 2 ай бұрын
...Wazirii Kabalansii Maneno Lakini sipika wew Kwasabab Huna kichaa Nyumban kwak Unaonaa Sawaa Tu achaa yakutokee
@lovenesdickson1824
@lovenesdickson1824 Ай бұрын
Mungu tutetee
@MikaNyalusi
@MikaNyalusi Ай бұрын
Hatariiiiii
@MeshackLukanda
@MeshackLukanda Ай бұрын
sawa,,mtanipa na mm Nchi Basi nijaribu maana naona mnakwepa kazi yenu naishi mwanza sengerema,,
@happykomba4456
@happykomba4456 Ай бұрын
Umenifuraisha utapata tu nchi ya kuongoza
@BONIFACEDOMINICK-j8l
@BONIFACEDOMINICK-j8l Ай бұрын
Wanachi hatuna haki sasa......
@godfreylyimo4177
@godfreylyimo4177 2 ай бұрын
Mh Spika ni vema ukatenganisha Bunge na Serikali....Ukweli Bunge lina kazi kubwa kwenye kuisimamia serikali yetu...
@faustinedeogratias4337
@faustinedeogratias4337 2 ай бұрын
Inabiti tuanze kuwateka na wao...
@josephjulio6112
@josephjulio6112 2 ай бұрын
Mpaka atekwe waziri ndio mtajibu maswali
@happyfiverickaldo4662
@happyfiverickaldo4662 Ай бұрын
😂😂😂😁😁😁😁😁
@tumlakimwaitumule
@tumlakimwaitumule 2 ай бұрын
Mbona mbunge kasema wazi ,Haja generalize Mambo
@ElizabethPriva
@ElizabethPriva Ай бұрын
Mungu ilinde Tanzania
@msafirially7849
@msafirially7849 Ай бұрын
Sawasawa Muheshimiwa
@BakryMkumbukwa
@BakryMkumbukwa Ай бұрын
Kweli
@SDM2024-z4s
@SDM2024-z4s 2 ай бұрын
Madam Boss umeelezea vizuri sana,
@jitabojilala6162
@jitabojilala6162 2 ай бұрын
Hufai kuwa kiongozi
@RajabuJuma-eu4xs
@RajabuJuma-eu4xs Ай бұрын
Mungu nakuomba viongozi Hawa uwatie hadabu wote Anza na tulia
@isayamwashibanda5819
@isayamwashibanda5819 2 ай бұрын
😭😭😭 MUNGU ikumbuke Tanzania
@GeraldMyuku
@GeraldMyuku 2 ай бұрын
Amen
@peacejunne5037
@peacejunne5037 Ай бұрын
ndugu zanguni mungu huyu tulieachiwa na wakoroni nasema tena na tena hawezi kua sehem ya kumaliza matatizo ya Afrika tuamke watu weus ili kuupata mwangaza wetu uliozimwa hapo kitambo sana, vinginevyo juu ya huyu mungu wa kanisa na msikiti mmmmh ah ahhh bado sana
@AlHamra-ej3mo
@AlHamra-ej3mo Ай бұрын
Huyu mwanamke abadharau sana wallah
@danieliwilsongurty
@danieliwilsongurty 17 күн бұрын
Mmm tunaambiwa mihemko ila haina shida
@gwantwamwalyaje8515
@gwantwamwalyaje8515 2 ай бұрын
Mm Naomba Tusicheze Na Maisha Ya Watu
@mbwanarajab7238
@mbwanarajab7238 2 ай бұрын
Kiukweli watanzania wa chini tuna changamoto kubwa sana Sijui kwamba tunajitambua vizur
@laiserkuyan6075
@laiserkuyan6075 2 ай бұрын
Mungu Nuzuru taifa letu hatuna serikali kila mkoa na vijijini watoto wetu wananyokwa kutolewa kafara mama wakambo na vyompo via dollar ikivupia macho
@RehemaMtemvu
@RehemaMtemvu 2 ай бұрын
Mungu wangu acha wale bata ata na sisi ni watu mungu alituumba kama wao ila kaburini kuna kazi
@hezekianaamo
@hezekianaamo Ай бұрын
Tulia umechemka sana Bora ungenyamaza kuliko hivyo
@Abs-tz8dl
@Abs-tz8dl Ай бұрын
Adui wa tanzania
@Frank-b2d6u
@Frank-b2d6u Ай бұрын
Wewe mwanamke muogope mungu haya mambo niendelevu tunaona hututendei haki hicho kicheo kama kina kupa wokovu nakukuingiza peponi sawa kama nitaratibu zakibinanam na zakimaisha kwa ujumla wenu watu kama nninyi hama utofauti na hao watekaji watu wanapigwa na hao polisi wenu harafu unajibu kirahisi hivi kama mwanamke usiezaa hatari sana
@psttitonakazaelimjema.9562
@psttitonakazaelimjema.9562 2 ай бұрын
Anaonge kamaatakavyo kwa sababu familia yake ipo salama.
@IssaMsalama-k6x
@IssaMsalama-k6x 2 ай бұрын
Hanauwakika familia yake aitahingia ktk majanga hayo,
@evansthobias6460
@evansthobias6460 Ай бұрын
Ingekuwa kwa watoto wao mh
@MikaNyalusi
@MikaNyalusi Ай бұрын
Balaaaa
@hamidumpiga6283
@hamidumpiga6283 Ай бұрын
Uka sawa spika
@salimumpimbi563
@salimumpimbi563 Ай бұрын
Hili speaker VIP mamae
@MtafyaHabari
@MtafyaHabari 2 ай бұрын
Humu hamna kitu
@justcruised
@justcruised Ай бұрын
Tulia ni ex usalama we taifa she is trained kuua revolution movement in Tanzania
@ClayMwitula
@ClayMwitula Ай бұрын
Amesema mauaji ya aina tofauti
@mberaemmanuel9091
@mberaemmanuel9091 Ай бұрын
Kila jambo lina mwesho wake mungu atupe hekima yake mwenyewe
@nitisilemwabenga2864
@nitisilemwabenga2864 Ай бұрын
sawa kwa sasa niwakati wenu
@ThomasMsumule
@ThomasMsumule Ай бұрын
Duuu hatarii Sana jaman
@KandoreHamic-yy6cl
@KandoreHamic-yy6cl Ай бұрын
Selikali ya ccm inatuchangany sana
@antoinekatembo8520
@antoinekatembo8520 2 ай бұрын
Madam speaker, YOU SHOULD NOT DEFEND THE GOVERNMENT, acha serikali ijibu… hapo ndipo kunapo kuwa tofauti wa mataifa ya magharib na barani kwetu Afrika!! His excellency Majaliwa, is one of the dude that I always respect tangu nikiwa mdogp na until kesho bado nitazidi kumueshimu tuu. Embu sikilizieni kwa umakini majibu yake. A decent quality one but also reputable leader!!
@AbdalaKambona-bw6zm
@AbdalaKambona-bw6zm Ай бұрын
Ww ni spika wa Tanzania au wa zanzibar
@ayshasaid1547
@ayshasaid1547 Ай бұрын
Muongo majariwa na tulia muogopeni mungu nadhani ingekua familia yake jasho lingekutoka
@AbdulBushir
@AbdulBushir Ай бұрын
Mbona swali limejibiwa na spika wa bunge? Alafu mtoa swali alifafanua vizur tu,,,kweli nchi inaelekea kuzimu mungu tulinde
@HamisiSella
@HamisiSella Ай бұрын
Aya makubwa jinga yote
@ipepeetube449
@ipepeetube449 2 ай бұрын
Tuwe na bunge la wananchi tofauti na bunge la tulia badala ya kusaidia ndio anapiga msumari
@CharlesMarigory
@CharlesMarigory Ай бұрын
Inauma sana kwa watanzania wenzetu kutekwa iwe kwa kishirikina au iwe kwa wivu wa mapenzi au iwe utekelezaji wa dola tunachotaka haki kwa watanzania tu serikali ifanye kazi yake na sio idara zingine zisizo julikana
@ezekielmadindula2679
@ezekielmadindula2679 Ай бұрын
Bogasi spika😊
@chidampiri1012
@chidampiri1012 2 ай бұрын
Huyu mama.......?
@LoiteyoAmakoMako
@LoiteyoAmakoMako 2 ай бұрын
Hatuwaeliwi
@ilovemiginamygodblessumany2466
@ilovemiginamygodblessumany2466 2 ай бұрын
Spika unakosea sana hujapotelewa ndugu wa damu au jamaa wa karibu mm ni ccm lakn hapo umejibu tofauti kabisa na jinsi swalii liloulza
@ezrarafael1249
@ezrarafael1249 Ай бұрын
Achana na ccm ndgu yang ni Bora ukaishi bila chama kuliko kuwaunga mkono hawawatu hujui tu kama wao Ndy chanzo Cha maisha yetu mabovu miaka 60 ya huru wao wanaishi kama wako peponi mpigakura wao kama yuko jehanam
@dastanifreck1009
@dastanifreck1009 Ай бұрын
Tutambue kua sote tutakufa hivi vyeo visitupe kiburi kiukweli inaumiza sana spka anajibu maneno kama haya Mungu atatoa majibu yamaswali yetu tuendeleeni kumuomba Mungu
@ImanNjogolo
@ImanNjogolo Ай бұрын
Wanataka pesa tu hao..hakuna uongozi wala utatuzi hapo.wehu tu.chi.acheni kama hamuwezi mmejaza vitambi tu..
@BenedictoTegezya-se8lc
@BenedictoTegezya-se8lc 2 ай бұрын
Hii nchi ina watu wapu uz sana
@KilianEmanuel
@KilianEmanuel Ай бұрын
Acha siasa.dada jibu swari ulilo ulizwa
@Uhuru-s8c
@Uhuru-s8c 2 ай бұрын
Bora hata Ndugai mmmh
@christineaimtonga9872
@christineaimtonga9872 2 ай бұрын
Uchunguzi mpaka lini?
MBOWE AMBANA WAZIRI MKUU BUNGENI - "UNANIPA MAJIBU MEPESI SANA"
11:04
Global TV Online
Рет қаралды 146 М.
Family Love #funny #sigma
00:16
CRAZY GREAPA
Рет қаралды 17 МЛН
Kluster Duo #настольныеигры #boardgames #игры #games #настолки #настольные_игры
00:47
REAL 3D brush can draw grass Life Hack #shorts #lifehacks
00:42
MrMaximus
Рет қаралды 12 МЛН
Friends make memories together part 2  | Trà Đặng #short #bestfriend #bff #tiktok
00:18
USIMCHUKIE MTU AMBAYE HUJAKOSANA NAYE!
0:10
Asali Mubashara
Рет қаралды 9
MBUNGE WA MBULU VIJIJINI ARUKA SARAKASI BUNGENI, AKIDAI BUNGENI.
10:48
The Day Ronaldinho Became a Brazilian Legend
12:50
VSP7 FOOTBALL
Рет қаралды 3 МЛН
SALIM KIKEKE NDIO  MMILIKI WA CROWN FM
18:28
Dizzim Online
Рет қаралды 166 М.
JOSEPH MBILINYI USO KWA USO NA TULIA WAPEANA MAKAVU LIVE MBEYA PACHIMBIKA
19:56
Family Love #funny #sigma
00:16
CRAZY GREAPA
Рет қаралды 17 МЛН