Рет қаралды 251
Taasisi ya chanjo Tanzania (TVLI) Kibaha ilipewa jukumu la kuhakikisha magonjwa 13 ya mifugo yaliyopewa kipaumbele nchini yanadhibitiwa, kutokana na hiloTVLI iliyo chini ya Wakala wa Veterinari Tanzania (TVLA) ilipata ufadhili kutoka Serikalini kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wa kujenga maabara ya kudhibiti ubora wa chanjo.
Uwepo wa maabara hii umechangia kuongezeka kwa uzalishaji wa chanjo kutoka aina tatu (3) zilizokuwa zinazalishwa kabla ya maabara hii mpaka kufikia aina sita (6) ambazo ni chanjo ya: Mdondo wa kuku, Kimeta, Chambavu, Homa ya mapafu ya Ng’ombe, Mchanganyiko (Kimeta na Chambavu) pamoja na Ugonjwa wa kutupa mimba kwa ng’ombe.
@elimudigitalmedia @millardayoTZA