Рет қаралды 2,464,016
MAJAMBAZI 3 WAUAWA GOBA WAKIRUSHIANA RISASI NA POLISI
Majambazi watatu wamefariki kufuatia majibizano ya risasi baina ya askari wa Jeshi la Polisi wakati wakidhibitiwa dhidi ya jaribio la uvamizi katika duka la Skymart lililopo Goba, Tegeta A, Wilaya ya Kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda ya Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro amesema majambazi hao walikuwa wanne wakiwa na bunduki mbili zenye jumla ya risasi 17 pamoja na pikipiki, ambapo askari polisi waliwakuta wakiwa kwenye hatua za mwisho kufanya ujambazi.
Amesema katika tukio hilo, askari mwenye namba F3625 Sajenti Eliamini, alijeruhiwa vibaya na majambaz hao ambao watatu kati yao nao walijeruhiwa na kufariki wakati wakikimbizwa hospitali.
Wasafi Digital imefika katika Zahanati ya Polisi Oysterbay, Kinondoni ambapo askari huyo alitejeruhiwa anapatiwa matibabu ambapo Mrakibu wa Polisi Zahanati ya Polisi Oysterbay, Rukia Mbwambo, amesema askari huyo anaendelea vizuri na matibabu,
Hata hivyo, Kamanda Muliro amesema, uchunguzi wa awali umegundulika kuwa miongoni mwa majambazi hao ni majambazi sugu ambao waishawahi kufikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbalimbali katika nyakati tofauti.
WATCH WASAFI TV📺
AZAM - 411 | DSTV - 296 | ZUKU - 028 | STAR TIMES - 444 & 333 | COCONUT TV - 20 | DODOMA CABLE - 113
LISTEN WASAFI FM 📻
88.9 DAR/ZNZ/PWANI 📻 | 104.1 DODOMA 📻 | 94.5 ARUSHA 📻 | 97.3 MBEYA 📻 | 94.9 MWANZA 📻 | SHINYANGA 106.3 📻 | KIGOMA 101.7 📻
Follow Us On:
INSTAGRAM: / wasafitv || / wasafifm
TWITTER: / wasafitv || / wasafifm
FACEBOOK: / wasafitv
𝑪𝒐𝒑𝒚𝒓𝒊𝒈𝒉𝒕 ©2021 𝑾𝒂𝒔𝒂𝒇𝒊 𝑴𝒆𝒅𝒊𝒂. 𝑨𝒍𝒍 𝒓𝒊𝒈𝒉𝒕𝒔 𝒓𝒆𝒔𝒆𝒓𝒗𝒆𝒅.
#wasafi #KamandaMuliro #wasafifm