MAMBO YA KUZINGATIA KWA KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI 2021

  Рет қаралды 71,002

MKULIMA SMART TV

MKULIMA SMART TV

2 жыл бұрын

KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI
Katika shamba lililo hudumiwa vizuri na kupandwa katika hali ya hewa na aina ya mbengu. Vitunguu hutoa kiasi cha tani (10) hadi 16 kwa ekari moja.
MATUNZO YA BUSTANI YA VITUNGUU
PALIZI
Mmea wa kitunguu una mizizi mifupi, hii husababisha kutunguu kuathirika sana na ushindani na magugu. Mizizi mifupi ina maana huufanya kukosa uwezo wa kustahimili ushindani wa magugu.
Magugu yana uwezo mkubwa wa kufyonza virutubisho ardhini kuliko mimea ya mazao, na ndio maana magugu hukua kwa haraka kuliko mazao. Hivyo inashauriwa katika shamba la vitunguu hakikisha unafanya palizi kwa wakati.
Idadi ya palizi inategemea na aina na wingi wa magugu wa eneo husika. Kwenye ameneo yenye magugu mengi, palizi hufika hadi 4, na kwa maeneo ambapo magugu sio tatizo palizi mbili zinatosha.
UMWAGILIAJI
Zao la vitunguu linahitaji maji ya kutosha katika kipindi chote cha ukuaji wa mmea na hasa wakati wa kutunga tunguu. Katika kipindi kisicho na mvua (mwezi mei hadi Agosti) Umwagiliaji ufanyike mara moja kwa wiki kwa udongo wa mfinyanzi tifutifu na vitunguu vilivyopandwa katika vijaruba.
Ili kuharakisha kukomaa kwa vitunguu unashauriwa kupunguza kiasi cha maji ya kumwagilia taratibu kadri zao linavyo kua. Pia ni vizuri uache kumwagilia maji mapema wiki nne hadi sita kabla ya kuvuna. Kwani muda kamili wa kukomaa na kuvuna kwa vitunguu ni siku 90 hadi 150 kutegemea na aina ya mbegu.
UVUNAJI WA VITUNGUU
Muda wa ukomaaji wa vitungu hutegemea aina ya vitunguu pamoja na hali ya hewa ya eneo husika. Aina za chotora (hybrid) mara nyingi hukomaa mapema, huchukua miezi 3 hadi 5 baada ya kusia mbegu. Aina za kawaida (OPV) na zile za kienyeji hazina ukomaaji unaofanana (do not mature uniformly), hukomaa kwa makundi makundi.
UKAUSHAJI WA VITUNGUU.
Baada ya kuvuna kitunguu, hatua inayofuata ni ukaushaji (curing) na hii inafanyikia palepale shambani. Kukausha kitunguu ni ule mchakato wa kukausha ile shingo ya kitunguu. Shingo ya kitunguu inapokauka inakifunga kitunguu, pia inaziba njia ambazo zinaweza kutumiwa na vijidudu kuingia ndani kuharibu kitungu.
Ukaushaji pia husaidia kupata kitunguu chenye ngozi iliyokauka na yenye rangi nzuri.
UHIFADHI WA VITUNGUU (STORAGE)
Kitungu ndio zao lenye uwezo wa kuhifadhika kwa muda mrefu zaidi kuliko mazao yote ya mboga mboga. Kitunguu baada ya kuvunwa bado kinakua ni kiumbe kinachoishi (living organism) ikimaanisha kinaenelea na michakato kama kupumua, kupoteza maji n.k Hivyo uhifadhi wake unahitaji umakini ili kuweza kukaa muda mrefu bila kuharibika.
MATUMIZI YA MBOLEA.
1. MBOLEA KUNDI LA KWANZA.
➡Mbolea za kupandia.
Hizi huwekwa kabla au mara tu ya kuhamishia miche shambani. Mbolea hizi zina lengo la kusaidia ukuaji mzuri wa mifumo ya mzizi (root systems) itakayosaidia mmea kufyonza virutubisho na maji kutoka ktk udongo.
Mbolea hizi zina madini/ kirutubisho kikuu cha fosforasi (P), na huitwa mbolea za fosfeti (Phosphate Fertilizers), kundi hili lina mbolea kama MOP, TSP, DAP, Minjingu n.k.
2. MBOLEA ZA KUKUZIA
Mbolea hizi huwekwa kipindi cha ukuaji wa mmea (vegetative growth) na hua na lengo la kuupa mmea afya na ukuaji mzuri utakaopelekea kuwa na majani mazuri yatakayotengeneza chakula cha kutosha kwaajili ya mmea.
Kirutubisho kikuu katika kundi la mbolea hizi ni Nitrogen (N). Baadhi ya mbolea zilizopo kwenye kundi hili ni pamoja na UREA, SA, CAN n.k.
Pia kwenye kundi hili zipo mbolea za maji zinazopigwa kwenye majani (foliar fertilizers) hujulikana pia kama booster.
3. MBOLEA ZA KUZALISHA/KUKOMAZIA KITUNGU
KILIMO CHA VITUNGUU MAJI
KILIMO CHA KITUNGUU MAJI:- MBOLEA YA KUKUZIA ...
#mkulimasmart
#shambadarasa
Jinsi Ya Kufanya Kilimo Cha Vitunguu Maji 2021
KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI
MAELEZO YA MSINGI KUHUSU KILIMO CHA VITUNGUU
Kanuni za kilimo bora cha vitunguu maji
kilimo cha kitaalamu cha vitunguu maji Tanzania.
FAIDIKA NA KILIMO CHA VITUNGUU MAJI.
uzalishaji wa vitunguu kibiashara
bei ya mbegu za vitunguu maji
bei ya vitunguu maji kwa gunia 2021
bei ya vitunguu maji 2020
heka moja ya vitunguu inatoa gunia ngapi
changamoto za kilimo cha vitunguu
kilimo cha vitunguu maji pdf
bei za mbegu za vitunguu
kilimo cha vitunguu maji dodoma

Пікірлер: 29
@BrivianWere
@BrivianWere 29 күн бұрын
Hello asante sana kwa mafunzo Sasa ningeulizaje, nitaezaje kujua vitunguu viko karibu kuanza kutoa au kuzaa
@WinterMensoChansa
@WinterMensoChansa 4 ай бұрын
Mimi nipo apa Zambia napenda sana mafundisho yenu
@rehemahramadhani3428
@rehemahramadhani3428 2 жыл бұрын
hell nahitaj kufany kilimo na nyiny kam mtapenda
@MKULIMASMART
@MKULIMASMART 2 жыл бұрын
Karibu
@TEACHER.CLEOPHAS
@TEACHER.CLEOPHAS 2 жыл бұрын
Ahsante!!!
@shambadarasaTV
@shambadarasaTV 2 жыл бұрын
SAFI SANA
@adelabenward6662
@adelabenward6662 3 ай бұрын
mnatoa ushauri kwa garama? au bure
@Ditram-ox6ed
@Ditram-ox6ed Ай бұрын
Nahitaji kujifunza vizuli zaidi ili nianze kulima vitunguu
@piusxinlv5958
@piusxinlv5958 Жыл бұрын
Sante sana kwa elimu
@sharpp9921
@sharpp9921 2 жыл бұрын
Asante kwamafunzo
@MKULIMASMART
@MKULIMASMART 2 жыл бұрын
Karibu
@panduvuai871
@panduvuai871 Жыл бұрын
Very fantastic
@ezevisionmediastudioezevis7855
@ezevisionmediastudioezevis7855 6 ай бұрын
Namba zenu wapi sasa
@StamiliBasili-gn5ds
@StamiliBasili-gn5ds Жыл бұрын
Nahitaji kulima vitunguu nifanyaje sasa
@jofreytv
@jofreytv Жыл бұрын
Tatizo masoko
@MKULIMASMART
@MKULIMASMART 2 жыл бұрын
KARIBU SANA
@rehemahramadhani3428
@rehemahramadhani3428 2 жыл бұрын
nimewatumia sms hamjaijibu
@MKULIMASMART
@MKULIMASMART 2 жыл бұрын
@@rehemahramadhani3428 WhatsApp us 0713178868
@omarymussa7627
@omarymussa7627 2 жыл бұрын
@@MKULIMASMART habari
@nasseralkharusi2060
@nasseralkharusi2060 Жыл бұрын
Amani kwa wenye kufata uongofu Ni mwezi gani unaanza kupanda
@piusxinlv5958
@piusxinlv5958 Жыл бұрын
Mfano naitaji panda eka moja huwa inaweza garim mtaji kiasi gani?
@MKULIMASMART
@MKULIMASMART Жыл бұрын
WhatsApp us
@catherinelandas1938
@catherinelandas1938 3 ай бұрын
@@MKULIMASMART hi
@lucykipanta8168
@lucykipanta8168 2 жыл бұрын
Kilimo cha vitunguu vinafaa sehem yenye hali ip ya hewa??
@MKULIMASMART
@MKULIMASMART 2 жыл бұрын
Isiwe na mvua nyingi
@MKULIMASMART
@MKULIMASMART 2 жыл бұрын
Kwa mafunzo WhatsApp number 0713178868
@saumbenson7312
@saumbenson7312 2 жыл бұрын
Heka moja inatoa gunia ngapi??
@MKULIMASMART
@MKULIMASMART 2 жыл бұрын
100
路飞太过分了,自己游泳。#海贼王#路飞
00:28
路飞与唐舞桐
Рет қаралды 15 МЛН
Red❤️+Green💚=
00:38
ISSEI / いっせい
Рет қаралды 82 МЛН
UZALISHAKI WA VITUNGUU
10:08
TAHA ONLINE TV
Рет қаралды 6 М.
I Filmed Plants For 15 years | Time-lapse Compilation
30:40
Boxlapse
Рет қаралды 11 МЛН
Kenya: Minting fortunes from garlic
4:46
Agribusiness TV
Рет қаралды 44 М.
KILIMO CHA MAHARAGE: UPANDAJI, MBOLEA NA UTUNZAJI
15:16
AGALUS TV
Рет қаралды 58 М.
Breeding method to grow garlic quickly to harvest
9:35
EY - Gardening
Рет қаралды 16 МЛН
路飞太过分了,自己游泳。#海贼王#路飞
00:28
路飞与唐舞桐
Рет қаралды 15 МЛН