Рет қаралды 7,925
June 8, 2018 Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Eng Hamad Masauni amesema Serikali inafanya uchunguzi na itachukua hatua kufuatia tukio la Askari wanaodaiwa kusababisha mwanamke kujifungua mtoto akiwa nje ya kituo cha polisi Morogoro walipokuwa wakimshikilia.
Hatua hiyo inafuatia hoja iliyotolewa na Mbunge wa Arumeru mashariki Joshua Nassari aliyetaka Bunge lijadili suala hilo kutokana na matukio kama hayo kujitokeza mara kwa mara huku Serikali ikiyakalia kimya.