SANAMU YA NYERERE YAVUNJWA, WASIYOJULIKANA WATAJWA ‘Tumekuta kipande cha shuka.’

  Рет қаралды 2,954

Mwananchi Digital

Mwananchi Digital

Күн бұрын

Katika hali isiyokuwa ya kawaida watu wasiofahamika wamevamia na kuvunja sanamu la Mwalimu Nyerere lililopo Mtaa wa Matola, Kata ya Chemchem Manispaa ya Tabora, ambapo wameondoka na shingo ya sanamu hilo pamoja na fimbo aliyokuwa akiishikilia Nyerere enzi za uhai wake.
Akizungumzia tukio hilo leo Jumamosi Septemba 21, 2024, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema kitendo hicho kimetokea usiku wa kuamkia leo.
Amesema wahalifu wamevunja na kuondoka na shingo ya sanamu hilo pamoja na fimbo, huku akisisitiza tayari uchunguzi kuhusu tukio hilo umeanza kufanyika.
"Tumefika hapa na kukagua eneo la tukio na ni kweli kwamba sanamu hili limeondolewa kutoka kwenye sehemu, ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye mnara wake. Sanamu hili limevunjwa maeneo matatu. Kikubwa tunachunguza kujua ni mazingira gani yamesababisha sanamu lifike chini,’’ amesema.
Ameongeza: ‘’Kwenye eneo la tukio tumekuta kipande cha shuka na suruali nyeusi. Kipande cha fimbo kilichotengenezwa na zege hakipo, hivyo uchunguzi tunaofanya utatupa majibu maana changamoto ya eneo husika ni eneo ambalo halina ulinzi, pia hakuna umeme, tukio hilo limegundulika asubuhi.

Пікірлер: 43
@ThomasAlute
@ThomasAlute 3 сағат бұрын
Wamefanya kazi nzuri mno kwa sababu watu wengine wanatekwa mumejifanya kimya eti kamanda wa polisi mkoa anaenda kupeleleza sanamu ya Nyerere ujinga mkubwa tulionao
@Awatee
@Awatee Сағат бұрын
😂😂😂😂Tanzania yetu iyo
@husseinmramba
@husseinmramba 52 минут бұрын
Acha mihemko mtoto wakiume umeshikizwa akili yako yote unakazi kukazana kutekwa tu, heb jifunze kupambanua mambo usiwe kama kondoo kwenda na mkumbo tu na kuto kutakari linaloendelea mbeleni
@OmmyJames-xn7ji
@OmmyJames-xn7ji 27 минут бұрын
SHIDA NI MAPALOKO NDIO WATEKAJI NA SACCOOS LAKINI WAGALATIA HAWAWEZI KUHOJI KWA WACHUNGAJI 😢😢😢😢😢
@nguruwekikwete1635
@nguruwekikwete1635 2 сағат бұрын
Dalili ya kuvunjika kwa taifa chini ya ccm ya samia na kugawanyika sehemu tatu
@EmmanuelNyinyigwa-m1o
@EmmanuelNyinyigwa-m1o 3 сағат бұрын
Bora wameivunja ilikuwa sanam ya hovyo sana iludiwe upya. Nyerere hakuwa akifanana hivyo.
@cheiknamouna2058
@cheiknamouna2058 Сағат бұрын
Hahahaaa hebu nicheke mie eti mzee analaani na anapata uchungu mbona matukio mengine hamuungani hivi mkalaani😂😂😂
@josephlorri431
@josephlorri431 3 сағат бұрын
Unganisha nukta...wanatishwa na sanamu ya Nyerere.. wapo wale wanaopotosha historia ya uhuru wetu..
@DevotaKavishe-p4w
@DevotaKavishe-p4w 49 минут бұрын
Hii nchi sijui kama tutavuka salama kwa kweli haya na hili sanamu limetukosea nini wanadamu
@kiconnection
@kiconnection 3 минут бұрын
kazi njema hatuwezi kuabudu sanamu badala ya MUNGU aliye hai na Muumba wa mbingu na nchi, sioni tatizo hapo, atukuzwe MUNGU aliye Mkuu kwa kufanyika hilo kuvunjwa kwa sanamu isiyo na uhai,
@Yasintaeustas
@Yasintaeustas Сағат бұрын
Tanzania yetu ya leoooo.
@xxxl-jf2ji
@xxxl-jf2ji 3 сағат бұрын
Pumbavuuu
@mataypanga5262
@mataypanga5262 Сағат бұрын
Nyerere mwenyewe ataletaje uhuru?. Hivi ukienda kuwinda ukaua mnyama kwa fimbo,utaenzi fimbo yako tu?😂
@ndolepeter2770
@ndolepeter2770 3 сағат бұрын
kwa uharibifu na fujo hizo ndy kabisaa mtaishia kunawa hamta kula
@saidimgina8299
@saidimgina8299 2 сағат бұрын
Ucheni ujinga umnaumia kisa sanamu huyu mtu kamuenzi nabii Ibrahim baba wa imani
@HanifaOman-oo4pl
@HanifaOman-oo4pl 6 минут бұрын
😂😂
@PrinceHendry-hp8vv
@PrinceHendry-hp8vv 3 сағат бұрын
Upuuzi tu na misanamu
@xxxl-jf2ji
@xxxl-jf2ji 3 сағат бұрын
😂😂😂😂😂😂😅😅😅😅😅😅😂
@SalmanMughal-lq5lt
@SalmanMughal-lq5lt 3 сағат бұрын
Upepo Labda umevunja Au watu walijua ndani yake Kuna dhahabu
@SarahEdithchambo
@SarahEdithchambo 53 минут бұрын
Hii ni hatari shida wanajua Nyerere ndio chimbuko la amani sasa watu wachache wanaotumwa hawanauelewa ndio wanafanya hivi acheni tu ccm iendelee kutawala upande wa 2 hakuna mtawala
@ceciliaathanas3135
@ceciliaathanas3135 2 сағат бұрын
Ila tz😂😂
@MtanganyikaTanganyika
@MtanganyikaTanganyika 52 минут бұрын
Mzee anasikia uchungu sana mkombozi ni MUNGU siyo uyo unayemsema hii inamanisha utawala utadondoka maana mwenye Dola kadondoka
@martinchambala9399
@martinchambala9399 3 сағат бұрын
Tuwalaani kwa nguvu mashetani waliofanya hivyo
@OfficialA83640
@OfficialA83640 2 сағат бұрын
Sanamu mnalaani lkn mauji mpo kimya😮
@Mrmohadi.OFFICIAL
@Mrmohadi.OFFICIAL 22 минут бұрын
Adi sanamu tena la vunjwa na wasio julikana duh
@annabyekwaso-wt7oi
@annabyekwaso-wt7oi 3 сағат бұрын
Aisee!kwanini kinaendelea kwenye Taifa letu jamani!
@HanifaOman-oo4pl
@HanifaOman-oo4pl 12 минут бұрын
Wasiyo julikana ni noma
@SalumonEustace-cl4mk
@SalumonEustace-cl4mk Сағат бұрын
Nchi ya hovyo kabsaa , badala ya kupambana na wanaoteka watu na kuwauwaa mnapambana na walioharibu sanamuu? ila police wetu hawaa kazii ipooo
@WilliamKivugo
@WilliamKivugo Сағат бұрын
Safi sana 😂😂😂😂😂
@SarahEdithchambo
@SarahEdithchambo 52 минут бұрын
Mshikamano nimuhimu wanayofanya vizazi zichache vicvyoelewa
@JeremiahKavakule
@JeremiahKavakule Сағат бұрын
Selikari mupo wapi hawa wanaotima sms kejeli ndiyo muanze nao watasaidua uchunguzi siyo munakaa kimya kama selikari haipo
@BahatiIsangu
@BahatiIsangu 2 сағат бұрын
Tanzani hiii jmn au nyingine
@SephaniaMsigwa
@SephaniaMsigwa Сағат бұрын
Ushetani gani huu
@TumpeNamkumbwa-x6z
@TumpeNamkumbwa-x6z 2 сағат бұрын
Ni watu wasiojulikana au?kwani hakuna walizi
@CTM.24Updates
@CTM.24Updates Сағат бұрын
Kwahiyo NYERERE amevunjika kiuno??😂😂😂
@Awatee
@Awatee Сағат бұрын
😂😂😂😂😂
@rogerabdallah439
@rogerabdallah439 8 минут бұрын
Katekwa na kuuliwa
@AbuodSeleman
@AbuodSeleman 2 сағат бұрын
TZ IMECHAFUKWA SASA
@saidihatibu-g5l
@saidihatibu-g5l 38 минут бұрын
😂😂😂
@HanifaOman-oo4pl
@HanifaOman-oo4pl 12 минут бұрын
😂😂😂 lnalillahi wainailahi rajuun. Allah tujaalie mwisho mwema. Misanamu ni haram ,,Uislam raha
@saimongilala8938
@saimongilala8938 3 сағат бұрын
Kwan Kuna nn tz jaman araaniwe mtu Alie fanya hivyo
@OmmyJames-xn7ji
@OmmyJames-xn7ji 20 минут бұрын
USILAANI WAKATI MAPALOKO WANAMALIZA MAALBINO
@rogerabdallah439
@rogerabdallah439 8 минут бұрын
Mmmmmmmmm😂😂😂😂😂😂
ASKARI WA FFU WAZINGIRA JIJI LA DAR, YADAIWA MAANDAMANO CHANZO
3:56
Mwananchi Digital
Рет қаралды 33 М.
Electric Flying Bird with Hanging Wire Automatic for Ceiling Parrot
00:15
SCHOOLBOY. Мама флексит 🫣👩🏻
00:41
⚡️КАН АНДРЕЙ⚡️
Рет қаралды 7 МЛН
Как подписать? 😂 #shorts
00:10
Денис Кукояка
Рет қаралды 6 МЛН
CHADEMA YATANGAZA NJIA ZITAKAZOTUMIKA KWENYE MAANDAMANO
2:10
Mwananchi Digital
Рет қаралды 9 М.
HALI ILIVYO MITAA MBALIMBALI DAR , POLISI WAFURIKA KILA KONA
4:16
Mwananchi Digital
Рет қаралды 3,3 М.
WASIOJULIKANA WADAIWA KUMWAGIA TINDIKALI KADA WA CCM YASEMEKANA...
2:29