Mfahamu Mzee Mshume Kiyate na alivyomsaidia Mwl. Nyerere katika Harakati za Uhuru.

  Рет қаралды 192

AfricanLiberation TV

AfricanLiberation TV

3 ай бұрын

Mshume Kiyate alikuwa mwanaharakati na mzalendo aliyeshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950. Vilevile alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa karibu sana na Hayati Mwalimu Nyerere hata kupelekea kumzungumzia mara kwa mara katika mazungumzo yake. Mwalimu siku moja katika kuwakumbuka rafiki zake wa zamani akizungumza na Dossa Aziz na wageni wengine nyumbani kwake Msasani, katika kuelezea kile alichokiita "the TANU spirit" yaani moyo wa upendo wa wana-TANU, alisema kuwa, siku moja wakati wa kudai uhuru alikuwa anatoka nyumbani kwake Magomeni akija Kariakoo kwa miguu kuelekea sokoni kutafuta mahitaji yake, lakini mfukoni alikuwa hana senti moja. Njiani akakutana na Mzee Mshume Kiyate. Alipomuuliza anakwenda wapi, alimfahamisha kuwa anakwenda sokoni lakini hana fedha za kununua chochote. Mzee Mshume aliingiza mkono katika koti lake na akatoa shilingi mia mbili akampa. (Ukitaka kujua thamani ya fedha hizo ikutoshe tu kuwa nyumba ya vyumba sita kujenga Kariakoo ilikuwa inagharimu shilingi mia tano).
Kutokana na hali hii Mshume Kiyate aliona itakuwa ni kumtwisha Mwalimu mzigo mzito ikiwa atakuwa anashughulika na kuwatafutia wanawe chakula na wakati huo huo anafanya kazi za TANU. Mzee Mshume akajitolea kuihudumia nyumba ya Mwalimu kwa chakula. Alifanya hivyo hadi uhuru ulipopatikana.
Baada ya maasi ya wanajeshi wa KAR tarehe 20 Januari, 1964 kuzimwa na jeshi la Kiingereza, TANU ilifanya mkutano mkubwa sana Jangwani. Mzee Mshume kwa niaba ya wazee wa TANU alipanda jukwaani na kumvisha Mwalimu kilemba kama ishara ya kuunga mkono uongozi wake.

Пікірлер
KUMBUKIZI YA MIAKA 24 YA MWL J K NYERERE NA SENSA
19:53
Nbs Tanzania
Рет қаралды 894
What it feels like cleaning up after a toddler.
00:40
Daniel LaBelle
Рет қаралды 79 МЛН
IJUE HISTORIA YA TANGANYIKA KABLA YAKUPATA UHURU
11:50
CLOUDSMEDIA
Рет қаралды 36 М.
Hili ndilo lilikua Lengo la Mwl. Nyerere juu ya Muungano wa Tanzania!
3:06
"Mtu Mwenye Akili Haulizi Kwanini Tuliungana"- Mwl. JK Nyerere.
4:03
AfricanLiberation TV
Рет қаралды 668
BABA WA TAIFA ALIILILIA TANZANIA KABLA YAKUKATA ROHO.
21:57
Wasafi Media
Рет қаралды 1,8 МЛН