Рет қаралды 72,910
Mvua iliyonyesha takriban kwa saa saba kuanzia saa tisa alfajiri ndani ya mkoa wa Dar es Salaam, imeacha maumivu kwa wakazi wa mkoa huo ambapo baadhi ya nyumba zimesombwa na maji, huku mawasiliano ya barabara yakikatika.
Wakazi wa Tegeta Nyuki na Mbezi Beach jijini hapa wamesema wako katika hali mbaya baada ya maji ya mvua inayoendelea kunyesha Januari 20, 2024, kutuama na kubomoa makazi yao.
Mwananchi Digital, leo imefika Mbezi Beach na Tegeta Nyuki kushuhudia wingi wa maji hayo, huku wananchi wakieleza kilio chao.