Рет қаралды 3,688
Wakili Peter Madeleka anayemwakilisha Paul Kisabo kwenye kesi ya inayomkabili Afisa Fatma Kigondo kwa kuwezesha genge la watu wanne kufanya ukatili kwa binti wa Yombo amesema, kesho Oktoba 16, 2024 atawasilisha maombi kwa Mahakama Kuu ya Tanzania ili kuangalia shauri la kesi hiyo kama linakiuka sheria.
Wakali Madeleka anatoa kauli hii baada ya kutokea mvutano baina yake na hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya wilaya ya Dodoma Nyambuli Tungaraja kwa kutupilia mbali hoja walizo wasilisha za kutaka afisa huyo kukamatwa kwa kuidharau mahakama kwa kushindwa kufika mahakamani Oktoba 7, 2024 na kutokupewa dhamana.
Wakili huyo amesema, uamuzi uliyotolewa ni kuwa hakimu hawezi kutoa amri ya kumkamata Fatma Kigondo na wala hawezi kutoa amri ya kunyima dhamana kwa kuwa dhamana ni haki ya mshtakiwa.
Unaweza kutufuatilia kupitia;
TWITTER: / thechanzo
INSTAGRAM: / thechanzo
FACEBOOK: / thechanzo
TIKTOK: www.tiktok.com....
Au tembelea tovuti yetu: www.thechanzo.com
Je, una habari? wasiliana nasi kupitia Telegram/WhatsApp +255 753 815 105
The Chanzo Initiative, 2024 © All Rights Reserved.