Ndoto Ya Kuwa Mwanajeshi Mpaka Kuwa Designer Mkubwa Tanzania | SALAMA NA MARTIN KADINDA PT 1

  Рет қаралды 22,720

YahStoneTown

YahStoneTown

Жыл бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Martin Kadinda ni rafiki yangu, ni moja ya wale wana ambao hana makuu na zaidi yeye anapeeenda sana kucheka, hata ukiangalia picha zake yeye ana tabasamu tu. Pengine hiyo ndo siri ya mafanikio yake tofauti yake na wengine na pengine hiyo ndo sababu ya mimi kumpenda sana. Pia ni FUNDI, tena mzuri tu sana. Kati ya mafundi wachache WAKWELI wa nchi hii Martin ni mmoja wapo, kama hawezi hawezi, hata siku moja hawezi chukua kazi yako alafu siku ya siku akakuharibia shughuli au mtoko. Kama yuko busy na mambo yake atakuambia rafiki, hiyo sitoweza tafadhali mtafute mtu mwengine aifanye. Napenda jinsi alivyo honest maana mimi huamini sana kwenye ukweli mgumu kuliko uongo mtamu.
Urafiki wetu ni wa miaka zaidi ya kumi sasa, anakua namuona na bila ya shaka nae ananiona nami ninavyokua, na wote tunaona kustawi kwa kila mmoja wetu, maendeleo kati yetu, challenges na urafiki wa mashaka kwa baadhi ya watu tunao wafahamu pamoja na kung’amua mambo mbali mbali kwa pamoja. Sisi si wana ambao tunazungumza DAILY ila ni wana ambao kila tulikutana basi huanzia pale tulipo ishia mara ya mwisho tulipo kutana. Hatuna neno kati yetu na wala urafiki wetu si wa KULAZIMISHA.
Napenda jinsi ambavyo anasogea kwenye maisha yake, Martin ni mmoja ya watu wachache ambao nawafahamu ambao HAWANA HARAKA ya MAFANIKIO, HANA MASHINDANO na MTU, anafanya yake kwa SPIDI yake na anashindana na yule Martin wa mwaka jana ambaye alimuambia mwaka huu In Shaa Allah atakua kapiga hatua hii na hii na hii na kuhakikisha ile mipango na malengo YANATIMIA kwa usimamizi wa Maulana.
Martin anawajua watu tele kwenye industries tofauti hapa kwetu na wala hutakaa umsikia akirusha majina ya watu hao ili aweze kujiingiza kwenye mazungumzo ambayo hayamhusu au hayana faida na yeye. Mara zote huwa ana focus na yale ambayo yanamhusu na wakati mwengine hayo pia ambayo yanamhusu akiona hayana muelekeo au hasara ni nyingi kuliko faida basi pia si mtu wa kung’ang’ania jambo kwasababu tu ni la mtu fulani au lina line fulani, anaamini kwenye kuanza upya na kwamba kila siku mpya ni sababu nyengine ya kuwa bora kuliko jana na ni nafasi nyengine ya kuweza kutimiza ndoto fulani.
Baba wa mtoto mmoja ambaye alimpata akiwa mdogo tu, Martin anampa mwanawe uhuru wa kuwa mtoto na kuwa yeye na si kumtanguliza mbele kwenye maisha ya yeye kama Baba yake na kumyima uhuru wa kuishi maisha yake kama mtoto na HURU. Tushaona mifano tele hai ya ma celebrity wa Bongo ambao wanawaweka au waliwaweka watoto wao mbele na badala yake wakaishia kuwa target ya matusi kutoka kwa walimwengu na mwisho wake wazazi waishia kulalamika kujumuishwa kwa watoto wao kwenye maisha yao. Tunatakiwa kuamini kwenye kila mtu kujichagulia maisha yake ambayo anataka kuishi na hatusemi kumpost mtoto kwenye mtandao ni jambo baya sana, ila kwa jamii ambayo kumtukana mtoto na wazazi wake haioni kitu cha hatari au kuumiza au kushangaza, nadhani kwa mzazi kumuacha mtoto awe mtoto mpaka pale atakapo jitambua na kuchagua mwenyewe pengine huo ndo ungekua uamuzi sahihi zaidi. Na sisemi pia kama ni sawa kwa walimwengu kufanya hivyo, ila ukishaona kuna mwanya wa jambo kama hilo, mmoja kuamua kuchagua faragha ni jambo jema zaidi.
Hii haikua mara ya kwanza mimi na Martin kukaa chini na kuongea kwenye TV ingawa mara ya mwisho inawezekana ikawa ni miaka 6 au 7 iliyopita lakini bado kulikua na haja na kiu ya kufanya hii, kama nilivyo kuambia hapo juu, tulikutana haijalishi ni muda gani umepita, siku zote tutaanzia pale tulipo ishia.
Yangu matumaini simulizi za urafiki, biashara, wazazi, mtoto, kazi na kuhangaika na kuji panga na kujipa nafasi ambako kumeongelewa humu kutakusaidia kwa kiasi flani kukutoa sehemu moja na kukupeleka sehemu nyengine. Na yangu matumaini pia uta enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪KZbin Link bit.ly/KZbinSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Пікірлер: 33
@mariastella1878
@mariastella1878 Жыл бұрын
Pole saana Martin, kifo cha mama yako kinafanana na cha my mom,hatukuwahi kuona anaumwa sana maisha yake yote,alikua wa kwanza kufariki kwenye family yetu,tunamshukuru Mungu kwa maisha ya mama zetu Glory to God🙏🙏
@moudmgomo5742
@moudmgomo5742 Жыл бұрын
salama unajua sister. I wish one
@josephinenamigadde5518
@josephinenamigadde5518 Жыл бұрын
Martin is so bright upstairs
@elizabethhonere2931
@elizabethhonere2931 Жыл бұрын
Story ya kifo cha mama yako inafanana kabisa na ya mama yngu..😭😭😭😭😭Mungu awalaze mahali pema peponi mama zetu
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 Жыл бұрын
Hujambo 🙌napenda anavy sem!!! Hujambo mimi ni Salama
@zeinababdi4757
@zeinababdi4757 Жыл бұрын
My beloved dada passed on the valentines day...may his soul rest in peace 🙏
@alexchungu6263
@alexchungu6263 Жыл бұрын
Angekuwa soldier, angependeza sanaaa
@rosemofuga8101
@rosemofuga8101 Жыл бұрын
She was a best mum and best wife MUNGU amrehemu
@nicolenabintu2509
@nicolenabintu2509 Жыл бұрын
Habari ya mother ndio ina niita moyo , Mungu wa wazazi wetu walio tangulia mbele za haki wateteye😂duniani hapa pagumu 🥰🙏🏿😭
@itNeza
@itNeza Жыл бұрын
Nipo Tayari Hapa Wakwanza Kabisa 😋💯❤️
@rosemofuga8101
@rosemofuga8101 Жыл бұрын
Pole sana brother Martin
@lynusjacob6727
@lynusjacob6727 Жыл бұрын
Me ckuamn Hadi wakati naweka udongo nilisikia maumivu ajabu namwon Martin maumivu aliyopitia co rahisi wanasema Bora wanaolia sanaaa
@leaherasto929
@leaherasto929 Жыл бұрын
Pole Sana Martin,, Mungu amrehemu mama aendelee kupumzika kwaamani AMINA
@elizabethsakina2306
@elizabethsakina2306 Жыл бұрын
Chidbenz next please 🤝
@heightsmays5963
@heightsmays5963 Жыл бұрын
Tunaomba mtuletee Mtanzania Moto Mabanga.
@fathumramadhan7567
@fathumramadhan7567 Жыл бұрын
hello madam salama napenda sana unachokifanya na watching nikiwa Doha Qatar one love 🇰🇪
@nicoscarolyne872
@nicoscarolyne872 Жыл бұрын
nipo tayari hapa wa pili kabisa
@queenlinda255
@queenlinda255 Жыл бұрын
Kwani Martin anaumri gani maana anasema alimuona mwinyi model those days
@twahasuleiman6135
@twahasuleiman6135 Жыл бұрын
Salama Leo umefunikwa... Na Martin. Hhhhhhhh
@Zainabuabdalah-vw1xw
@Zainabuabdalah-vw1xw
🎉
Пранк пошел не по плану…🥲
00:59
Саша Квашеная
Рет қаралды 6 МЛН
A clash of kindness and indifference #shorts
00:17
Fabiosa Best Lifehacks
Рет қаралды 127 МЛН
HAWA NDIO MASTAA TISA  WA BONGO WENYE FOLLOWERS WENGI INSTAGRAM
4:59
Salama Na Masoud Kipanya
52:05
YahStoneTown
Рет қаралды 14 М.