"Sijawahi Kuutafuta Umaarufu, Wema Asipopokea Simu Yangu Namuelewa" | SALAMA NA MARTIN KADINDA PT2

  Рет қаралды 14,610

YahStoneTown

YahStoneTown

Күн бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Martin Kadinda ni rafiki yangu, ni moja ya wale wana ambao hana makuu na zaidi yeye anapeeenda sana kucheka, hata ukiangalia picha zake yeye ana tabasamu tu. Pengine hiyo ndo siri ya mafanikio yake tofauti yake na wengine na pengine hiyo ndo sababu ya mimi kumpenda sana. Pia ni FUNDI, tena mzuri tu sana. Kati ya mafundi wachache WAKWELI wa nchi hii Martin ni mmoja wapo, kama hawezi hawezi, hata siku moja hawezi chukua kazi yako alafu siku ya siku akakuharibia shughuli au mtoko. Kama yuko busy na mambo yake atakuambia rafiki, hiyo sitoweza tafadhali mtafute mtu mwengine aifanye. Napenda jinsi alivyo honest maana mimi huamini sana kwenye ukweli mgumu kuliko uongo mtamu.
Urafiki wetu ni wa miaka zaidi ya kumi sasa, anakua namuona na bila ya shaka nae ananiona nami ninavyokua, na wote tunaona kustawi kwa kila mmoja wetu, maendeleo kati yetu, challenges na urafiki wa mashaka kwa baadhi ya watu tunao wafahamu pamoja na kung’amua mambo mbali mbali kwa pamoja. Sisi si wana ambao tunazungumza DAILY ila ni wana ambao kila tulikutana basi huanzia pale tulipo ishia mara ya mwisho tulipo kutana. Hatuna neno kati yetu na wala urafiki wetu si wa KULAZIMISHA.
Napenda jinsi ambavyo anasogea kwenye maisha yake, Martin ni mmoja ya watu wachache ambao nawafahamu ambao HAWANA HARAKA ya MAFANIKIO, HANA MASHINDANO na MTU, anafanya yake kwa SPIDI yake na anashindana na yule Martin wa mwaka jana ambaye alimuambia mwaka huu In Shaa Allah atakua kapiga hatua hii na hii na hii na kuhakikisha ile mipango na malengo YANATIMIA kwa usimamizi wa Maulana.
Martin anawajua watu tele kwenye industries tofauti hapa kwetu na wala hutakaa umsikia akirusha majina ya watu hao ili aweze kujiingiza kwenye mazungumzo ambayo hayamhusu au hayana faida na yeye. Mara zote huwa ana focus na yale ambayo yanamhusu na wakati mwengine hayo pia ambayo yanamhusu akiona hayana muelekeo au hasara ni nyingi kuliko faida basi pia si mtu wa kung’ang’ania jambo kwasababu tu ni la mtu fulani au lina line fulani, anaamini kwenye kuanza upya na kwamba kila siku mpya ni sababu nyengine ya kuwa bora kuliko jana na ni nafasi nyengine ya kuweza kutimiza ndoto fulani.
Baba wa mtoto mmoja ambaye alimpata akiwa mdogo tu, Martin anampa mwanawe uhuru wa kuwa mtoto na kuwa yeye na si kumtanguliza mbele kwenye maisha ya yeye kama Baba yake na kumyima uhuru wa kuishi maisha yake kama mtoto na HURU. Tushaona mifano tele hai ya ma celebrity wa Bongo ambao wanawaweka au waliwaweka watoto wao mbele na badala yake wakaishia kuwa target ya matusi kutoka kwa walimwengu na mwisho wake wazazi waishia kulalamika kujumuishwa kwa watoto wao kwenye maisha yao. Tunatakiwa kuamini kwenye kila mtu kujichagulia maisha yake ambayo anataka kuishi na hatusemi kumpost mtoto kwenye mtandao ni jambo baya sana, ila kwa jamii ambayo kumtukana mtoto na wazazi wake haioni kitu cha hatari au kuumiza au kushangaza, nadhani kwa mzazi kumuacha mtoto awe mtoto mpaka pale atakapo jitambua na kuchagua mwenyewe pengine huo ndo ungekua uamuzi sahihi zaidi. Na sisemi pia kama ni sawa kwa walimwengu kufanya hivyo, ila ukishaona kuna mwanya wa jambo kama hilo, mmoja kuamua kuchagua faragha ni jambo jema zaidi.
Hii haikua mara ya kwanza mimi na Martin kukaa chini na kuongea kwenye TV ingawa mara ya mwisho inawezekana ikawa ni miaka 6 au 7 iliyopita lakini bado kulikua na haja na kiu ya kufanya hii, kama nilivyo kuambia hapo juu, tulikutana haijalishi ni muda gani umepita, siku zote tutaanzia pale tulipo ishia.
Yangu matumaini simulizi za urafiki, biashara, wazazi, mtoto, kazi na kuhangaika na kuji panga na kujipa nafasi ambako kumeongelewa humu kutakusaidia kwa kiasi flani kukutoa sehemu moja na kukupeleka sehemu nyengine. Na yangu matumaini pia uta enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
‪KZbin Link bit.ly/KZbinS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Пікірлер: 39
@nhondomalale8147
@nhondomalale8147 Жыл бұрын
Both of the two (interviewed and interviewer) are genius. They know both what to speak and how to do it.
@raymondmuga7542
@raymondmuga7542 Жыл бұрын
I have never understood this guy before, but today he gave me a good interview, smart dude, keep it up
@happinessngassa4864
@happinessngassa4864 Жыл бұрын
I just love the way he present himself
@zainabsibuma-omary7061
@zainabsibuma-omary7061 Жыл бұрын
Congratulations MK, you are smart and have a great vision. We're proud of you 👏
@didakalaule7840
@didakalaule7840 Жыл бұрын
Hujawahi kukosea Salama nilitamani msimalize maongezi 🔥🔥🔥
@mostyhodari2145
@mostyhodari2145 Жыл бұрын
One of the best interview this year all the best guys.
@mamlee8167
@mamlee8167 Жыл бұрын
Martin is a very smart guy .You can tell that he was raised well.
@nhondomalale8147
@nhondomalale8147 Жыл бұрын
Sijui kama kutakuja kutokea mhojaji (interviewer) kama salama jabir Lily ommy. They have more than a school and talent, they have technics. Unakuta mhojaji anakuhoji kana kwamba anajua majibu tayari ya mhojiwa. You two guys, congratulations
@scholamodestus9386
@scholamodestus9386 Жыл бұрын
Umemsahau millard ayo na SNS
@ilovejesus9303
@ilovejesus9303 Жыл бұрын
Very classy, very smart, very intelligent 👏 👌 👍
@mosessarya2174
@mosessarya2174 Жыл бұрын
this show is big we know the side of people we never knew big up to the team
@rosemofuga8101
@rosemofuga8101 Жыл бұрын
Yaani hapo kwenye kuongea kihehe hapo nimepaludia kama mara nane hivi nacheka balaa, hongera bro unaona hukukataa baada ya kuambiwa na bibi sasa una a beautiful young lady
@tedepakinabo7547
@tedepakinabo7547 Жыл бұрын
I love this Kaka 👌💖💖💖 May God shower you with lots of Blesses🙏. The best interview 🙌 👌 👏 💪 ✨️ 👍 💖💖💖
@zwatts38
@zwatts38 Жыл бұрын
What a gentleman..
@rosemofuga8101
@rosemofuga8101 Жыл бұрын
Brother Martin kumbe mhehe,nimeipenda hiyo ya (ulakana kabisa huyo mwanako)
@pillyolsen6346
@pillyolsen6346 Жыл бұрын
Maritim nimependa bure wewe umeogea ukweli alafu unaakili mstarabu sana hogera sana kaka utafika mbali inshallah
@nashatahmed1995
@nashatahmed1995 Жыл бұрын
Namna anavyoelezea msiba wa mama yake ukweli amenikumbusha msiba wa Mama yangu.
@blandinamyinga9489
@blandinamyinga9489 Жыл бұрын
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣ulakana uyo mwanako dahh""nimekumbuka mbali saaaaaaaaaana
@rosemofuga8101
@rosemofuga8101 Жыл бұрын
Piga kelele kwa mhehe wake weweeeeeeeeee
@blandinamyinga9489
@blandinamyinga9489 Жыл бұрын
@@rosemofuga8101 😂😂
@ibramrzebra1675
@ibramrzebra1675 Жыл бұрын
Martin the King of fashion
@fafafafa7175
@fafafafa7175 Жыл бұрын
Nimetamani kisiishe ❣️❣️❣️❣️
@stephanoedimund7841
@stephanoedimund7841 Жыл бұрын
SALUTE
@niwaherikochecha7452
@niwaherikochecha7452 Жыл бұрын
Salama kindly interview Terence Mwakaliku
@rosemofuga8101
@rosemofuga8101 Жыл бұрын
Yaani hii interview ilikuwa babu kubwa
@winfridamwigilwa2107
@winfridamwigilwa2107 Жыл бұрын
Interview nzuri sana
@mfaumemkigoma4370
@mfaumemkigoma4370 Жыл бұрын
Watanzania tunashida sana hivi haiwezekani huongea ukamaliza bila kuongea kingereza ,kama hapo kaka Muha mwenzangu kiswahili ndio kimemkuza ,lakin ajifanya kingereza tujue kasoma sipendi,salama uwe unaanda na interview za kingereza kwaajili ya wageni mnatuchanganya nyie waswahili
@mummytt1516
@mummytt1516 Жыл бұрын
I like it
@tedepakinabo7547
@tedepakinabo7547 Жыл бұрын
Salama 🙌🤗🥰🥰🥰💖💝
@calvindonalds5373
@calvindonalds5373 Жыл бұрын
INterview na Mchungaji Hananja iliishia wapi boss?
@yusraramadhan8203
@yusraramadhan8203 Жыл бұрын
😍👏🏿
@dianerditto
@dianerditto Жыл бұрын
Elfu huanzia moja
@stellah3844
@stellah3844 Жыл бұрын
🔥🔥🔥🔥
@sylviamsumba2212
@sylviamsumba2212 Жыл бұрын
Salama na Fredrick bundala(sns)
@rhodajackson2213
@rhodajackson2213 Жыл бұрын
Jamani , ni nini hiki , story ya Mama yangu ...Wapumzike kwa Amani Mama Zetu
@maulidmalik5364
@maulidmalik5364 Жыл бұрын
Kwan mpka muongee icho kidhunguuu jaman
@davidheche839
@davidheche839 Жыл бұрын
Salama umesema ukweli sana kuhusu Mtani, Martin sikuwahi kufanya nae kazi ila ntamtafuta baada ya hii interview, Mtani alikataaga kazi yangu sababu schedule yake imejaa nilishangaa sana, na akichukua kazi siku anayokwambia fitting unamkuta anakungoja
@rosemofuga8101
@rosemofuga8101 Жыл бұрын
MB zangu haziendagi bure
@ashurashabani7249
@ashurashabani7249 Жыл бұрын
Tunaomba kipendi kinacho fuata chidi benzi
Хасанның өзі эфирге шықты! “Қылмыстық топқа қатысым жоқ” дейді. Талғарда не болды? Халық сене ме?
09:25
Демократиялы Қазақстан / Демократический Казахстан
Рет қаралды 332 М.
Cook with Wema Sepetu - S06E06 Martin Kadinda
8:46
Wema Sepetu
Рет қаралды 24 М.
Pesa imejificha katika vitu vinne - Sheikh Walid Alhad
20:37
Kalamutz
Рет қаралды 115 М.