Serikali Yashindwa Kuikataa au Kuikubali Taarifa Yake.Ni Kuhusu Kuongeza Maeneo ya Hifadhi Kaskazini

  Рет қаралды 13,238

The Chanzo

The Chanzo

2 ай бұрын

Mjadala mkali umeibuka Bungeni leo Juni 03,2024, kufuatia Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka kuuliza msimamo wa serikali kuhusu nyaraka iliyovuja inayoonesha mapendekezo ya kubadili maeneo ya wafugaji Kaskazini kuwa mapori tengefu.
Nyaraka hiyo imeendelea kuzua gumzo kubwa katika jamii za wafugaji hasa kutokana na sehemu kubwa ya Ardhi inayopendekezwa kufanywa hifadhi.
Akijibu hoja ya Ole Sendeka Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki alieleza kuwa suala hilo sio rasmi.
"Nyaraka hiyo ambayo anaitaja haipo mezani kwangu, haijatolewa na chombo rasmi kwa hiyo nilikua naomba wala tusiizungumzie kwa sababu tunazidi kuleta taharuki kwa wananchi. Mheshimiwa Spika taratibu za kiserikali zinajulikana,namna ya kutenga maeneo kama mapori tengefu zinajulikana, kama itafika wakati huo na tathmini hiyo itakuwa inaendelea basi taratibu za kiserikali rasmi zitafanya kazi," alieleza Kairuki
Hata hivyo Ole Sendeka alionesha kutokuridhika na kutaka majibu Zaidi kutoka serikalini.
"Namheshimu sana Waziri, lakini wa kweli Mheshimiwa Waziri kwanza niseme sipokei taarifa na sipokei kwa sababu moja, mchakato ulipoanza ulianzia Bungeni kufuatia taarifa ya Waziri katika bajeti ya 2021/22 ya kupandisha hadhi mapori hayo, wakaenda kutuma timu za wataalamu zimekuja katika Wilaya zetu," alieleza Ole Sendeka.
"Watalamu Wameleta taarifa, bahati mbaya taarifa yao ilipoletwa kwa Waziri ikavuja na taarifa hiyo ni hii hapa. Taarifa hiyo wananchi wote wanayo, tukijifanya hatuioni inatuharibia kura katika ukanda wa Kaskazini. Kwa sababu taarifa wananchi wanayo na bahati mbaya taarifa sio nzuri inapendekeza maeneo karibu yote ya wafugaji katika wilaya hizo zibadilishwe ziwe mapori tengefu,"
Mjadala uliendelea huku Ole Sendeka akiitaka serikali iikatae taarifa hiyo, jambo ambalo halikufanyika.

Пікірлер: 40
@EliaoniTerry
@EliaoniTerry Ай бұрын
Tuache longolongo, waziri ajibu maswali ya timu iliundwa au haikuundwa,? Ukweli ni kwamba kuna hila inafanyika, na kwa ukweli nikwamba mhe Ole sendeka yuko sahihi. Ccm acheni kuiuza nchi hii.
@deogratiusmaila676
@deogratiusmaila676 Ай бұрын
CCM , kumbe Mheshimiwa Rais wa mioyo ya watu Lisu yuko sahihi
@walidmgonja3644
@walidmgonja3644 Ай бұрын
Duh!choko unachekesha wewe.Tayari ushamuita shoga rais wa moyo wako😅😅😅
@bonnymakuke3153
@bonnymakuke3153 Ай бұрын
​@@walidmgonja3644choko ni wewe na ukoo wako Sasa kosa lake hapo ni lipi!! Kwani uongo lisu ndo rais wa mioyo ya watu kama umeumia pita kule
@LemayanOlesenet-mq2yl
@LemayanOlesenet-mq2yl Ай бұрын
Hii taarifa ipo,msitufiche
@user-nf1tg3kt3y
@user-nf1tg3kt3y Ай бұрын
Wabunge na spika wote ni wapumbavu wasiojitambua lakini olesendeka yupo Sahihi kabisa Hawa CCM ni majambazi wote yaani kesi ya nyani unaipeleka kwa ngedere utashinda kweli
@user-zk9ox3di4b
@user-zk9ox3di4b 27 күн бұрын
asante sana ndugu yangu ole sendeka tegemeo letu wamassai wote atutakubali kamwe
@LemayanOlesenet-mq2yl
@LemayanOlesenet-mq2yl Ай бұрын
Tumeshapata taarifa ya Olesendeka CCM,kuna haja ya kuwaacha kbs
@seifsaidseifsaid1210
@seifsaidseifsaid1210 Ай бұрын
Huyu hafai kuwa waziri alishafeli toka wakati wa magufuri
@RamatLonjumuya
@RamatLonjumuya Ай бұрын
Serikali ya kitapeli
@salumbujjo2320
@salumbujjo2320 Ай бұрын
Serikali imeoza hiyo kama msajili wa vyama nimzalendo ni bora angefuta cha cha ccm ili kunusulu vizazi vijavyo
@carolakinasha2106
@carolakinasha2106 Ай бұрын
Ashe Olesendeka. Asante Oloing'oni
@paull8659
@paull8659 Ай бұрын
Serikali ya majambazi..
@davidmalogo7100
@davidmalogo7100 Ай бұрын
Yani olesendeka mungu akulinde mana yani wewehapo nisawa naswala upo kwenye kundi la simba sikumoja uje ujiuzulu ubunge kwasauti mbeleyabunge nakusema sitaki ubunge kwasababu yakuza maeneo yawamasai
@The1979bornagain
@The1979bornagain Ай бұрын
Hivi inawezekana kuna uhuni unafanyika ndani ya serikali kuhujumu wananchi? Presentation ya waziri inaonesha wazi kuna tatizo serikalini na kuna incompetence ndani ya wizara ya Maliasili. Mfano kuna uhusiano gani kwa waziri kuingia mwezi wa tisa na uhuni unaoendelea wizarani kwake? Ina maana hakukufanyika makabidhiano ya yeye aliyeingia na aliyetoka? Hakukabidhiwa hili?
@user-mj2te4dy7q
@user-mj2te4dy7q Ай бұрын
Kama jambo Hilo halipo watu wanahamishwa kwanini na wanajeshi wanajenga nyumba acheni zarau tutakutana kwenye kura tunawapiga chini upigaji umezidi na Hela zinawatia viburi mmeshiba 😂😂
@feiswalsalim2117
@feiswalsalim2117 Ай бұрын
mhashimiawa bado serikali haija na wew ndio serkali unamanishaa niji mhaeshimiwa
@georgekimasaofficial1629
@georgekimasaofficial1629 Ай бұрын
Kumbe ndiyo maana mnabinafsisha mali za watanzania bila watanzania wenye Mali kujuwa pia tumeona taarifa kuwa Kuna mikataba imeingiwa na serikali na inchi ya Korea kusini kuhusu mbandali zetu na madini sjui hili lipo vipi.
@KasangaKalanga-vo6od
@KasangaKalanga-vo6od Ай бұрын
Swala lipo acheni ngonjera, waziri hafai
@holyspiritpropheticministr3687
@holyspiritpropheticministr3687 Ай бұрын
Nchi hii mbona mnatuabisha ,just straight answer but people playing politics ,You people need to wake up and tunahitaji hili taifa tuanze kuamka usingizini
@ombenijady8409
@ombenijady8409 Ай бұрын
Kaz unayo spika 😅
@mahengedaktari-ek8go
@mahengedaktari-ek8go Ай бұрын
Safi sana spika
@simongwandu7392
@simongwandu7392 Ай бұрын
Mnaiuwa CCM waziwazi
@LoataMollel
@LoataMollel 26 күн бұрын
Aenda wapi
@LoataMollel
@LoataMollel 24 күн бұрын
Asitaafu aende wapi
@lomunyaklesikar
@lomunyaklesikar Ай бұрын
Hapo hakuna Haji ya kweli ebu ole sendeka ako sawa
@ernestmayonjo8424
@ernestmayonjo8424 Ай бұрын
Mawazili wanajibu vizuli lakini hilijambolipo kwasababu Kila wilaya linafanyamipango ya vyanzo vya mapato kwahiyo itapataje mapato ndiyo wanatenga maeneo nayo wanapata mapato kuwatoza wananchi kamavile wavuvi nk
@simongwandu7392
@simongwandu7392 Ай бұрын
Nani aliandika serikali isidanganye imesainiwa na nani
@onessytiganga4722
@onessytiganga4722 Ай бұрын
Wataalamu wamevujisha tayari
@evelynmwaimu-vd9jo
@evelynmwaimu-vd9jo Ай бұрын
Aibu
@evelynmwaimu-vd9jo
@evelynmwaimu-vd9jo Ай бұрын
Hiyo ni geresha report wanaijua
@feiswalsalim2117
@feiswalsalim2117 Ай бұрын
aslm samahani kubadisha hathi kivi namba nifahamu mnatua jia gani kubafila hathi
@WazaeliStefano
@WazaeliStefano Ай бұрын
Kwanini mnaanza na kusifia kwanza halafu mnatiriri lawama kibao
@ThomasSaigarai
@ThomasSaigarai Ай бұрын
Kwaya nalasi
@saruni5673
@saruni5673 Ай бұрын
Bora nikae kimya
@happyjeremiahmhuli4043
@happyjeremiahmhuli4043 Ай бұрын
Ooooo
@user-jl5uh1xq9f
@user-jl5uh1xq9f Ай бұрын
Kimbembe mungeni
@user-nf1tg3kt3y
@user-nf1tg3kt3y Ай бұрын
Mavi kabisa
@liberatuceboniphace4004
@liberatuceboniphace4004 Ай бұрын
Spika yupo makini sana
@gwaluganosaiba629
@gwaluganosaiba629 Ай бұрын
Ole sendeka umefikia umri wa kustaaf
Самый Молодой Актёр Без Оскара 😂
00:13
Глеб Рандалайнен
Рет қаралды 12 МЛН
Clowns abuse children#Short #Officer Rabbit #angel
00:51
兔子警官
Рет қаралды 79 МЛН
Spot The Fake Animal For $10,000
00:40
MrBeast
Рет қаралды 178 МЛН
JUSSA AFICHUA SIRI NZITO YA MUUNGANO
34:06
AL FATAH TV ONLINE
Рет қаралды 56 М.
MDUDE AKIELEZA YALIYO MSIBU AKIWA MIKONONI MWA POLISI
52:26
Mwanzo TV Plus
Рет қаралды 9 М.
Самый Молодой Актёр Без Оскара 😂
00:13
Глеб Рандалайнен
Рет қаралды 12 МЛН