Рет қаралды 160
Wizara ya Afya imesema kuwa bado inajipanga katika utoaji wa huduma za Toto Afya Kadi lakini haikueleza ni lini mpango huo utakamilika ingawa watoto wanaendelea kupata huduma kupitia vifurushi maalumu.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Mei 27,2024 na Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Ulyankulu Rehema Migilla.
Kwenye Swali lake mbunge huyo amehoji ni lini Serikali itarudisha mfumo wa Toto Afya Kadi ambao uliondolewa licha ya kuwa na msaada mkubwa kwa wananchi hasa watoto. Migilla pia amehoji kwa nini Hospitali kubwa zinadai barua za rufaa ili kuwahudumia watoto chini ya miaka mitano ambao matibabu yao yanaelezwa ni bure.
Naibu Waziri amesema mpango wa Toto Afya Kadi umebadirika na sasa watoto wanahudumiwa kupitia utaratibu wa shule na vifurushi vya Bima ya Afya vya najali,Wekeza na Timiza ambavyo wanajiunga kupitia wazazi wao.